USTAARABU kwenye NYUMBA ZA KUPANGA......!

USTAARABU kwenye NYUMBA ZA KUPANGA......!

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Posts
12,271
Reaction score
1,069
Jamani salama lakini?..

Awali ya yote tutakiane heri ya mwaka mpya wa 2013...!


Ndugu wana-jf naamini kabisa kuna watu humu jamvini wana maisha ya kawaida kabisa ya kitanzania ambayo hata mim ninaishi...!kwamba kuna watu tunaishinyumba za kupanga ambazo unakuta kuna facilities ambazo mnafanya costs sharing ikiwemo umeme,maji,kulipia watu wa kutoa taka,n.k...

Sasa kuna baadhi wa wapangaji wenzetu wamekuwa na tabia za ajabu sana zinazoashiria kukosa ustaarabu kabisa...!kwamba inapofika muda sahihi wa kuchanga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kukabiliana na bills mbali mbali wao huanza mbinu mbinu zisizo na tija...mara mtu anaanza kurudi usiku mnene na kujihimu kuondoka....mara mtu anakuja na kauli ya 'sina hela' mpaka mwisho wa mwezi.....!mara anakuwa mkali...!lakin the same person ndiye anayeungurumisha hita na majiko ya umeme 24/7...halafu huyo huyo unakuta ana bustani ya mchicha uwanjani...

Sasa mimi nashindwa kuelewa kwamba kuna ugumu gani wa kuyapangilia maisha yako na familia yako ukiwa unajua uwepo wa hizi gharama?....kwanini lakini kuna watu hapa tunapoishi wanatukwaza sana...anasababisha tuwe tunalipa penalties kila mwezi!......


LEO NINAOMBA TUJADILIANE NAMNA YA KUISHI KWA USTAARABU KWENYE NYUMBA ZA KUPANGA....kwa sababu haya maisha usipokuwa pro-active kwenye nyumba ya mwenzio utawezaje kumanage bills kwenye nyumba yako?.....

Tusaidiane jamani
 
Heri ya mwaka mpya kaka, mara nyingi wanaofanya hivyo ni makusudi tu ili mpate adha tu ya penalties alafu yeye ndio anakuwa wakwanza kulalamika umeme/maji yakikatwa, ina kera sana.
 
halafu kila siku anarudi amelewa,hata kama ofa ndo upewe wewe kila siku!!!!inaudhi sana,watu wengine hawajaumbwa na aibu,.kuna mshkaji wangu flani yeye chumbani kwake kuna main switch(sijui ndo switch board),sasa asiyelipa bill anamkatia umeme laini yake
 
Tuongezee hapo hapo kaka mkubwa ( heri ya mwaka mpya nawe, uwe wa heri desemba tuhamie kwenye pagale letu mwaya). Kuna na wababa nao hawanaa hela ya kuacha home afu wanadai walipewa ofa. Yaani mwanaume anatembeza kengele halipi bill ya maji, ya umeme, hanunui msosi you end up wondering kama angezaliwa mpunga tukatengeneza mchele na vibibi!

Kiujumla ni tabia ya ubinafsi tu, fulk stop! Hata bar kuna mkaka ama mdada anafanya wenzie ndo kama wazazi wake. Yaani bill ikija yeye anachokoroa meno tuu! Kha!

Kaka pole mwaya. 'Hata kwetu wapo' ukuburudishe saa hii yenye machungu hadi january iishe manake ni mtafutano!
 
Kiujumla ni tabia ya ubinafsi tu, fulk stop! Hata bar kuna mkaka ama mdada anafanya wenzie ndo kama wazazi wake. Yaani bill ikija yeye anachokoroa meno tuu! Kha!

hahahahahahahahah!
 
Watu wanakera sana kwenye nyumba za kupanga hususa ni unapokuja mgawanyo wa bills, mtu anakuletea vijisababu vya hapa na pale angali anazo hela za kukupatia ili muachane salama.

Nadhani watu hao hupenda sana kufatwafatwa na kusumbuliwa na maneno ndo akulipe hizo bills, muda mwingine eti hutaka uone umuhimu wake mahali hapo, INAKERA SANA.

hebu fikiria mtu anakataa kulipa bills za nyumbani lakina Bar unazilipa bila shida yoyote.
 
Kwa kweli inakera sanaaaaaaaaaaa, kiasi unaweza ukapigana,maana kila ukimwambia mwenzio kuwa mchange mnunue umeme mwingi anakujibu yeye hana pesa, sasa mm nazichuma wapi? kwa kweli niliamua kujiwekea Luku yangu mwenyewe, kwa sasa sina matatizo hayo tena, watajijua huko wao wenyewe.
 
'...on ma side a coin haz 2 sides i.e wen u laf ur neiba z cryn labda cku imekataa may b tuwape MUDA kwa sera za chama!'
 
inakera sana, au ndo ile unadaiwa bili ya umeme na wakati hukuwepo mwezi mzima, tena kwa kuongezea hapo na wale wenye nyumba wa kudai kodi ht kabla ya wakati nao wanaboa na kukera sana.

 
Bila hivo huwezi jenga!

Huo ni ukumbusho fanya hima utafute chako, inakera lakini ni muhimu sana (Mimi imenisaidia sana hii)
 
mmh, yaani nakuchukiaje?

Una vijembe vya chini chini sana, ila nimekukubali.

Tuongezee hapo hapo kaka mkubwa ( heri ya mwaka mpya nawe, uwe wa heri desemba tuhamie kwenye pagale letu mwaya). Kuna na wababa nao hawanaa hela ya kuacha home afu wanadai walipewa ofa. Yaani mwanaume anatembeza kengele halipi bill ya maji, ya umeme, hanunui msosi you end up wondering kama angezaliwa mpunga tukatengeneza mchele na vibibi!

Kiujumla ni tabia ya ubinafsi tu, fulk stop! Hata bar kuna mkaka ama mdada anafanya wenzie ndo kama wazazi wake. Yaani bill ikija yeye anachokoroa meno tuu! Kha!

Kaka pole mwaya. 'Hata kwetu wapo' ukuburudishe saa hii yenye machungu hadi january iishe manake ni mtafutano!
 
Si bora hiyo ya kwako. Kuna jamaa mmoja yeye pesa anatoa ila kila akirudi usiku umeme haujanunuliwa. Amechoka mpaka amefikia kutaka kununua luku yake mwenyewe.
 
Heri ya mwaka mpya na wewe pia.
Nyumba ya kupanga bana inataka mkutane walau wetu wenye kufanana kwa tabia, vinginevyo usumbufu ni lazima mkuu.

Nakumbuka mimi nilikuwa naishi sinza nilipoanza kujenga kimya kimya sikulipa umeme wala maji wala hela ya kuzoa takataka,
wakanishtaki kwa mama mwenye nyumba, siku anakuja kwenye kesi ndo siku nahama, nikampa maneno mazuri tu kuwa nikipata hela nitalipa chukua namba yangu ya simu, (wakati huo nilikuwa bado sijamjua Mungu vizuri), mwisho wa yote niliwaachia deni wenye nyumba kwa kuwa nilikuwa nakaa nyumba nzima ya uwani.
 
halafu kila siku anarudi amelewa,hata kama ofa ndo upewe wewe kila siku!!!!inaudhi sana,watu wengine hawajaumbwa na aibu,.kuna mshkaji wangu flani yeye chumbani kwake kuna main switch(sijui ndo switch board),sasa asiyelipa bill anamkatia umeme laini yake
wenye nyumba wengine ni wenda wazimu akiondoka anazima main switch hata kama ushalipia
 
Kuna mmoja anakaa hapa sistu du wa nguvu ukimfuata anakuongelesha vienglish afu kuanzia kesho yake full kukununia,mjini hapa tumekuja kutafuta mambo ya kulaliana kifedha cio kabisa
 
Jamani salama lakini?..

Awali ya yote tutakiane heri ya mwaka mpya wa 2013...!


Ndugu wana-jf naamini kabisa kuna watu humu jamvini wana maisha ya kawaida kabisa ya kitanzania ambayo hata mim ninaishi...!kwamba kuna watu tunaishinyumba za kupanga ambazo unakuta kuna facilities ambazo mnafanya costs sharing ikiwemo umeme,maji,kulipia watu wa kutoa taka,n.k...

Sasa kuna baadhi wa wapangaji wenzetu wamekuwa na tabia za ajabu sana zinazoashiria kukosa ustaarabu kabisa...!kwamba inapofika muda sahihi wa kuchanga kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kukabiliana na bills mbali mbali wao huanza mbinu mbinu zisizo na tija...mara mtu anaanza kurudi usiku mnene na kujihimu kuondoka....mara mtu anakuja na kauli ya 'sina hela' mpaka mwisho wa mwezi.....!mara anakuwa mkali...!lakin the same person ndiye anayeungurumisha hita na majiko ya umeme 24/7...halafu huyo huyo unakuta ana bustani ya mchicha uwanjani...

Sasa mimi nashindwa kuelewa kwamba kuna ugumu gani wa kuyapangilia maisha yako na familia yako ukiwa unajua uwepo wa hizi gharama?....kwanin lakikuna watu hapa tunapoishi wanatukwaza sana...anasababisha tuwe tunalipa penalties kila mwezi!......


LEO NINAOMBA TUJADILIANE NAMNA YA KUISHI KWA USTAARABU KWENYE NYUMBA ZA KUPANGA....kwa sababu haya maisha usipokuwa pro-active kwenye nyumba ya mwenzio utawezaje kumanage bills kwenye nyumba yako?.....

Tusaidiane jamani

Kuna MIJITU kwa asili ni FREE RIDERS!!! Yaani akipata gharama yoyote inayotakiwa kuchangiwa lazima atafute kutochangia, na ikishindikana kabisa walau achangie kidogo saaana!!!! NI TABIA ya baadhi ya watu!!!

Utashangaa akiwa na kwake, gharama zisizokwepeka atalipa kama kawaida!!! Labda tuu jamii imguse kwenye kuchangia kutengeneza barabara, kusomba uchafu...NDIYO MAJIRANI WATAJUA USHENZI WA TABIA ZAKE!!!
 
Heri ya mwaka mpya na wewe pia.
Nyumba ya kupanga bana inataka mkutane walau wetu wenye kufanana kwa tabia, vinginevyo usumbufu ni lazima mkuu.

Nakumbuka mimi nilikuwa naishi sinza nilipoanza kujenga kimya kimya sikulipa umeme wala maji wala hela ya kuzoa takataka,
wakanishtaki kwa mama mwenye nyumba, siku anakuja kwenye kesi ndo siku nahama, nikampa maneno mazuri tu kuwa nikipata hela nitalipa chukua namba yangu ya simu, (wakati huo nilikuwa bado sijamjua Mungu vizuri), mwisho wa yote niliwaachia deni wenye nyumba kwa kuwa nilikuwa nakaa nyumba nzima ya uwani.

avatar yako haifanani na unayozungumza.
 
Kunasiku moja luku ilikata mjrngoni kwetu ulipopitishwa mchango wapangaji wakaanza ohh mbona umeme tumenunua juzi umeishaje haraka hivi

Kuona watu wanasuasua kuchanga mimi nikajitolea nikawapa pesa za kununua umeme utakaotufikisha mwisho wa mwezi, alafu ndo mchango upite kama kawaida kwa maana tulikuwa tunachanga kila mwisho wa mwezi.


Kutoa pesa ikawa shida, badala ya kunishukuru wakaanza kuniteta etin mimi ndo nimeutumia umeme vibaya ndo maana nimetoa pesa.

Nilipozipata news nikawaulizas wote wakaruka. oka siku hiyo sijawahi jipendekeza na wanajutia

Sometime ukiona watu hawaeleweki kuwa kauzu kimtindo
 
Back
Top Bottom