Old - Hand
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 2,042
- 1,951
Chegu
Ni maumbile mume kupenda mke, na mke kupenda mumeWanasema alikuwa anapenda sana Mademu.
kabla sija uwendea huu uzi nakushukuru sana mkuu kuleta huuzi tena inabidi niache hata kula nipae naoJOHN OKELLO
JANUARI 12 ni siku ya kukumbuka Mapinduzi ya Zanzibar yapata miaka 44 iliyopita. Lakini jambo moja ambalo katika historia ya mapinduzi hayo ni kukosekana kwa mtu muhimu aliyeyashiriki.
Jambo hili linaweza kuwa na mwangwi wa kibaguzi au wa kuwatenga katika kumbukumbu za tukio hilo muhimu lililoondoa utumwa na utwana uliokubuhu visiwani Unguja na Pemba. Mtu huyo ni Field Marshal John Okello.
Mapinduzi.
Kumbukumbu za historia zinaonyesha kuwa Okello aliingia Zanzibar mwaka 1963 na kuwasiliana na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP). Kundi hilo lilikuwa linajipanga kuangalia namna ya kuondoa utawala wa Waarabu.
Akiwa Zanzibar, Okello alikuwa mwanachama wa chama cha wapiga rangi – akiwa anapaka rangi majumba mbalimbali. Wakati wa muda wake wa ziada alikuwa akiunda kikundi kidogo cha askari wa Kiafrika.
Kikundi hiki cha kijeshi kilishika na kufuata amri zilizokuwa zinatolewa Okello kama kiongozi ambazo ni pamoja na kutojihusisha na masuala ya ngono, kutokula nyama mbichi na kutokunywa pombe.
Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini. Aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Pemba.
Usiku mmoja kabla ya mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru kina mama wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.
Uasi
Januari 12, 1964 akiwa anaungwa mkono na asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanakandamizwa – wengi wao wakiwa Waafrika – Okello na kikosi chake waliweza kuingia katika mji wa Stone Town, Zanzibar, kulikokuwa maskani ya Sultan.
Inaelezwa kuwa takriban watu 10,000 waliuawa, licha ya kwamba kikosi cha Okello kilikuwa na silaha duni. Okello na kikosi chake walilishangaza Jeshi la Polisi Zanzibar na kuchukua ofisi zao.
Kwenye hotuba yake iliyotangazwa kwa njia ya redio, Okello alitangaza kuwa yeye ni ‘Field Marshal wa Zanzibar na Pemba’ na alimwamuru Sultan aue familia yake na kisha ajiue mwenyewe, la sivyo Okello ataifanya kazi hiyo mwenyewe.
Hata hivyo, Sultani mwenyewe alikuwa tayari ameshajipatia maficho ya usalama nchini Uingereza, na waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine pia waliwahi kutoroka.
Kuwekwa pembezoni
Kutokana na kufanikiwa kwa mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa waziri mkuu. Baadaye alikuja kuwa Makamu wa Rais.
Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.
Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.
Utata kuhusu kifo chake
Baada ya Okello kupigwa marufuku Zanzibar na Tanganyika, aliishi maisha ya kuhamahama kutoka nchi moja hadi nyingine. Aliishi Kenya na baadaye Congo Kinshasa na Uganda. Aliwahi kufungwa mara kadhaa na mara ya mwisho alionekana akiwa na kiongozi wa Uganda mwaka 1971 na baadaye alipotea.
Katika kitabu cha ‘Revolution on Zanzibar’ kilichoandikwa na Don Petterson inadhaniwa kuwa Idi Amin alimwona Okello kuwa ni tishio kwake na mara nyingine inaelezwa kuwa baada ya Amin kujipandisha cheo na kuwa Filed Marshal, inaelezwa kuwa Okello alisema kwa dhihaka, “Uganda hivi sasa ina Field Marshal wawili.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Idd Amini alipanga mipango ya mauaji dhidi ya Okello, lakini pamoja na hali hiyo kifo chake kimebakia kuwa ni cha utata.
Alikotoka
John Gideon Okello alizaliwa mwaka 1937 wilayani Lango, Uganda. Ni mwanamapinduzi asiye na kifani barani Afrika.
Lakini licha ya kuongoza Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyouondoa utawala wa Sultan Jamshid bin Abdullah na kuwezesha kuanzishwa kwa Jamhuri ya Zanzibar, pia amekuwa hafahamiki sana.
Alianza kuishi maisha ya uyatima akiwa na miaka 11. Alipofikisha umri wa miaka 15 aliondoka nyumbani kwao na kwenda kutafuta ajira katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki.
Kuanzia mwaka 1944 alikuwa amefanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na ukarani, mtunza bustani na mfanyakazi katika idara na shughuli mbalimbali. Hata hivyo, alijifunza kufanya biashara ya kuuza matofali na baadaye alimudu kufanya kazi ya uashi, lakini alikamatwa mjini Nairobi, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa; hata hivyo yeye mwenyewe aliwahi kuelezwa kuwa alikamatwa kutokana na makosa yaliyohusiana na hali ya jinsia. Alifungwa miaka miwili gerezani. Kifungoni ndiko kulikomfanya awe na fikra za kimapindizi.
Mara nyingi umekuwapo uvumi kuwa huenda Okello alikuwa amepata mafunzo yake nchini Cuba, lakini jambo hili halikuwahi kuthibitishwa na Okello mwenyewe.
Mwaka 1959 aliingia kisiwani Pemba katika harakati zake za kutafuta ajira kwenye mashamba ya karafuu, lakini badala yake alijiunga na jeshi la polisi.
Hata hivyo, baadaye alijiunga na Chama cha Afro-Shirazi kilichokuwa kinapinga jamii ya watu wachache kuhodhi uchumi wa Zanzibar na Pemba.
Kuna wengi walifanya mambo yanayofanana na Okello. Miongoni mwao ni Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye mapinduzi ya Cuba licha ya kwamba alikuwa ni mzaliwa wa Argentina.
Leo hii Che Guevara ni jina linalosifika na kuheshimika nchini Cuba kutokana na mchango wake. Haiyumkiniki jina la Okello nalo lingekuwa ni jina la kuheshimika kwenye na kukumbukwa kwenye Mapinduzi ya Zanzibar lakini ndivyo imekuwa sivyo.
salary
A Knight In Tanzania-Journey From Old Ifakara

Hakuna aliyemgeuka mwenzake, Che Guevara alimtaka Komredi Fidel Castro awe Kiongozi wa Cuba punde tu baada ya Mapinduzi matukufu ya 1959.Na upi ukweli kuhusiana na kugeukana baina ya Che Guevara na Fidel Castro baada ya kushika madaraka ya Cuba...?
Niliisoma sehem ila ilikuwa kifupi mno.
ni kweliAnasema ushiriki was Nyerere kwa ukombozi wa Congo ulikuwa mdogo sana
Alikuwa useless kwenye ukombozi wa Congo
Kasome historia yake vizuri mkuuDaaa..yaani hapo ndo huwa ninakumbuka Maneno ya marehemu Remmy "kifoooo...kifoooo...kifo hakina huruma".
Yaani komando na mpiganaji mahiri kabisa anakuja kuuwawa kizembe zembe tena na "askari chapombe". Inasikitisha sana...we kifo huna adabu kabisa.
OK sawa, ila wewe kama ungekuwa nayo hiyo historia yake ungesaidia Ku share nasi hapaKasome historia yake vizuri mkuu
aaaaah mkuuu vipiiiHakuna aliyemgeuka mwenzake, Che Guevara alimtaka Komredi Fidel Castro awe Kiongozi wa Cuba punde tu baada ya Mapinduzi matukufu ya 1959.
Che Guevara alikuwa na majukumu ya kwenda Nchi nyingine kwa ajili ya kufanya ukombozi. Kazi aliyoifanya Cuba ilimtosha hivyo hakutaka wadhifa wowote.
Ila fitna za madaraka, ziliwagombanisha Komredi Fidel Castro na Mwanamapinduzi mwingine wa Cuba, Huber Matos kiasi cha Fidel Castro kumweka Kizuizini Huber Matos.
Ugomvi wa Fidel Castro na Huber Matos ulisababisha kifo tata cha Mwanamapinduzi mwingine Camilo Cienfuegos ambaye baada ya kutumwa na Castro kwenda kumkamata Huber Matos, ndege aliyopanda Camilo wakati akirejea jijini Havana ilipotea na haikuwahi kuonekana tena licha ya kutafutwa kila kona.
Maneno yalizuka kuwa ndege aliyopanda Camilo Cienfuegos itakuwa imelipuliwa na ndege vita za Cuba kwa amri ya Fidel Castro. Che Guevara alijitokeza kupinga tetesi hizo za kuuwawa kwa Camilo na uwepo wa uhusika wa Castro katika sakata hilo.
Kwa leo niishie hapo!!
unamlambisha mtu asali alafu hapo hapo una mwambia tema mate jamanii

Yaah Che Guevara walitofautiana misimamo na Fidel Castro kipind fulani wakati Guevara akiwa waziri ktk serikali ya Castro.....Na upi ukweli kuhusiana na kugeukana baina ya Che Guevara na Fidel Castro baada ya kushika madaraka ya Cuba...?
Niliisoma sehem ila ilikuwa kifupi mno.
Mimi naona hawapo na kama wapo ni wanafiki, wanaojali matumbo yao kwanza.Jamaa alikuwa hatari sana...ila watu kama hawa hujitoa muhanga kwa maisha ya watu na duniani saa hii wamebaki wachache sana
WA sasa hivi hawapoganii maisha ya watu wanyonge bali wanafadhiliwa ili wapore mali za nchi na madaraka.Hata hi Leo wapo ila sasa kuna mbinu mpya na za kileo mapigano ya waasi Wa congo yanafadhiliwa, Sudan kusini Na kwengineko kwa mbinu mbadala na huo alotumia Che Guevara Wa kupigana bega kwa bega na anaowasaidia, na ya sasa hivi ni mabaya zaidi
Mkuu hitler wajerumani na dunia ndio hawataki mwelewa ila ilichangia kwa kiasi kikubwa ecomic reform za ujeruman pamoja na kupunguza kama c kumaliza un employmentAisee kuna baadhi ya binadamu wanaumea kwa sababu ya maisha duni wanayoishi wengine
kuna watu wanaandika majina yao vizuri kama CHE GUEVARA na wengine wanaandika majina yao vibaya kama HITLER