Usiyoyajua kuhusu Che Guevera

Usiyoyajua kuhusu Che Guevera

Wengi wamezoea kuiona picha yake kama alama ya ukombozi na mapinduzi ya kweli lakini ni wachache wanaomjua vizuri. Jina lake halisi anaitwa Ernesto ‘Che’ Guevara, alizaliwa Juni 14, 1928, Rosario, Argentina na yafuatayo ni mambo kumi kumhusu:
47c27697e05c871bd221327e27e0540c.jpg

1. Alikuwa mwanaharakati na mwanamapinduzi aliyezisaidia nchi nyingi kupata uhuru kupitia vita vya msituni, zikiwemo Cuba, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Msumbiji na nyingine nyingi.

2. Licha ya kusumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, aliweza kusafiri sehemu mbalimbali, zikiwemo zenye baridi kali na kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya kuwasaidia wanyonge.

3. Alisomea udaktari katika Chuo Kikuu cha Buenos Aires alikohitimu na kupata digrii (shahada) ya udaktari wa binadamu.

4. Akiwa bado anasomea udaktari, alifunga safari kwa kutumia pikipiki ambapo alisafiri umbali wa kilometa 4,500 na baadaye kilometa nyingine 8,000 kutembelea nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini. Hali ya umaskini na ukandamizaji aliyoikuta huko ndiyo iliyomfanya awe mpiganaji wa msituni.

5. Harakati za kwanza za kimapinduzi zilizompa umaarufu, ni pale alipomsaidia Fidel Castro wa Cuba kumpindua Dikteta Fulgencio Batista wa nchi hiyo kupitia vita vya msituni akiwa mkuu wa jeshi.

6. Amewahi kufika Dar es Salaam mwaka 1966 ambapo alikutana na wapigania uhuru wa Msumbiji, Frelimo na kukubaliana kusaidiana kupigania uhuru wa nchi hiyo.

7. Baadaye aliondoka Afrika na kuelekea Bolivia kuendelea na harakati za kumtoa madarakani kiongozi aliyekuwa akitawala kimabavu nchi hiyo, René Barrientos ambapo aliunda jeshi la porini kwa ajili ya kumpindua lakini ikashindikana.

8. Baada ya kushindwa kwa mapinduzi ya Bolivia, Che Guevara alikamatwa eneo liitwalo Yuro baada ya kuzingirwa na wanajeshi wa Bolivia.

9. Baada ya kukamatwa kwake, aliteswa sana na siku chache baadaye akauawa kwa kupigwa risasi nyingi na mwanajeshi mlevi aitwaye Mario Terán.

10. Kufuatia kifo chake, mataifa mengi duniani yalitangaza siku kadhaa za maombolezo, ikiwemo Cuba ambapo Fidel Castro alitangaza siku tatu za maombolezo.
Umejuaje sijayajua na mimi nimesoma kitabu cha Jon Lee Anderson "Che Guevara: A Revolutionary Life" kilipotoka tu na kufuatilia habari hizi kwa miaka mingi?

che-is-a-biography-of-ernesto-che-guevara-by-jon-lee-anderson-D9CJM9.jpg
 
JOHN OKELLO

JANUARI 12 ni siku ya kukumbuka Mapinduzi ya Zanzibar yapata miaka 44 iliyopita. Lakini jambo moja ambalo katika historia ya mapinduzi hayo ni kukosekana kwa mtu muhimu aliyeyashiriki.
Jambo hili linaweza kuwa na mwangwi wa kibaguzi au wa kuwatenga katika kumbukumbu za tukio hilo muhimu lililoondoa utumwa na utwana uliokubuhu visiwani Unguja na Pemba. Mtu huyo ni Field Marshal John Okello.
Mapinduzi.

Kumbukumbu za historia zinaonyesha kuwa Okello aliingia Zanzibar mwaka 1963 na kuwasiliana na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP). Kundi hilo lilikuwa linajipanga kuangalia namna ya kuondoa utawala wa Waarabu.
Akiwa Zanzibar, Okello alikuwa mwanachama wa chama cha wapiga rangi – akiwa anapaka rangi majumba mbalimbali. Wakati wa muda wake wa ziada alikuwa akiunda kikundi kidogo cha askari wa Kiafrika.
Kikundi hiki cha kijeshi kilishika na kufuata amri zilizokuwa zinatolewa Okello kama kiongozi ambazo ni pamoja na kutojihusisha na masuala ya ngono, kutokula nyama mbichi na kutokunywa pombe.

Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini. Aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Pemba.
Usiku mmoja kabla ya mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru kina mama wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.
Uasi
Januari 12, 1964 akiwa anaungwa mkono na asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanakandamizwa – wengi wao wakiwa Waafrika – Okello na kikosi chake waliweza kuingia katika mji wa Stone Town, Zanzibar, kulikokuwa maskani ya Sultan.
Inaelezwa kuwa takriban watu 10,000 waliuawa, licha ya kwamba kikosi cha Okello kilikuwa na silaha duni. Okello na kikosi chake walilishangaza Jeshi la Polisi Zanzibar na kuchukua ofisi zao.
Kwenye hotuba yake iliyotangazwa kwa njia ya redio, Okello alitangaza kuwa yeye ni ‘Field Marshal wa Zanzibar na Pemba’ na alimwamuru Sultan aue familia yake na kisha ajiue mwenyewe, la sivyo Okello ataifanya kazi hiyo mwenyewe.
Hata hivyo, Sultani mwenyewe alikuwa tayari ameshajipatia maficho ya usalama nchini Uingereza, na waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine pia waliwahi kutoroka.
Kuwekwa pembezoni
Kutokana na kufanikiwa kwa mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa waziri mkuu. Baadaye alikuja kuwa Makamu wa Rais.
Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.
Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.
Utata kuhusu kifo chake
Baada ya Okello kupigwa marufuku Zanzibar na Tanganyika, aliishi maisha ya kuhamahama kutoka nchi moja hadi nyingine. Aliishi Kenya na baadaye Congo Kinshasa na Uganda. Aliwahi kufungwa mara kadhaa na mara ya mwisho alionekana akiwa na kiongozi wa Uganda mwaka 1971 na baadaye alipotea.
Katika kitabu cha ‘Revolution on Zanzibar’ kilichoandikwa na Don Petterson inadhaniwa kuwa Idi Amin alimwona Okello kuwa ni tishio kwake na mara nyingine inaelezwa kuwa baada ya Amin kujipandisha cheo na kuwa Filed Marshal, inaelezwa kuwa Okello alisema kwa dhihaka, “Uganda hivi sasa ina Field Marshal wawili.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Idd Amini alipanga mipango ya mauaji dhidi ya Okello, lakini pamoja na hali hiyo kifo chake kimebakia kuwa ni cha utata.
Alikotoka
John Gideon Okello alizaliwa mwaka 1937 wilayani Lango, Uganda. Ni mwanamapinduzi asiye na kifani barani Afrika.
Lakini licha ya kuongoza Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyouondoa utawala wa Sultan Jamshid bin Abdullah na kuwezesha kuanzishwa kwa Jamhuri ya Zanzibar, pia amekuwa hafahamiki sana.
Alianza kuishi maisha ya uyatima akiwa na miaka 11. Alipofikisha umri wa miaka 15 aliondoka nyumbani kwao na kwenda kutafuta ajira katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki.
Kuanzia mwaka 1944 alikuwa amefanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na ukarani, mtunza bustani na mfanyakazi katika idara na shughuli mbalimbali. Hata hivyo, alijifunza kufanya biashara ya kuuza matofali na baadaye alimudu kufanya kazi ya uashi, lakini alikamatwa mjini Nairobi, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa; hata hivyo yeye mwenyewe aliwahi kuelezwa kuwa alikamatwa kutokana na makosa yaliyohusiana na hali ya jinsia. Alifungwa miaka miwili gerezani. Kifungoni ndiko kulikomfanya awe na fikra za kimapindizi.

Mara nyingi umekuwapo uvumi kuwa huenda Okello alikuwa amepata mafunzo yake nchini Cuba, lakini jambo hili halikuwahi kuthibitishwa na Okello mwenyewe.
Mwaka 1959 aliingia kisiwani Pemba katika harakati zake za kutafuta ajira kwenye mashamba ya karafuu, lakini badala yake alijiunga na jeshi la polisi.
Hata hivyo, baadaye alijiunga na Chama cha Afro-Shirazi kilichokuwa kinapinga jamii ya watu wachache kuhodhi uchumi wa Zanzibar na Pemba.
Kuna wengi walifanya mambo yanayofanana na Okello. Miongoni mwao ni Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye mapinduzi ya Cuba licha ya kwamba alikuwa ni mzaliwa wa Argentina.
Leo hii Che Guevara ni jina linalosifika na kuheshimika nchini Cuba kutokana na mchango wake. Haiyumkiniki jina la Okello nalo lingekuwa ni jina la kuheshimika kwenye na kukumbukwa kwenye Mapinduzi ya Zanzibar lakini ndivyo imekuwa sivyo.

salary

A Knight In Tanzania-Journey From Old Ifakara
 
Zaidi ya Cuba, ni wapi pengine alipofanikiwa?
 
Na upi ukweli kuhusiana na kugeukana baina ya Che Guevara na Fidel Castro baada ya kushika madaraka ya Cuba...?
Niliisoma sehem ila ilikuwa kifupi mno.
 
Je mafunzo ya kijeshi na upambanaji aliyapata wapi?
 
Huyu jamaa ni miongoni mwa watu ambao nikiwasoma nasikia furaha na uchungu sana....

Huyu jamaa aliuawa na CIA baada ya kumkamata huko Bolivia...

Ubinadamu wa huyu jamaa ni wa kiwango kizuri kabisa....

Alikufa akitimiza majukumu yake.Wakati yeye akishinda maporini kuwasaidia wengine waishi kwa amani wengine walikuwa wakiwaza kuiba na kutafuta wanawake wengi zaidi wawezavyo....
 
mkuu samahan hivi che alihusika mapinduzi ya zanzibar
Kuna tetesi na hisia zisizothibitishwa kwamba Che Guevara alishiriki ama kupanga au katika mapambano ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 kwa upande wa kikosi cha wanaharakati wa Kikomunisti wa Umma Party (UP) ambao wengi wao walipata mafunzo ya kijeshi nchini Misri na Cuba.

Uvumi wa aina hiyo ulikuwa hai siku ya Mapinduzi kwa duru za kibalozi visiwani, wageni na wapita njia walionukuliwa wakisema waliwaona Wacuba (wenye madevu); au kwamba walisikia wapambanaji hao wakiongea Kihispaniola.

Kama hilo halikuwa kweli, basi bila shaka watu waliokuwa wakiongelewa ni wale vijana wa Abdulrahman Babu wa Umma Party, wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka Cuba, waliorejea nchini Zanzibar wakiongea lugha ya Kihispaniola kwa ufasaha mkubwa.

Tukio lingine linalofanya watu wafikirie Che Guevara alikuwa na mkono wake katika Mapinduzi ya Zanzibar ni ziara yake mwaka mmoja baada ya Mapinduzi, Februari hadi Aprili 1965 wakati huo akijiandaa kuelekea Congo.

Uzito wa ziara yake Visiwani haukuwa wa kawaida kwani ingawa sherehe za kwanza za Mapinduzi Visiwani zilitakiwa kufanyika Januari 12, 1965, ziliahirishwa hadi Februari 12, 1965 pengine kumsubiri awasili kwa ziara ya siri visiwani Februari 11, 1965 ili ashiriki kwa siri siku inayofuata.

Rais Abeid Amani Karume alimpokea kwa bashasha kubwa na kumkabidhi kwa Ali Sultani (Mhitimu wa Mafunzo ya Kijeshi Cuba, 1962) akisema: “Sikiliza Ali! Nakukabidhi mgeni huyu, “Comrade” mwenzenu uwe naye wakati wa ziara yake hapa Zanzibar na umhudumie vizuri”.

Che alipewa kwa siri kubwa nyumba ya kulala na ulinzi madhubuti pale Beit-Ras hadi alipoondoka kwenda Dar es Salaam akiwa njiani kuelekea Congo kwa mapambano.

Jambo ambalo Karume hakuelewa ni kwamba, Che na Ali Sultani walikuwa wanajuana tangu mwaka 1961 kule Cuba wakati Chama cha kiharakati cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kilipofungua Ofisi Havana,Cuba; na tena mwaka mmoja baadaye, pale Ali na wanaharakati wenzake wa ZNP walipokwenda mafunzoni nchini humo mwaka 1962 kabla ya kujiengua ZNP pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Babu mwaka 1963 kuunda Umma Party, kilichoshiriki Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Usiku wa Februari 12, 1965, Che alikutana na Makomredi waliokuwa Cuba mwaka 1962 katika karamu maalumu iliyoandaliwa na kufanyika nyumbani kwa Ali Mahfoudh eneo la Migombani.

Waliokuwepo ni pamoja na Ali Mahfoudh mwenyewe, Mohamed Ali Foum, Ali Abdullah Bafaki, Salim Ali Ahmed Salim na wengine. Kanali Mahfoudh ndiye alikuwa Mkuu wa kwanza wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Zanzibar (Zanzibar People’s Liberation Army) – ZPLA kufuatia Mapinduzi.

Che alisikitika kuwakosa baadhi ya Makomredi, kama Amour Dugheish, Salim Saleh, Hashil Seif Hashil, Ali Mshangama na wengine ambao wakati huo walikuwa mafunzoni nchini Urusi na Indonesia.

Ziara ya Che Guevara Visiwani ndiyo iliyoibua tetesi zilizonaswa na “vyanzo” vya Ubalozi wa Marekani mjini Dar Es Salaam kwamba, mpiganaji huyo alikuwa pamoja na Babu nchini Tanzania; lakini Mwalimu Nyerere akakanusha na kujifanya hajui kitu.
 
safi sana mkuu
 
Che still kuna Baadhi ya jamii hko Latin america zinamchukulia km MESSIAH aliyetumwa na Mungu for the sake of humanity
Watu wanamwomba ht ktk iBaDa zao
Ni imani yao, ila hii inaonyeaha Jamaa yuko Hai ktk mAisha ya Watu ya kila siku na athari alioiacha inaishi BADO ktk akili, nafsi, Mioyo ya watu
 
Kuna watu wapo tayar kijitoa kwaajili ya wengine ila wanaishia kipondwa na magreat thinkers wa kwenye sosho media eg alfons lusako anavoogelea kejeli kwa kujitoa kwaajili ya wengi pale mliman
 
Back
Top Bottom