Usiyoyajua kuhusu Coco Beach!

Usiyoyajua kuhusu Coco Beach!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,760
Reaction score
3,270
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa mdau wa kutembelea fukwe zetu zilizopo Dar na kwingine upepo unakovuma.story ya leo itagusa matukio ya COCO BEACH!
Tukio la kwanza nimeende Coco na mwenza wangu kula upepo wa bahari yetu ya hindi.nimepark gari.ilikuwa mida ya saa kumi na mbili na nusu,kigiza kinaanza.tukashuka na kwenda pembezoni mwa bahari kuyakaribia maji chumvi. kulikuwa na wadau wengine wanatamalaki hapo pia.

kama kawaida ya wapendanao tulikuwa zero distance busu kwa mbali.tukaamua tukae pembezoni kwenye mawe tukipiga stori za hapa na pale,mara akaja askari hana uniform kajitambulisha na kudai kitendo chetu cha kukaa kwa kukaribiana na kukiss kando ya bahari ni kufanya mapenzi hadharani, nikauliza kivipi? hakuna aliyevua nguo hapo wala kumshika mwenzie.ikawa tumezua zogo.nikamaliza ile tafrani na yule askari.

Tukio la pili nilienda Coco safari nyingine niliamua sasa nikae kwenye gari na mwenza wangu.kosa nililofanya sikufunga milango ya gari.kuna vijana huwa wanapitisha biashara zao pembeni ya gari kama gari ni tinted bado wanapita mbele ya gari na kuchungulia watu walioko kwenye gari kujua kama ni wapenzi na kama mmezama kwenye mahaba hata kama hamfanyi ngono kwenye gari wanaenda kutoa taarifa kwa maaskari.ambao wanakuja kuwakamata na kuwabambikia kesi! siku hiyo walifungua gari na kudai tuna kiss karibu na eneo la waziri mkuu.

pale Coco kuna makazi yake.(sio Majariwa)tukakamatwa mpaka oysterbay kituoni.tulipaki nje askari mmoja aliingia ndani mwingine alibaki nasisi.tulibishana hatimae tukayamaliza.
Mara nyingine ya mwisho tulienda pale Coco beach club.kwenye parking ile nimekaa kidogo wakaja askari watano na siraha zao wanaopatrol kule baharini tukawafungulia milango wakaona hakuna lolote pia tulijibu maswali yao kwa ufasaha na uzoefu wakasepa zao.

kabla hatujaondoka kwakuwa tulikaa kwenye gari mda mrefu tukipiga story na kuagiza tunachotaka na kula kwenye gari wakatokea askari wengine wawili wenye uniform tofauti na wa mwanzo wakawa wanapiga mahesabu ya kutuzingira na kufungua milango ya gari na kushtukiza kama kuna chochote kinafanyika.niliona mchezo mzima kwenye site/driving mirror.mmoja alianza kutambaa(craw) kulijia gari letu.

kwakuwa mda wote nikiwa kwenye gari huwa nakuwa makini na linakuwa limewashwa.nikaliondoa kwa kasi.sijawahi rudi tena kule labda nikiwa na hamu ya mishikaki ya Samaki kwa kipara ndio naenda na kuacha gari mbali na nikiwa peke yangu.

Fundisho ukiwa na gari popote lock milango yake pia elewa ukiwa COCO Beach na mwenza chukua tahadhali vinginevyo unaweza kugeuzwa mradi na polisi wetu.pia usiwaamini wale wauza biashara wanaokujia kwenye gari au pale ulipo kaa wanashirika na askari wa kule.

Wish you a lovely long week end,keep your faith in what you believe.
'
 
Ha ha ha ha haaa! Umenikumbusha mbali sana! Kuna Jamaa Mmoja mwembamba mfupi, kakomaaa sana sura, halafu anavaaa suruali flani Hivi mbwanga Za kushonesha Zina marinda ya kutosha, sometimes anapiga Na tshirt flan Hivi Mpauko yenye Nyuzi legevu! Huyu Jamaa alinifanya nipachukie sana CoCo hasa mchana!

Nina Kama Miaka mi'3 Hivi sijafika coco mchana! Hua naingia pale Anzia Saa tano Usiku!
 
Matatizo mengine ni ya watu wenye hali fulani na economic status fulani za kuwa na magari, sisi wa TZ 11, hayo hayatukuti tena hizo patrol, zinafanywa kwenye fukwe waendazo wenye magari, sisi watu wa madogo kuporomoka kama kwetu Shimo la Udogo, fukwe zetu ni Mtoni Kijichi, huko hakuna patrol ya aina yoyote, mkienda beach na mwezio, kigiza kikianza tuu kuingia watoto wanarudi nyumbani, wakubwa wanabaki ufukweni hadi kujivinjari kwa raha zenu.

Ndio maana mitaa ya uswahilini sana hata guest hakuna!, guest za nini wakati viambaza tuu vinatosha?!.

Utajiri raha lakini pia ni shida na umasikini ni shida ila pia kuna raha zake!.

Pasco
 
Ha ha ha ha haaa! Umenikumbusha mbali sana! Kuna Jamaa Mmoja mwembamba mfupi, kakomaaa sana sura, halafu anavaaa suruali flani Hivi mbwanga Za kushonesha Zina marinda ya kutosha, sometimes anapiga Na tshirt flan Hivi Mpauko yenye Nyuzi legevu! Huyu Jamaa alinifanya nipachukie sana CoCo hasa mchana!

Nina Kama Miaka mi'3 Hivi sijafika coco mchana! Hua naingia pale Anzia Saa tano Usiku!
mkuu kule nakuona kama kituo cha polisi.siamini Raia wala Polisi wa kule! ni nouma.
 
Mode please shift this topic to 'mahusiano/mapenzi it is here by default not design.Thanks.
 
Ahahahhaaahh umeikumbusha mbali sana coco sitapasahau hao maaskari wengine feki mwaka 2009 walitukamata nikiwa na mchuchu wangu wakaanza mkwara aisee tulitoa hela zote tulizokua nazo tukabaki na nauli tu mwisho tukagundua maaskari wale ndo zao wanakamataga wapenzi tu
 
Kuna yule jamaa anafarasi wake pale, Siku moja miaka Hiyo tulichelewa tulikuwa tunapiga picha kwenye yule faras wakaja askali wawili wametangulia wawili wapo nyuma.
Wale wambele wakatupiga biti tuu wakatuambia tumalizie tusepe. Wale waliokuwa nyuma waliofika wakamdaka kwenye farasi wakambananisha wakamchomoa hela nyingi ...na mikwara tele...
Ndio mwisho Wa kwenda koko...
 
Kwani lazima muende bichi ya coco mbona kuna bichi ya Kigamboni na bagamoyo
 
so why coco beach,nenda cine club,kawe club,ama beach za kueleweka.kuna wakati nilikua mteja sana kule kwa wanajeshi kule kawe bia bei chee,kuna siku walimbananisha jamaa kichapo mpaka alikunya.sikwenda tena
 
Ha ha ha ha haaa! Umenikumbusha mbali sana! Kuna Jamaa Mmoja mwembamba mfupi, kakomaaa sana sura, halafu anavaaa suruali flani Hivi mbwanga Za kushonesha Zina marinda ya kutosha, sometimes anapiga Na tshirt flan Hivi Mpauko yenye Nyuzi legevu! Huyu Jamaa alinifanya nipachukie sana CoCo hasa mchana!

Nina Kama Miaka mi'3 Hivi sijafika coco mchana! Hua naingia pale Anzia Saa tano Usiku!
Saa5 usiku? Mweeeeeeee, basi wewe ni bundi mtu tu sasa maana hakuna namna.
 
Sasa kama beach yenyewe ni ya mateso hivyo ni bora tu ibinafsishwe
 
ningerudisha gari nyuma kidogo na kumkanyaga askari vidole kisha nikaondoka...
 
Ahahaa njoo kigamboni ni mchuchu wako kuna beach huku za maana husumbuliwi na mtu fanya unavyotaka.
 
Ha ha ha ha haaa! Usiku pananoga sana pale! Nakaa mpaka Saa saba Au nane then narudi home Au napitia triple 7 Kuona mambo yanaendaje!
Duhhhhh, basi wewe ni sheeedah!!!!
Alafu unapiga vyombo eeeh?!
 
Back
Top Bottom