Uso kwa uso na mtoto wa Rais Mwinyi (mbunge wa A/M)utetezi wake kuhusu watoto wa vigogo na vyeo

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,
Hivi karibuni nilihudhuria kikao cha wabunge wa Afrika mashariki kilichohusu utawala bora. Huko nilipata fursa ya kukutana Mtoto wa Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi ambaye pia ni mbunge wa Afrika Mashariki. Kikao hicho kiliongozwa na m/kiti na mbunge wa afrika mashariki kutoka Burundi.

Wakati wa majadiliano niliibua hoja nyingi ya kuonesha udhaifu wa serikali ktk kutekeleza utawala bora. Mojawapo ya hoja hizo ni kuhusu watoto wa wakubwa kupewa fursa ya uongozi serikalini na ktk nafasi za kisiasa isivyo halali, jambo ambalo ni kinyume na utawala bora. Hoja yangu hiyo ilimuibua Mbunge Mwinyi na kulazimika kuijibu. Mh. mwinyi alisema huwa ninapokuwa kwenye vikao kama hivi huwa sijibu hoja kama hizi moja kwa moja lakini hii nalazimika kuijibu kuweka rekodi sawa ila akasisitiza kwa upande wa familia yake tu - Rais mstaafu Mwinyi. Baada ya kikao tulilazimika kuendeleza mjadala huo kwa ufupi wakati wa chakula cha mchana + wadau wengine.

Majibu yake kwa ujumla ya kutetea watoto wa vigogo kupata vyeo vikubwa ni kama haya yafuatayo.

Kwanza alisema ktk familia yao ( Rais Ali Hasan Mwinyi) walioko ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm ni yeye na Kaka yake Husein Mwinyi (waziri) tu, kati ya watoto 8 au 9 hivi (Idadi kamili imenitoka) Japo hakusema wale wengine wana nafasi gani na wapi? Kwa hiyo, katika upendeleo huo wao hawapo.

Pili, akasema watoto wa viongozi kama watanzania wengine nao wana haki ya kupata fursa hizo, ila tu wawe na uwezo wa kufanya shughuli hizo na akasema mimi na kaka yangu Husein kazi tuliyopewa tunaiweza na hatujapendelewa. sote tulipigiwa kura na kupata ubunge (kaka pia ni mbunge)

Tatu, alisisitiza kwamba kwa kawaida watoto wa wachunguji hupenda kazi za wazazi wao - uchungaji. Vivyo hivyo, watoto wa Mashekh nao ni mashekh. kwa mantiki hiyo ni kawaida sana kwa mtoto wa Rais kutamani siasa, siyo kawaida kutoipenda. Akasema hata kule Amerika Gorge Bush (mstaafu) ni mtoto wa Rais.
Clinton naye alikaribia kuipata nafasi ya mumewe nk. mifano ni mingi duniani.

Nne, mtoto wa kiongozi si tu kwamba anaipenda siasa lakini pia anajifunza mbinu, mikakati na kila aina ya mahitaji yatakayomfanikisha yeye kufanikiwa kama baba yake. Na mtoto Rais au kiongozi mkubwa anakuwa amejifunza kutoka kwa mhusika mwenyewe (horse Mouth) ambaye amefanikiwa mpaka kufikia kiwango cha juu. Hivyo, inategemewa kuwa mtoto wa Rais atakuwa na mafunzo mengi au uzoefu mwingi wa kufanikiwa ktk nafasi za kisiasa kama baba yake aliyefikia mafanikio ya juu sana, hivyo mtoto wa mwanasiasa mkubwa ana nafasi kubwa ya kufanikiwa.

My take;
Hoja hii nimeileta baada ya kuona listi inayozungushwa ktk simu na JF ya vigogo 13 waliowapenyeza watoto wao ktk nafasi za kisiasa kupitia ccm (japo sijathibitisha ukweli wa listi hiyo).

Je huu utetezi unatosha kutetea watoto wa vigogo waliojaa ktk nafasi za serikali na siasa? Bado nakumbuka listi ya watoto wa vigogo benki kuu?

Pamoja na kwamba nilimbana kwa BMW(baba, mama na Watoto) ya JK ktk siasa hakutaka kuwatetea specific leaders japo alitoa maelezo hayo ya jumla tu kama hapo juu.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni lazima ajitetee, na kinadharia yuko sahihi. Lakini practically, ushahidi una-suggest otherwise. BOT watoto wa vigogo wamejaa - na wengi wao hata basic qualifications hawana (rejea kesi ya kugushi vyeti na kujipatia kazi kwa kutumia vyeti hivyo, ila sijui imeisha au bado inaendelea). Mifano ipo mingi, huwezi kuniambia hao wote wanasifa!
 
Ndio mwisho wake wa kufikiri, hivi nyerere angewachukua walimpatie fedha wakati wanadai uhuu, hao akina mwinyi wangefika hapo?
 
Ni lazima ajitetee, na kinadharia yuko sahihi. Lakini practically, ushahidi una-suggest otherwise. BOT watoto wa vigogo wamejaa - na wengi wao hata basic qualifications hawana (rejea kesi ya kugushi vyeti na kujipatia kazi kwa kutumia vyeti hivyo, ila sijui imeisha au bado inaendelea). Mifano ipo mingi, huwezi kuniambia hao wote wanasifa![/QUOTE

Suala la BOT sijui walipotezea wapi.
 
Mkuu Mikael P Aweda utetezi wake lazima ufikie hapo na lazima ajitetee kujionyesha kuwa yuko sahihi na wala hakuna kosa na lazima awatetee na wengine kuwa wanalolifanya liko sahihi kabisa
Ila hatuwezi kutetea kuwa ni lazima mtoto wako afanye kazi unayoifanya wewe baba yake kwa maana kama baba ni mwanasheria na mtoto ni lazima awe mwanasheria hiyo hapana kuna sehem hizo mambo zinakataa
Walikuwa wapi wakati baba yao hajawa kiongozi wakapigana wenyewe bila kutumia kufahamika kwa baba kujiingiza kwenye siasa
hatutetei sio CCM pekee hata vyama vingine
Kama wanataka nafasi wapambane bila kutumia umaarufu wa mtu yoyote
Alichokisema kinamtetea na ni katika kujitetea wala hatuwezi kumpinga kwa hilo ila kasi kwa sasa inaongezeka sana na ni katika kuonyesha kwamba kuna kingine wanachopigania kama kulinda maslahi ya familia zaidi
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri cha kutambua hapa si kwamba watu wanalalamika kwamba mtoto wa kiongozi asiwe na yeye kiongozi,hapana!,swala ni kwamba anatumia jina la mzazi wake kupata hiyo nafasi!.Kama mzee mkubwa,mtoto na mama wamepita,na hawajapita kihalali,wametumia jina la mkuu.Hilo ndo linalalamikiwa,inatakiwa kwenye uchaguzi wowote kuwe na fair play.
 
Nafikiri ahali yangu mtoa mada inabidi ujupanga na kufunguka zaidi.

Mimi sioni ajabu kwa hilo kwani Mtoto wa nyoka siku zote anakuwa nyoka.

Nitakupa mifano michache sana
1. Mtoto wa Khalfan Ngasa (aliyekuwa mchezaji wa Pamba Mwanza ni Mrisho Ngasa mchezaji wa Simba
2. Mtoto wa John Tegete aliyekuwa mchezaji na sasa kocha wa Toto Afr naye ni mchezaji wa wa Young Africans Jerry tegete
3. Ukoo wa akina Matumla ambao ni wapiganaji ngumi
4. kama utamjua Pprofesa Austin Shaba mtoto wake pia alikuwa Dr
5. Lakin hata Mimi mwenyewe kati ya watoto wangu 6 wawili ni wachumi kama mimi na watatu ni wanasharia kama mama yao.

Hilo si jambo la ajabu.
 
Hiyo mifano yako inalingana vipi na siasa? Kwani watoto wako wanapigiwa kura kuwa wachumi kama wewe au wanakaa darasani? Unjua kwa nini jamii nyingi zilikataa usultani na ufalme? Ntakwambia ni kwa sababu ya kufanya automativc power transfer ambayo si sahihi! Yule mama na mwanaye wamepita huko walikogombea bila kupingwa wewe mtoto wako alikuwa mchumi bila mtihani? I will be supriesed if you say yes.

Je unajuwa Mwinyi kamfadhili mangapi Kikwete kisiasa na Kikwete asijibu shukrani?
 
Nafikiri ahali yangu mtoa mada inabidi ujupanga na kufunguka zaidi.

Mimi sioni ajabu kwa hilo kwani Mtoto wa nyoka siku zote anakuwa nyoka.

Nitakupa mifano michache sana
1. Mtoto wa Khalfan Ngasa (aliyekuwa mchezaji wa Pamba Mwanza ni Mrisho Ngasa mchezaji wa Simba
2. Mtoto wa John Tegete aliyekuwa mchezaji na sasa kocha wa Toto Afr naye ni mchezaji wa wa Young Africans Jerry tegete
3. Ukoo wa akina Matumla ambao ni wapiganaji ngumi
4. kama utamjua Pprofesa Austin Shaba mtoto wake pia alikuwa Dr
5. Lakin hata Mimi mwenyewe kati ya watoto wangu 6 wawili ni wachumi kama mimi na watatu ni wanasharia kama mama yao.

Hilo si jambo la ajabu.

Barubaru hatukatai kwao kuwa wanasiasa kama baba zao au mama zao
tatizo ni kuwa wametumia njia gani kufikia hapo
Je jina la baba limewanyanyua au walipambana wao kama wao kupata nafasi
Watoto wako wamesoma na wamepambana na hawakutumia kufahamika kwako wewe kupata nafasi au kufaulu masomo yao. Walisoma na kufaulu si kwa kuwa wana jina kama lako wakapata upendeleo au wakawaambia maprof wao na Lecturers wao kuwa aise sisi ni watoto wa Barubaru na tunahitaji kufaulu
Hao unaosema tunahoji njia zilizotumika na wengine unaona wamepita bila kupingwa kwa sababu ya majina yao tuu
nani asiyejipenda akapambane na mtoto wa fulani ambaye anagombea
hapo ndipo tunaona kuwa mambo sio sawa kabisa
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri cha kutambua hapa si kwamba watu wanalalamika kwamba mtoto wa kiongozi asiwe na yeye kiongozi,hapana!,swala ni kwamba anatumia jina la mzazi wake kupata hiyo nafasi!.Kama mzee mkubwa,mtoto na mama wamepita,na hawajapita kihalali,wametumia jina la mkuu.Hilo ndo linalalamikiwa,inatakiwa kwenye uchaguzi wowote kuwe na fair play.

Je, ni kosa mtoto kutumia umaarufu wa baba kupata nafasi. Mbona ccm wanatumia jina la Mwl Nyerere kupata kura? Kama mtu akisema mim ni mtoto wa x aliyefanya vizuri ktk cheo y. mkinichagua mimi nitafanya vizuri kama baba yangu x kuna ubaya gani?. Am just challenging you?
 
Ukoo wa Mzee rukhusa labda kwenye siasa wanaweza kwani kuna mmoja tulipiga darasa pamoja duuu...ilikuwa kichwa nazi lakini sasa hivi anakula bata
 
Ungemuuliza kwenye uwajibikaji mbona wanakuwa wagumu inapotokea wamefanya uzembe katika nafasi zao kama mabumu ya mbagala na badae gongo la mboto?
Pili watoto wa vigogo hawashitakiki rejea kauli ya magufuli watoto waliojipachika mizani.
 
watoto wa vigogo kikatiba hawana marufuku ya kugombea nafasi za kisiasa
kikubwa ni kujadili uwezo wao katika kuongoza .
Hivi kuna anyehoji utendaji wa January Makamba.
Waulize Vodacom Kama Mwamvita ni incompentent.
Kuzaliwa familia za vigogo si kiroja.
 
Barubaru hatukatai kwao kuwa wanasiasa kama baba zao au mama zao
tatizo ni kuwa wametumia njia gani kufikia hapo
Je jina la baba limewanyanyua au walipambana wao kama wao kupata nafasi
Watoto wako wamesoma na wamepambana na hawakutumia kufahamika kwako wewe kupata nafasi au kufaulu masomo yao. Walisoma na kufaulu si kwa kuwa wana jina kama lako wakapata upendeleo au wakawaambia maprof wao na Lecturers wao kuwa aise sisi ni watoto wa Barubaru na tunahitaji kufaulu
Hao unaosema tunahoji njia zilizotumika na wengine unaona wamepita bila kupingwa kwa sababu ya majina yao tuu
nani asiyejipenda akapambane na mtoto wa fulani ambaye anagombea
hapo ndipo tunaona kuwa mambo sio sawa kabisa

Hivi makongoro Nyerere akisema nichagueni kwa sababu nitafanya vizuri kama nyerere baba yangu ni kosa? Mimi nadhani tatizo ni kubwa zaidi ya watoto. Watz pia wanapenda kufuata upepo wa majina makubwa bila kujali kama majina hayo yameleta faida gani kwetu kama Taifa.
 
Nafikiri ahali yangu mtoa mada inabidi ujupanga na kufunguka zaidi.

Mimi sioni ajabu kwa hilo kwani Mtoto wa nyoka siku zote anakuwa nyoka.

Nitakupa mifano michache sana
1. Mtoto wa Khalfan Ngasa (aliyekuwa mchezaji wa Pamba Mwanza ni Mrisho Ngasa mchezaji wa Simba
2. Mtoto wa John Tegete aliyekuwa mchezaji na sasa kocha wa Toto Afr naye ni mchezaji wa wa Young Africans Jerry tegete
3. Ukoo wa akina Matumla ambao ni wapiganaji ngumi
4. kama utamjua Pprofesa Austin Shaba mtoto wake pia alikuwa Dr
5. Lakin hata Mimi mwenyewe kati ya watoto wangu 6 wawili ni wachumi kama mimi na watatu ni wanasharia kama mama yao.

Hilo si jambo la ajabu.

Barubaru, sina tatizo na mtoto mwenye sifa, lakini huyo anaegushi cheti ana sifa zipi hata astahili kupewa kazi??? Ina maana hakuna wenye sifa stahiki?
 
Hiyo mifano yako inalingana vipi na siasa? Kwani watoto wako wanapigiwa kura kuwa wachumi kama wewe au wanakaa darasani? Unjua kwa nini jamii nyingi zilikataa usultani na ufalme? Ntakwambia ni kwa sababu ya kufanya automativc power transfer ambayo si sahihi! Yule mama na mwanaye wamepita huko walikogombea bila kupingwa wewe mtoto wako alikuwa mchumi bila mtihani? I will be supriesed if you say yes.

Je unajuwa Mwinyi kamfadhili mangapi Kikwete kisiasa na Kikwete asijibu shukrani?[/QUOTE Safari_ni _safari naona umemjibu vyema sana maana hapa anaongelea mambo mawili tofauti
Mimi nikiwa mwalimu na mtoto wangu akasoma na yeye kuwa mwalimu sina shida nae maana amepambana
Ukoo wa akina matumla hawabebwi na yeyote wanapigana uwanjani na wanashida au kushindwa na hawako pale au hakuna refa anayewabeba kuwaambia kwa kuwa nyie ni ukoo wa akina Matumla mtashinda mapambano yenu
Au hawaendi jukwaani kujinadi kuwa sisi ni wa ukoo wa akina Matumla so tunaomba hili pambano tushinde
au hakuna walipopita bila kupigana na kupewa mkanda kisa ni wa ukoo wa Matumla
 
Last edited by a moderator:
Barubaru hatukatai kwao kuwa wanasiasa kama baba zao au mama zao
tatizo ni kuwa wametumia njia gani kufikia hapo
Je jina la baba limewanyanyua au walipambana wao kama wao kupata nafasi
Watoto wako wamesoma na wamepambana na hawakutumia kufahamika kwako wewe kupata nafasi au kufaulu masomo yao. Walisoma na kufaulu si kwa kuwa wana jina kama lako wakapata upendeleo au wakawaambia maprof wao na Lecturers wao kuwa aise sisi ni watoto wa Barubaru na tunahitaji kufaulu
Hao unaosema tunahoji njia zilizotumika na wengine unaona wamepita bila kupingwa kwa sababu ya majina yao tuu
nani asiyejipenda akapambane na mtoto wa fulani ambaye anagombea
hapo ndipo tunaona kuwa mambo sio sawa kabisa

Hapo ndipo ninaposema waTanzania ni lazima mfunguke mawazo na kuona mbali sana.

labda nikuulize JE ILI KUWA KIONGOZI WA KISIASA HUKO TANZANIA UNAHITAJI UWE NA ILMU KWA KIASI GANI. Mimi ninavyojua zamani ilikuwa mtu kujua kusoma na kuandika.

Suala la pili, Je hao watoto hawajafikia kiwango hicho bali wamependelewa?

nasubiri majibu yako hapa kabla sijaendelea kukudarsisha zaidi
 
Je, ni kosa mtoto kutumia umaarufu wa baba kupata nafasi. Mbona ccm wanatumia jina la Mwl Nyerere kupata kura? Kama mtu akisema mim ni mtoto wa x aliyefanya vizuri ktk cheo y. mkinichagua mimi nitafanya vizuri kama baba yangu x kuna ubaya gani?. Am just challenging you?

Si kosa ndio maana Makongoro alipata heshima sana kugombea Ubunge Arusha (na sio Butiama) kupitia NCCR ingawa angeupata pia kama angegombea kupitia CCM. Tatizo lililopo ni pale utitiri wa wagombeaji unapojidhihirisha kushabihiana na wasimamia uchaguzi
 
Ukoo wa Mzee rukhusa labda kwenye siasa wanaweza kwani kuna mmoja tulipiga darasa pamoja duuu...ilikuwa kichwa nazi lakini sasa hivi anakula bata

Nafikiri kama ni kweli hiyo ndo tatizo. Kupeana nafasi za BOT na serikalini wakati mtu hafai kwa lolote. Anapewa kwa vigezo vya rushwa.
 
Back
Top Bottom