Usiweke imani yako kwa mtu au kitu

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,362
1,619
Habari wakuu. Natumai mu wazima wa afya na bado mnachukua tahadhari za COVID 19. Pengine kichwa cha habari kimekuvuta upite hapa. Karibu sana.

Kati ya vitu ambavyo vimenisaidia kukomboa fikra moja wapo ni hiki ninachokueleza leo. Umewahi kuwaamini watu ukawapa dhamana ya jambo fulani na hata upendo wako lakini hawakufanya kama ulivyotaka? Umewahi kuamini unachofanya ndicho pekee kitaendesha maisha yako na ikafika mahali ukakwama?

Umewahi kuamini mke au mume ndiye nguzo pekee na ikatokea vinginevyo ukapata taabu sana? Umewahi kuamini marafiki na wakakurudisha nyuma sana na hata kufikia hatua isiyo njema? Umewahi kuamini watu na wakakusaliti. Au kuamini kuwa ahadi fulani walizokupa watazitekeleza na ikakupotezea muda na kukirudisha nyuma.

Umewahi kuwaamini viongozi, wa dini au serikali ukawafwatilia ukagundua sivyo walivyo ukaondoa imani kwao na hata kwa Mungu? Mifano ipo mingi sana

Leo naongelea suluhisho lake

Kila kitu kina Msingi. Amini katika msingi sahihi. Weka msingi katika kila jambo na uufuate hautakaa uyumbe kamwe.
Unataka kufanya biashara fuata misingi sahihi.

Unataka kuingia kwenye uhusiano fuata misingi sahihi. Unataka kuwa na imani, ijue misingi ya imani yako amini katika misingi hiyo na sio watu.

Katika kazi unayofanya jua msingi wake amini katika hilo kwa lolote litakalotokea msingi bado utakuwa nao utaweza kujenga mengine juu yake.

Kwenye uhusiano wowote kuna vitu ambavyo ni vya msingi sana unapaswa kuvijua na kuviamini kabla hujafanya maamuzi lolote litakalotokea utakuwa umejiandaa.

Nakutakia siku njema
 
Back
Top Bottom