Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,389
- 12,020
Bidhaa inapotengenezwa hasa ya afya huambatana na tafiti na uthibitisho wakutosha kabla ya kuruhusiwa kutumika katika shughuli maalumu iliyokusudiwa. Kubadilisha matumizi ya bidhaa ya afya sio jambo linaloshauriwa hata kidogo mara nyingi ni hatari na huweza kuambatana na madhara makubwa.
Kumekuwa na mtindo wa kujipaka mafuta ya kukamulia wanyama watu wamekuwa wakiyatumia kama mafuta ya kawaida ya kwenye ngozi . Mafuta haya yametengenezwa kwaajili ya ngozi ya ng'ombe ambayo kimsingi na kibiolojia haifanani na ngozi ya binadamu, na wala hairuhusiwi kutumika kwa matumizi hayo.
Madhara unayoweza kuyapata "Haijaidhinishwa mpaka tafiti zifanywe"
Yanaweza kuwa na kemikali au viungo ambavyo havijathibitishwa kuwa salama kwa ngozi ya binadamu
- Kwa binadamu yanaweza kusababisha muwasho, vipele, mzio (allergy), au kuziba vinyweleo
- Hayajapimwa wala kuidhinishwa kwa matumizi ya
Ya ngozi ya binadamu
- Hayana viambata na misombo inayopatikana katika mafuta ya kawaida ya kujipaka binadamu kama vitamin A , E , K na F