Uso kwa uso na mtoto wa Rais Mwinyi (mbunge wa A/M)utetezi wake kuhusu watoto wa vigogo na vyeo

Hivi makongoro Nyerere akisema nichagueni kwa sababu nitafanya vizuri kama nyerere baba yangu ni kosa? Mimi nadhani tatizo ni kubwa zaidi ya watoto. Watz pia wanapenda kufuata upepo wa majina makubwa bila kujali kama majina hayo yameleta faida gani kwetu kama Taifa.
Michael p paweda kwenye nafasi kama hizi ni kosa kwa sababu watu wanamjua Nyerere na wanajua utendaji wake
Kwa nini usipambane kama wewe ufanye kile ambacho unajua kitakuwa kwenye uwezo wangu badala ya kutumia umaarufu wa mtu mwingine kujitafutia kura
Yeye alikuw ana uwezo wake na hata kwa dawa huwezi kuufikia
Huwezi kufikia umaarufu wa mtu ila wewe una umaarufu wako na utumie kupata kile unachotaka na sio kuutumia wa mtu mwingine
 
Last edited by a moderator:
Hivi makongoro Nyerere akisema nichagueni kwa sababu nitafanya vizuri kama nyerere baba yangu ni kosa? Mimi nadhani tatizo ni kubwa zaidi ya watoto. Watz pia wanapenda kufuata upepo wa majina makubwa bila kujali kama majina hayo yameleta faida gani kwetu kama Taifa.
Michael p aweda kwenye nafasi kama hizi ni kosa kwa sababu watu wanamjua Nyerere na wanajua utendaji wake

Ukweli husemwa:

Mimi naona kama vile mlikuwa mnapoteza muda tu kwa malipo ya raslimali za mlalahoi wa Tanzania.

Samahani, lakini kwa mtu mwenye hekima, usingepoteza muda wako kumuuliza swali na kumsikiliza 'mtuhumiwa wa rushwa ya kutumia nafasi ya Baba katika jamii kupata kazi' ukategemea atakupa jibu mwafaka.

Halafu tulivyo na akili zilizofungwa na ukoloni mamboleo, eti kwa vile familia ya Bush alifanya hivyo basi ni halali hata kwa Watanzania.

Halafu eti katika wanane au tisa tuko wawili tu kwenye siasa. kwani hiyo ni idadi ndogo?. Halafu tatizo siyo kuwa kwenye siasa, Tatizo ni nafasi zao kwenye siasa. kama ni hivyo, kwa nini hakuamua tu kuwa katibu tawi au kata wa CCM na akaishia hapo. kwa nini nafasi ya juu kisiasa? UBUNGE NA UWAZIRI
 
Nafikiri ahali yangu mtoa mada inabidi ujupanga na kufunguka zaidi.

Mimi sioni ajabu kwa hilo kwani Mtoto wa nyoka siku zote anakuwa nyoka.

Nitakupa mifano michache sana
1. Mtoto wa Khalfan Ngasa (aliyekuwa mchezaji wa Pamba Mwanza ni Mrisho Ngasa mchezaji wa Simba
2. Mtoto wa John Tegete aliyekuwa mchezaji na sasa kocha wa Toto Afr naye ni mchezaji wa wa Young Africans Jerry tegete
3. Ukoo wa akina Matumla ambao ni wapiganaji ngumi
4. kama utamjua Pprofesa Austin Shaba mtoto wake pia alikuwa Dr
5. Lakin hata Mimi mwenyewe kati ya watoto wangu 6 wawili ni wachumi kama mimi na watatu ni wanasharia kama mama yao.

Hilo si jambo la ajabu.
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa, Kama haki inatendeka katika kupata nafasi hizo.
Likija swala la Dr. Hussein Mwinyi na uwazili, basi angefuata nyayo za Baba yake kuwajibika punde makosa yatokeapo. Mabomu Mbagala & Gongolamboto, migomo ya Madaktari X2.
Likija swala la Ridhiwani, kupita bila kupingwa, wakati sehemu nyingine wagombea wametishiana bunduki? huko ni kubebwa
Ukiangalia uwezo wa Nape katika nafasi ya juu aliyokuwa nayo, ameshindwa na anapwaya. It seems like he doesn't know his job period. Kabebwa.
Wapo wengi hawana uwezo kabisa, tena weupe, bila ya kamba hawawezi kuvuka mto
 
Hapo ndipo ninaposema waTanzania ni lazima mfunguke mawazo na kuona mbali sana.

labda nikuulize JE ILI KUWA KIONGOZI WA KISIASA HUKO TANZANIA UNAHITAJI UWE NA ILMU KWA KIASI GANI. Mimi ninavyojua zamani ilikuwa mtu kujua kusoma na kuandika.

Suala la pili, Je hao watoto hawajafikia kiwango hicho bali wamependelewa?

nasubiri majibu yako hapa kabla sijaendelea kukudarsisha zaidi

Mkuu Barubaru bado tunaona mbali na bado tuna safari ndefu sana kwenye kufikia unakotaka wewe tukuamini kuwa tunataka kufikia
Biashara ya kujua kusoma na kuandika ni kigezo ila kujua unagombea uongozi ili iweje na unataka nini na kuwafanyia nini wananchi wako ambao unaenda kuwatumikia kigezo ambacho hakuna anayekifanyia kazi zaidi ya kutafuta maslahi binafsi zaidi na kutafuta sehem ya kupata yale wao wanayoyaona yana manufaa kwao zaidi
Kuutafuta umaarufu kwa maana ya kusema kuwa mimi ni mtoto wa fulani nitafanya kama baba au mama yangu anayoyafanya kwenye uongozi wake hicho ni zaidi ya kupendelewa nmaana tunawasikia wengine wanatumia majina ya kiongozi fulani kuwa nimetumwa na fulani nije nigombee (refer UWT)
Kama unataka uongozi simama pale upambane kama wewe na wala usitumie jina wala sifa za mtu mwingine kupambana
 
Last edited by a moderator:
Hivi makongoro Nyerere akisema nichagueni kwa sababu nitafanya vizuri kama nyerere baba yangu ni kosa? Mimi nadhani tatizo ni kubwa zaidi ya watoto. Watz pia wanapenda kufuata upepo wa majina makubwa bila kujali kama majina hayo yameleta faida gani kwetu kama Taifa.

Makongoro atakuwa mjinga kusema hivyo. Watu wanauelewa utofauti wa uwezo wake na wa baba yake, vilevile kwa Ridhiwani na hao Mamwinyi......
 
Si kosa ndio maana Makongoro alipata heshima sana kugombea Ubunge Arusha (na sio Butiama) kupitia NCCR ingawa angeupata pia kama angegombea kupitia CCM. Tatizo lililopo ni pale utitiri wa wagombeaji unapojidhihirisha kushabihiana na wasimamia uchaguzi

Kwa maoni yangu, tatizo la ccm ni la kimfumo zaidi. Wameweka mfumo unawawezesha watoto wa wakubwa kupenya humo humo kwa kufuata utaratibu waliojiwekea ambao walalahoi hawawezi kupenya. lakini kwa maelezo ya huyo bwana kwa kuwabana kwamba wamevunja sheria ni ngumu kiasi fulani kuwabana.
Tatizo ni kwamba wao ndo waliojitengenezea taratibu hizo.
Kwa mfano. Kwenye mchujo wa nafasi za kupigiwa kura hufanya yafuatayo.
a)Kutumia ushawishi wao kuwaambia wapinzani wao wa ndani ya chama kujitoa - mfano mzuri ni BMW.
b) kupitishwa na mtu ambaye ni dhaifu ili ushinde kura ya maoni mifano ni mingi.
 
Nikiwa specific, labda niulize je, Salma Kikwete angewania ujumbe wa NEC ya Magamba iwapo mumewe asingekuwa Rais? I mean, aliwahi kweli kufikiria kuingia kwenye siasa akiwa anafundisha primary school kule Kawe? Na je, angepita bila kupingwa kule Lindi iwapo mume wake asingekuwa mwenyekiti wa taifa wa Magamba? Nini kimemsukuma huyu ex-primary school teacher (tena nasikia alianzia Grade C), kugombea ujumbe wa NEC?
 
Mkuu Barubaru bado tunaona mbali na bado tuna safari ndefu sana kwenye kufikia unakotaka wewe tukuamini kuwa tunataka kufikia
Biashara ya kujua kusoma na kuandika ni kigezo ila kujua unagombea uongozi ili iweje na unataka nini na kuwafanyia nini wananchi wako ambao unaenda kuwatumikia kigezo ambacho hakuna anayekifanyia kazi zaidi ya kutafuta maslahi binafsi zaidi na kutafuta sehem ya kupata yale wao wanayoyaona yana manufaa kwao zaidi
Kuutafuta umaarufu kwa maana ya kusema kuwa mimi ni mtoto wa fulani nitafanya kama baba au mama yangu anayoyafanya kwenye uongozi wake hicho ni zaidi ya kupendelewa nmaana tunawasikia wengine wanatumia majina ya kiongozi fulani kuwa nimetumwa na fulani nije nigombee (refer UWT)
Kama unataka uongozi simama pale upambane kama wewe na wala usitumie jina wala sifa za mtu mwingine kupambana

lakin kumbuka mwisho wa yote kwa anaegombea uongozi na kura kutoka kwa wananchi/ wanachama.

sasa suala hapa linarudi kwa wananchi/ wanachama wanaowachagua na si mtoto wa kigogo.

Kumbuka hata watu wa Mara wamembwaga mtoto wa muasisi wa CCM huko Tanzania. makongoro Nyerere.

nafikiri mna kazi kubwa kwa kuwaelimisha wanachama wenu kuwa mtu anachaguliwa kutokana na utashi na uongozi wake kwa jamii na sio kwa nasaba yake.

Poleni sana
 
Hebu niambie utashi alonao DR HUSSEIN MWINYI unaomwezesha kuchaguliwa bila influence ya baba yake au waliopata kunufaika na urais wa baba yake. Unamjua Advocate Fatuma Karume? unajua yuko wapi kikazi?......IMMA Advocates na sihitaji kukwambia hawa ni akina nani........ila ujue na Ridhiwani aliwahi kuwa huko pia
 
Michael p aweda kwenye nafasi kama hizi ni kosa kwa sababu watu wanamjua Nyerere na wanajua utendaji wake
Kwa nini usipambane kama wewe ufanye kile ambacho unajua kitakuwa kwenye uwezo wangu badala ya kutumia umaarufu wa mtu mwingine kujitafutia kura
Yeye alikuw ana uwezo wake na hata kwa dawa huwezi kuufikia
Huwezi kufikia umaarufu wa mtu ila wewe una umaarufu wako na utumie kupata kile unachotaka na sio kuutumia wa mtu mwingine

Nakubaliana na wewe.
Inavyotakiwa ni kosa kubwa sana ila kwa hali halisi kisiasa inakuwa kinyume chake, na hiyo ndo tatizo la mfumo wetu.
 
Kwa nchi za wenzetu mambo yanafanyika kiuwazi ingawa na faulo zinatokea kama nduguye Bush aliyekuwa Gavana alimvyomsaidia kushinda urais.Lakini kwa nchi za kiafrika mambo ni tofauti mtu anapokuwa kiongozi lazima familia yake pia ijiingize kwenye uongozi tumeona Uganda,Libya na nchi nyingine hivi Mwinyi asingekuwa rais unafikiri mtoto wake angeacha udoktari na kuingia kwenye siasa.Nani alimjua January Makamba kabla baba yake hajawa katibu mkuu wa ccm
sasa hivi kuna vyeo vinatolewa kulipana fadhila hasa haya mambo ya kujenga mtandao wa kuingia ikulu yalipoanza ni heri tungekuwa na usultani ikajulikana moja na hata Aman Karume hakufikia vigezo vilivyowekwa kwa mgombea urais kupitia cc lakini vilibadilishwa makusudi hali hii si tu imeondoa umoja tuliokuwa nao bali pia imejenga chuki kwani hao watoto wengine wa vigogo tulisoma nao na uwezo wao tunautambua toka tukiwa mashuleni ndio maana tunahoji inakuwaje leo wapate hizi nyazifa nzito serikalini
 
Nikiwa specific, labda niulize je, Salma Kikwete angewania ujumbe wa NEC ya Magamba iwapo mumewe asingekuwa Rais? I mean, aliwahi kweli kufikiria kuingia kwenye siasa akiwa anafundisha primary school kule Kawe? Na je, angepita bila kupingwa kule Lindi iwapo mume wake asingekuwa mwenyekiti wa taifa wa Magamba? Nini kimemsukuma huyu ex-primary school teacher (tena nasikia alianzia Grade C), kugombea ujumbe wa NEC?
Vivyo hivyo kwa Hussein Mwinyi. Huyu tuliambiwa alisomea udaktari, lakini kadri nijuavyo hajawahi hata siku moja kufanya kazi hospitali. Badala yake tukasikia amegombea ubunge na kuteuliwa kuwa waziri. Experience ya utawala: zero.
Ila tu ana jina la Mwinyi na baba yake aliwahi kuwa rais.
 
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa, Kama haki inatendeka katika kupata nafasi hizo.
Likija swala la Dr. Hussein Mwinyi na uwazili, basi angefuata nyayo za Baba yake kuwajibika punde makosa yatokeapo. Mabomu Mbagala & Gongolamboto, migomo ya Madaktari X2.
Likija swala la Ridhiwani, kupita bila kupingwa, wakati sehemu nyingine wagombea wametishiana bunduki? huko ni kubebwa
Ukiangalia uwezo wa Nape katika nafasi ya juu aliyokuwa nayo, ameshindwa na anapwaya. It seems like he doesn't know his job period. Kabebwa.
Wapo wengi hawana uwezo kabisa, tena weupe, bila ya kamba hawawezi kuvuka mto

Nakubaliana na wewe, Kwa kiwango kikubwa, sijui walishindaje chaguzi zao, lakini Mwinyi waziri anatakiwa awe ameshajiuzulu muda mrefu kwa kauli yake ya kusema mabomu hayatalipuka tena halafu yakalipuka tena gongo la Mboto. ( mdogo wake A/M) naye sijui performance kwenye Bunge hilo. Time will tell.
 
Nikiwa specific, labda niulize je, Salma Kikwete angewania ujumbe wa NEC ya Magamba iwapo mumewe asingekuwa Rais? I mean, aliwahi kweli kufikiria kuingia kwenye siasa akiwa anafundisha primary school kule Kawe? Na je, angepita bila kupingwa kule Lindi iwapo mume wake asingekuwa mwenyekiti wa taifa wa Magamba? Nini kimemsukuma huyu ex-primary school teacher (tena nasikia alianzia Grade C), kugombea ujumbe wa NEC?

Nafikiri JK ndo kazidi kabisa. BMW yake ni hatari kwa ccm. Ukiangalia uwezo wao, utagundua kuwa majina yamewapitisha isivyo halali.
 
Hebu niambie utashi alonao DR HUSSEIN MWINYI unaomwezesha kuchaguliwa bila influence ya baba yake au waliopata kunufaika na urais wa baba yake. Unamjua Advocate Fatuma Karume? unajua yuko wapi kikazi?......IMMA Advocates na sihitaji kukwambia hawa ni akina nani........ila ujue na Ridhiwani aliwahi kuwa huko pia

Mara ningi siwezi na nasipendi kujadili watu. Lakin Dr Hussein Mwinyi ana utashi mkubwa ndio maana alichaguliwa kuwa mbunge wa Mkuranga kabla kuvuka maji na kuchaguliwa mjini unguja. Pasi na shaka yoyote ana mvuto mkubwa sana kwa wapiga kura wake na ndio maana akachaguliwa.

Kama utajiepusha na utumwa wa akili wa kuona KUWA NI DHAMBI KUBWA KWA MTOTO WA KIGOGO KUGOMBEA UONGOZI na kujali uwezo na utashi wa uongozi wa jamii utakuwa umejitenga sana na dhambi ya ubaguzi kwa watoto wa vigogo.

Mimi nakushauri angalia vigezo na maamuzi yote yanabaki kwa wapga Kura ambao ndio wanaomchagua au kumbwaga.

Pole sana
 
Kimsingi, linapokuja suala la Ubunge au teuzi nyengine za kidemokrasia, hatupaswi kuwalaumu watoto wa vigogo hata kidogo, badala yake tunapaswa kujilaumu sisi wananchi tunaowachagua; kwamba tunapumbazwa na majina (iwapo hana uwezo)

Kwa nafasi za kuteuliwa au kupachikwa, tatizo halikomi kwenye CCM tu. CCM wanaongoza, lakini na CHADEMA hawapo nyuma. Wanawake wa viti maalum bungeni kwa vyama vyote viwili wanathibitisha uozo huo ulipo.

Misho wa yote, tunarudi kule kule kuwa mwenye kuweza kubadili hili ni mwananchi.
 
Michael p aweda kwenye nafasi kama hizi ni kosa kwa sababu watu wanamjua Nyerere na wanajua utendaji wake
Kwa nini usipambane kama wewe ufanye kile ambacho unajua kitakuwa kwenye uwezo wangu badala ya kutumia umaarufu wa mtu mwingine kujitafutia kura
Yeye alikuw ana uwezo wake na hata kwa dawa huwezi kuufikia
Huwezi kufikia umaarufu wa mtu ila wewe una umaarufu wako na utumie kupata kile unachotaka na sio kuutumia wa mtu mwingine

Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa lakini sivyo ilivyo. Je, tufanye nini ili turudishe nchi kwenye reli?
 
lakin kumbuka mwisho wa yote kwa anaegombea uongozi na kura kutoka kwa wananchi/ wanachama.

sasa suala hapa linarudi kwa wananchi/ wanachama wanaowachagua na si mtoto wa kigogo.

Kumbuka hata watu wa Mara wamembwaga mtoto wa muasisi wa CCM huko Tanzania. makongoro Nyerere.

nafikiri mna kazi kubwa kwa kuwaelimisha wanachama wenu kuwa mtu anachaguliwa kutokana na utashi na uongozi wake kwa jamii na sio kwa nasaba yake.

Poleni sana

mkuu Barubaru hapo kwenye bolod sorry mimi sijui unaongelea wanachama wa nini maana mimi siongelei chama
Na hebu jaribu kusoma hapo juu nimeshasema wanachama wa vyma vyote na sijabagua chama
Kuna wanachama wanaowapigia kura na hapo ni kujua walikuwa wanawaza nini wakati wanawachagua hao watu je ni nasaba au ni kule kuwa aliyechaguliwa ana vigezo vinavyompa nafasi hiyo
Na wale waliopita bila kupingwa je wanastahili hizo nafasi au watu waliogopa kupambana na mgombea wakajitoa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom