Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Wakuu,
Hivi karibuni nilihudhuria kikao cha wabunge wa Afrika mashariki kilichohusu utawala bora. Huko nilipata fursa ya kukutana Mtoto wa Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi ambaye pia ni mbunge wa Afrika Mashariki. Kikao hicho kiliongozwa na m/kiti na mbunge wa afrika mashariki kutoka Burundi.
Wakati wa majadiliano niliibua hoja nyingi ya kuonesha udhaifu wa serikali ktk kutekeleza utawala bora. Mojawapo ya hoja hizo ni kuhusu watoto wa wakubwa kupewa fursa ya uongozi serikalini na ktk nafasi za kisiasa isivyo halali, jambo ambalo ni kinyume na utawala bora. Hoja yangu hiyo ilimuibua Mbunge Mwinyi na kulazimika kuijibu. Mh. mwinyi alisema huwa ninapokuwa kwenye vikao kama hivi huwa sijibu hoja kama hizi moja kwa moja lakini hii nalazimika kuijibu kuweka rekodi sawa ila akasisitiza kwa upande wa familia yake tu - Rais mstaafu Mwinyi. Baada ya kikao tulilazimika kuendeleza mjadala huo kwa ufupi wakati wa chakula cha mchana + wadau wengine.
Majibu yake kwa ujumla ya kutetea watoto wa vigogo kupata vyeo vikubwa ni kama haya yafuatayo.
Kwanza alisema ktk familia yao ( Rais Ali Hasan Mwinyi) walioko ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm ni yeye na Kaka yake Husein Mwinyi (waziri) tu, kati ya watoto 8 au 9 hivi (Idadi kamili imenitoka) Japo hakusema wale wengine wana nafasi gani na wapi? Kwa hiyo, katika upendeleo huo wao hawapo.
Pili, akasema watoto wa viongozi kama watanzania wengine nao wana haki ya kupata fursa hizo, ila tu wawe na uwezo wa kufanya shughuli hizo na akasema mimi na kaka yangu Husein kazi tuliyopewa tunaiweza na hatujapendelewa. sote tulipigiwa kura na kupata ubunge (kaka pia ni mbunge)
Tatu, alisisitiza kwamba kwa kawaida watoto wa wachunguji hupenda kazi za wazazi wao - uchungaji. Vivyo hivyo, watoto wa Mashekh nao ni mashekh. kwa mantiki hiyo ni kawaida sana kwa mtoto wa Rais kutamani siasa, siyo kawaida kutoipenda. Akasema hata kule Amerika Gorge Bush (mstaafu) ni mtoto wa Rais.
Clinton naye alikaribia kuipata nafasi ya mumewe nk. mifano ni mingi duniani.
Nne, mtoto wa kiongozi si tu kwamba anaipenda siasa lakini pia anajifunza mbinu, mikakati na kila aina ya mahitaji yatakayomfanikisha yeye kufanikiwa kama baba yake. Na mtoto Rais au kiongozi mkubwa anakuwa amejifunza kutoka kwa mhusika mwenyewe (horse Mouth) ambaye amefanikiwa mpaka kufikia kiwango cha juu. Hivyo, inategemewa kuwa mtoto wa Rais atakuwa na mafunzo mengi au uzoefu mwingi wa kufanikiwa ktk nafasi za kisiasa kama baba yake aliyefikia mafanikio ya juu sana, hivyo mtoto wa mwanasiasa mkubwa ana nafasi kubwa ya kufanikiwa.
My take;
Hoja hii nimeileta baada ya kuona listi inayozungushwa ktk simu na JF ya vigogo 13 waliowapenyeza watoto wao ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm (japo sijathibitisha ukweli wa listi hiyo).
Je huu utetezi unatosha kutetea watoto wa vigogo waliojaa ktk nafasi za serikali na siasa? Bado nakumbuka listi ya watoto wa vigogo benki kuu?
Pamoja na kwamba nilimbana kwa BMW(baba, mama na Watoto) ya JK ktk siasa hakutaka kuwatetea specific leaders japo alitoa maelezo hayo ya jumla tu kama hapo juu.
Naomba kuwasilisha.