Usiwaamini sana marafiki wa ukubwani na ambao mmepotezana kipindi kirefu kisha kukutana tena

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Maana kuna jamaa ni mfanyakazi mwenzangu nimekuwa na urafiki naye wakikazi kwa muda wa miezi mitano ila sijawahi kukaa naye sehemu hata moja kula naye bata, ila juzi tukiwa kwenye kikao cha kazini tukaenda kupanga lodge moja kila mtu room yake sema zinaangaliana milango.

Sasa mimi nilimwamini sana, kumbe wakati natoka kwenda nje jamaa alizama room kwangu na kuingia kwenye bag langu ambapo kulikuwa na Tsh 300,000 nakuiba 80,000, na nilijua kesho yake baada ya kuzihesabu pesa na kukuta zipo 220,000 badala ya 300,000 nikajua ni jamaa tu, tena nina bahati hakuamua kuniibia pesa zote yaani aliingia kwenye bag na kuzichambua vizuri na kuzirudishia kama alivyozikuta.

Nina bahati pesa nyingine nilikuwa natembea nazo kwenye pochi mfukoni na nina bahati mwizi aliamua kunihurumia.

Kiukweli hilo suala limenifanya kupunguza mazoea ya karibu sana na watu tunaokutana tu bila kuwajua vizuri na kwa mazingira ninayoishi sitokubali kupeleka mwanamke au mshikaji kushinda ghetto kwangu la sivyo natakiwa kuwa makini sana.
 
Ulijuaje kuwa ni yeye aliyechukua

Ulijuaje kuwa ni yeye aliyechukua?
Alichagua kuchukua kiasi tu na sio pesa yote ili nisigundue na kunihurumia Kwa sababu tunafanya kazi inayofanana,na alikuwa anajua Nina kiasi icho kwenye bag kupitia story story zetu,angekuwa mtu mwingine angechukua pesa zote,na vyumba vyetu vilikuwa vinatazamana na nilitoka Kwa muda WA nusu chumbani kwangu Kwa muda WA nusu saa na nilisahau kufunga mlango nahisi alikuja kunicheck na hakunikuta ivyo akapata kishawishi cha kufungua bag langu maana baada ya kuchukua pesa alirudishia zingine kama alivyozikuta na aliogopa kuchukua zote maana ningegundua mapema na kama angekuwa mwizi aliyetoka mbali angechukua zote na kutokomea , maana ilo eneo tulikuwa watu watatu tu mimi,mhudumu WA lodge na uyo jamaa yangu na baada ya mhudumu kutupa room tu hakuwa na access ya kuingia tena
 
Kama haujamuona utakuwa unakosea Sana kumtuhumu.

I speak from Experience.
Ok, usikute kweli aisee ila eneo ilo tulikuwa watatu tu yeye,mimi na mhudumu WA iyo lodge,na naamini ni ngumu mhudumu kufanya wizi smart kama huo
 
Una uhakika gani ni yeye? Yeye katoa wapi ufunguo?

Nishawahi kuibiwa hela ile hotel iko nyuma ya Msamvu bus station ‘Morogoro, ni zamani mpk nimepasahau jina. BTW ilikuwa tu ndogo,, nina hakika ilichukuliwa na mfanya usafi.

Maana nilimpisha, nikashuka chini kwenda kwenye chai. Kuja kurudi hazipo kama nilivyokuwa nimeacha.
 
Alichagua kuchukua kiasi tu na sio pesa yote ili nisigundue na kunihurumia Kwa sababu tunafanya kazi inayofanana,na alikuwa anajua Nina kiasi icho kwenye bag kupitia story story zetu,angekuwa mtu mwingine angechukua pesa zote,na vyumba vyetu vilikuwa vinatazamana na nilitoka Kwa muda WA nusu chumbani kwangu Kwa muda WA nusu saa na nilisahau kufunga mlango nahisi alikuja kunicheck na hakunikuta ivyo akapata kishawishi cha kufungua bag langu maana baada ya kuchukua pesa alirudishia zingine kama alivyozikuta na aliogopa kuchukua zote maana ningegundua mapema na kama angekuwa mwizi aliyetoka mbali angechukua zote na kutokomea , maana ilo eneo tulikuwa watu watatu tu mimi,mhudumu WA lodge na uyo jamaa yangu na baada ya mhudumu kutupa room tu hakuwa na access ya kuingia tena
Sio wezi wote wanaiba pesa zote.
 
Umeibiwaaa na malayaaaa sio mwanaa we ndo snich mim mwanangu aliniibia simu tulikua tushare room ila nilimfuta nikamwambia mwanangu mim mwenyewe mwizi kama wew so rudisha simu yangu akarudisha kwa siri ila ushikaji uliendelea kama kawa.......tukapiga na k vant kubwa
 
Sio wezi wote wanaiba pesa zote.
Kumbe?😀😀ndo Leo najua ila Kwa akili za kawaida mwizi anayechukua pesa kidogo na kuacha nyingine uwa hayupo mbali na eneo la tukio ila mwizi wa kupita angebeba zote,Nina bahati sana
 
Umeibiwaaa na malayaaaa sio mwanaa we ndo snich mim mwanangu aliniibia simu tulikua tushare room ila nilimfuta nikamwambia mwanangu mim mwenyewe mwizi kama wew so rudisha simu yangu akarudisha kwa siri ila ushikaji uliendelea kama kawa.......tukapiga na k vant kubwa
Bro sikuwa na malaya Wala sikulala na malaya
 
inaweza ikawa ni muhudumu maana nao wanavitabia hivyo wakiona umetoka hujaacha funguo reseption wanapita kuangalia kama umefunga mlango wakikuta haujafungwa ndio hivyo imekula kwako
 
Umeibiwaaa na malayaaaa sio mwanaa we ndo snich mim mwanangu aliniibia simu tulikua tushare room ila nilimfuta nikamwambia mwanangu mim mwenyewe mwizi kama wew so rudisha simu yangu akarudisha kwa siri ila ushikaji uliendelea kama kawa.......tukapiga na k vant kubwa
Iyo ni balaa😀
 
Ok, usikute kweli aisee ila eneo ilo tulikuwa watatu tu yeye,mimi na mhudumu WA iyo lodge,na naamini ni ngumu mhudumu kufanya wizi smart kama huo

Wizi umetofautiana Sana kuwa makini usije ukawa guilty

Wizi wa watu wa Tanzania upo katika scarcity mindset na sio katika kujitafutia utajiri na maisha mazuri

Mimi niliibiwa simu mbili na mwizi akaacha simu moja na nilikuwa nimelala ghetto.

So hiyo kesi yako inawezekana huyo jamaa akawa hajakuibia trust me
 
Duh kweli inaweza kuwa mhudumu
 
We ndyo snitch sasa
Umejuaje ni yeye
Yaani sababu ulizotoa hazina mashiko kabisa
 
Wizi umetofautiana Sana kuwa makini usije ukawa guilty

Wizi wa watu wa Tanzania upo katika scarcity mindset na sio katika kujitafutia utajiri na maisha mazuri

Mimi niliibiwa simu mbili na mwizi akaacha simu moja na nilikuwa nimelala ghetto.

So hiyo kesi yako inawezekana huyo jamaa akawa hajakuibia trust me
Ndo maana kwenye kesi uwa Kuna kuwa na suspects na ningeamua kukiamusha wangehusika wote mhudumu na mshikaji
 
Mara ya mwisho kuhesabu hiyo pesa ni wapi.
Hadi naingia na kuweka ilo bag nilikuwa na icho kiasi cha pesa,ila nimeamua kupotezea tu maana pesa utafutwa sema imenisaidia tu kuwa makini zaidi na watu
 
Back
Top Bottom