Usiyoyajua kuhusu Che Guevera

Usiyoyajua kuhusu Che Guevera

Yap alifika hadi Ilala kuna mgahawa pale aliwahi kugonga menu mara nyingi tu
Hehehe!ila alifika kwa mondlane hapo mikocheni beach,kama unaingia azura gym...ndani huko kulia kuna Nyumba ambayo mondlane aliuwawa.....
Cheguevara alionekana usiku mnene akitia timu hapo....ishu hyo nlimegewa na Mzee mmoja aliyekuwa anaishi jirani yke....ambapo wakati huo baada ya Tukio la kuuwawa mondlane Mzee wake alichukuliwa naye kwa mahojiano

Ova
 
Shukran sana
 
ukiona nyumba imesimama vizuri ujue kunamsingi imara uliojengwa kabla, ujasiri, misimamo mikali na kujiamini kwa che guevara kumetokana na nature ya watu wa taifa lake la argentina, si watu wabinafsi, hawapendi kuona mtu au kikundi cha watu kikinyanyasa watu wengine, wazalendo, wanapenda usawa katika jamii.

kwaiyo spirit hiyo haikuanzia kwake kulikua na watu kama juan jose casteli, manuel belgrano, william brown na carlos maria de alvear, waliongoza mapambano dhidi ya spanish collonial rule 1810 na hatimaye argentina inakuja kupata uhuru 1816 na hawakuishia apo mapambano yaliendelea adi katika nchi za chile, uruguay na paraguay kuhakikisha nazo zinakua huru na kujitawala. amezaliwa kwenye taifa la wanamapinduzi, amekua kwa wanamapinduzi thats why na yeye ni muumini wa mapinduzi.
 
Aisee kuna baadhi ya binadamu wanaumea kwa sababu ya maisha duni wanayoishi wengine

kuna watu wanaandika majina yao vizuri kama CHE GUEVARA na wengine wanaandika majina yao vibaya kama HITLER
Hitller alikuwa mtu safi asee
 
Wengi wamezoea kuiona picha yake kama alama ya ukombozi na mapinduzi ya kweli lakini ni wachache wanaomjua vizuri. Jina lake halisi anaitwa Ernesto ‘Che’ Guevara, alizaliwa Juni 14, 1928, Rosario, Argentina na yafuatayo ni mambo kumi kumhusu:
47c27697e05c871bd221327e27e0540c.jpg

1. Alikuwa mwanaharakati na mwanamapinduzi aliyezisaidia nchi nyingi kupata uhuru kupitia vita vya msituni, zikiwemo Cuba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji na nyingine nyingi.

2. Licha ya kusumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, aliweza kusafiri sehemu mbalimbali, zikiwemo zenye baridi kali na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kuwasaidia wanyonge.

3. Alisomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires alikohitimu na kupata digrii (shahada) ya udaktari wa binadamu.

4. Akiwa bado anasomea udaktari, alifunga safari kwa kutumia pikipiki ambapo alisafiri umbali wa kilometa 4,500 na baadaye kilometa nyingine 8,000 kutembelea nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini. Hali ya umaskini na ukandamizaji aliyoikuta huko ndiyo iliyomfanya awe mpiganaji wa msituni.

5. Harakati za kwanza za kimapinduzi zilizompa umaarufu, ni pale alipomsaidia Fidel Castro wa Cuba kumpindua Dikteta Fulgencio Batista wa nchi hiyo kupitia vita vya msituni akiwa mkuu wa jeshi.

6. Amewahi kufika Dar es Salaam mwaka 1966 ambapo alikutana na wapigania uhuru wa Msumbiji, Frelimo na kukubaliana kusaidiana kupigania uhuru wa nchi hiyo.

7. Baadaye aliondoka Afrika na kuelekea Bolivia kuendelea na harakati za kumtoa madarakani kiongozi aliyekuwa akitawala kimabavu nchi hiyo, René Barrientos ambapo aliunda jeshi la porini kwa ajili ya kumpindua lakini ikashindikana.

8. Baada ya kushindwa kwa mapinduzi ya Bolivia, Che Guevara alikamatwa eneo liitwalo Yuro baada ya kuzingirwa na wanajeshi wa Bolivia.

9. Baada ya kukamatwa kwake, aliteswa sana na siku chache baadaye akauawa kwa kupigwa risasi nyingi na mwanajeshi mlevi aitwaye Mario Terán.

10. Kufuatia kifo chake, mataifa mengi duniani yalitangaza siku kadhaa za maombolezo, ikiwemo Cuba ambapo Fidel Castro alitangaza siku tatu za maombolezo.
Hiii kauli ya cini ina maana kubwa.
 
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom