Sizani kama wapo...kama wapo utawatafuta kwa tochiHivi siku hizi wapo wanamapinduzi wa aina ya Che? Maana nchi nyingi zimeshaweka kando Ujamaa/Ukomunist!
Mkuu Zanzibar alihusika Field Marshall John Okellomkuu samahan hivi che alihusika mapinduzi ya zanzibar
Haya makinikia ya kwetu wanapenda tu kuweka majina yao kwenye vitu vikubwa vikubwa ambavyo hata hawajafika kusaidia kwa lolote. STUPID IDIOTS!!!!Aisee kuna baadhi ya binadamu wanaumea kwa sababu ya maisha duni wanayoishi wengine
kuna watu wanaandika majina yao vizuri kama CHE GUEVARA na wengine wanaandika majina yao vibaya kama HITLER
Jina lake linatamkwa vipi?Mkuu ongezea na hili,
Jina alilotumia Che kuingia Congo kwa mara hiyo ya pili lilikuwa Ramon Benetiz.
Baada ya Che kujifunza Kiswahili kidogo, alijipa yeye mwenyewe na wenzake hao wawili majina ambayo ingekuwa rahisi kwa Wacongo kuwaita. Dreke, aliyekuwa wa pili baada ya Che, akaitwa Moja, Papi akaitwa Mbili na Che akajiita Tatu.
Aprili 20, siku moja tu baada ya kuwasili, Che na watu wengine 14 wakaondoka Dar es Salaam kwa gari kuelekea Kigoma. Barabara ilikuwa mbaya wakati huo na safari yenyewe ilichukua siku mbili. Kwa mujibu wa maelezo ya kwenye Pasajes, Che na wenzake walipanda boti kupitia Ziwa Tanganyika na kwenda Congo.
Che alikaa katika mapambano ya kumsaidia Kabila dhidi ya majeshi ya Joseph Kasavubu na baadaye Mobutu Sese Seko kwa muda wa miezi saba. Wacuba waliokuwa na Che hawakufanikiwa katika azma yao.
Katika kitabu cha Anderson kuhusu Che nilichokieleza kabla, yaliandikwa mengi kuhusu namna Che alivyoshindwa kutimiza azma yake. Mosi, ni aina ya viongozi ambao aliwakuta Congo ambao hawakuwa wakifanana kitabia na mtu kama Castro.
Wakati akina Castro walipambana katika eneo la milima la Sierra Maestra kila siku bila kutoka, Kabila alionekana kwenye uwanja wa mapambano mara moja tu katika wakati wote ambapo Che alikuwa vitani.
Mara zote Kabila na wenzake walikuwa na udhuru wa kutokuwepo vitani. Wanamapinduzi wa aina ya Kabila walikuwa wakifanya siasa zao kwenye viwanja vya ndege, hoteli za kitalii na majiji makubwa duniani.
Che aliporudi Dar kutoka Congo alilalamika kuhusu wapiganaji wa Kabila. Alisema alivunjika moyo nao kwa vile hawakuwa na maana na kwamba mara nyingi wakivuta bangi tu.
Kama walivyo wanamapinduzi wengine mahiri, Che Guevara pia alikiri makosa yake binafsi kwenye vita hiyo ya Congo ambayo ilishindwa kupata matokeo yaliyotarajiwa.Akiandika katika kitabu chake hicho cha Pasajes de la Guerra Revolucionaria (Congo), Che aliandika.
“Kuna mambo kadhaa ambayo pengine sikuyafanya vizuri kwenye mapambano yale. Labda nilikuwa mkali sana kwa askari wangu. Nilikuwa nikitumia mbinu za adhabu ambazo wakati mwingine si za kawaida kwa askari kama vile kuwashindisha njaa.
“Pili, nilikuwa na uhusiano mzuri na wananchi masikini na askari wa chini kuliko wale wa ngazi za juu. Kasoro ninayoijutia ni kwamba sikujifunza vya kutosha lugha ya Kiswahili na hili lilininyima fursa ya kuwasiliana vizuri na watu wengi zaidi.
“Nimejifunza mengi Congo; yakiwamo makosa ambayo sitaraji kuyarudia. Labda yatakuwepo mengine ambayo nitayarudia na mengine mapya nitakayoyafanya. Sasa nimeamini zaidi kuhusu mapambano haya ya msituni dhidi ya ubeberu kuliko ilivyokuwa kabla.Sitasahau kuhusu kushindwa kwangu huku na mafunzo haya niliyojifunza Congo.
Mario Terán wakati huo alikua ni Mwanajeshi (Sajenti) wa miaka 27 aliyekuwa na tabia ya ulevi (Alcoholic). Alijitolea kumuua Guevara kwa nia ya kulipiza kisasa baada ya wanajeshi wenzake watatu aliokuwa nao kwenye COMBANIA moja (B-Company) (wote waliitwa "Mario") kuuwawa na jeshi lililokuwa likiongozwa na Guevara.
Samahani mkUu Alikua Ni mwanajeshi wa nchi Gani ???Mario Terán wakati huo alikua ni Mwanajeshi (Sajenti) wa miaka 27 aliyekuwa na tabia ya ulevi (Alcoholic). Alijitolea kumuua Guevara kwa nia ya kulipiza kisasa baada ya wanajeshi wenzake watatu aliokuwa nao kwenye COMBANIA moja (B-Company) (wote waliitwa "Mario") kuuwawa na jeshi lililokuwa likiongozwa na Guevara.
Mario Terán alikuwa mwanajeshi wa Bolivia mkuu
Aha ... kwasababu Kuna habari moja niliisoma kuhusu huyu jamaa Nikaona CIA walihusika sana katika mauaji ya huyu mtuMario Terán alikuwa mwanajeshi wa Bolivia mkuu
Hata zamani walikua wachache ila show yao lazima litoke vumbi... [HASHTAG]#leoyasasandiokaleyakesho[/HASHTAG]Jamaa alikuwa hatari sana...ila watu kama hawa hujitoa muhanga kwa maisha ya watu na duniani saa hii wamebaki wachache sana
Mkuu ongezea na hili,
Jina alilotumia Che kuingia Congo kwa mara hiyo ya pili lilikuwa Ramon Benetiz.
Baada ya Che kujifunza Kiswahili kidogo, alijipa yeye mwenyewe na wenzake hao wawili majina ambayo ingekuwa rahisi kwa Wacongo kuwaita. Dreke, aliyekuwa wa pili baada ya Che, akaitwa Moja, Papi akaitwa Mbili na Che akajiita Tatu.
Aprili 20, siku moja tu baada ya kuwasili, Che na watu wengine 14 wakaondoka Dar es Salaam kwa gari kuelekea Kigoma. Barabara ilikuwa mbaya wakati huo na safari yenyewe ilichukua siku mbili. Kwa mujibu wa maelezo ya kwenye Pasajes, Che na wenzake walipanda boti kupitia Ziwa Tanganyika na kwenda Congo.
Che alikaa katika mapambano ya kumsaidia Kabila dhidi ya majeshi ya Joseph Kasavubu na baadaye Mobutu Sese Seko kwa muda wa miezi saba. Wacuba waliokuwa na Che hawakufanikiwa katika azma yao.
Katika kitabu cha Anderson kuhusu Che nilichokieleza kabla, yaliandikwa mengi kuhusu namna Che alivyoshindwa kutimiza azma yake. Mosi, ni aina ya viongozi ambao aliwakuta Congo ambao hawakuwa wakifanana kitabia na mtu kama Castro.
Wakati akina Castro walipambana katika eneo la milima la Sierra Maestra kila siku bila kutoka, Kabila alionekana kwenye uwanja wa mapambano mara moja tu katika wakati wote ambapo Che alikuwa vitani.
Mara zote Kabila na wenzake walikuwa na udhuru wa kutokuwepo vitani. Wanamapinduzi wa aina ya Kabila walikuwa wakifanya siasa zao kwenye viwanja vya ndege, hoteli za kitalii na majiji makubwa duniani.
Che aliporudi Dar kutoka Congo alilalamika kuhusu wapiganaji wa Kabila. Alisema alivunjika moyo nao kwa vile hawakuwa na maana na kwamba mara nyingi wakivuta bangi tu.
Kama walivyo wanamapinduzi wengine mahiri, Che Guevara pia alikiri makosa yake binafsi kwenye vita hiyo ya Congo ambayo ilishindwa kupata matokeo yaliyotarajiwa.Akiandika katika kitabu chake hicho cha Pasajes de la Guerra Revolucionaria (Congo), Che aliandika.
“Kuna mambo kadhaa ambayo pengine sikuyafanya vizuri kwenye mapambano yale. Labda nilikuwa mkali sana kwa askari wangu. Nilikuwa nikitumia mbinu za adhabu ambazo wakati mwingine si za kawaida kwa askari kama vile kuwashindisha njaa.
“Pili, nilikuwa na uhusiano mzuri na wananchi masikini na askari wa chini kuliko wale wa ngazi za juu. Kasoro ninayoijutia ni kwamba sikujifunza vya kutosha lugha ya Kiswahili na hili lilininyima fursa ya kuwasiliana vizuri na watu wengi zaidi.
“Nimejifunza mengi Congo; yakiwamo makosa ambayo sitaraji kuyarudia. Labda yatakuwepo mengine ambayo nitayarudia na mengine mapya nitakayoyafanya. Sasa nimeamini zaidi kuhusu mapambano haya ya msituni dhidi ya ubeberu kuliko ilivyokuwa kabla.Sitasahau kuhusu kushindwa kwangu huku na mafunzo haya niliyojifunza Congo.
Kiasi flani CIA walijaribu kumtafuta ila pia Historia inasema hakuna Mtu aliyekuwa anaogopwa na CIA kama Ernesto Guevara. Philip Agee ambaye alikuwa CIA agent (1957-1968) anasema "There was no person more feared by the company (CIA) than Che Guevara because he had the capacity and charisma necessary to direct the struggle against the political repression of the traditional hierarchies in power in the countries of Latin America"Aha ... kwasababu Kuna habari moja niliisoma kuhusu huyu jamaa Nikaona CIA walihusika sana katika mauaji ya huyu mtu
Sent using Jamii Forums mobile app
Shukrani sana nimekuelewaKiasi flani CIA walijaribu kumtafuta ila pia Historia inasema hakuna Mtu aliyekuwa anaogopwa na CIA kama Ernesto Guevara. Philip Agee ambaye alikuwa CIA agent (1957-1968) anasema "There was no person more feared by the company (CIA) than Che Guevara because he had the capacity and charisma necessary to direct the struggle against the political repression of the traditional hierarchies in power in the countries of Latin America"
Karibu mkuu