Usithubutu kununua LUKU kwa M-PESA

Usithubutu kununua LUKU kwa M-PESA

Voda bana majanga nilihamisha PESA toka NMB kuja m PESA kuja kuipata in SKU NNE jaman hawa hawafai
 
Ni kweli luku kwa mpesa ni shida. Nililazimika kwenda tanesco ndiyo wakanipa hizo number za token.
 
Mpesa kwa LUKU kiukweli inasumbua,ukinunua unasubiri zaidi ya masaa kupata namba.
Wanaboa kiukweli utafikiri huduma ni bure bwana!
 
Kaka wakikuita kama Le mutuz nenda peke yako!! Joke
 
Mimi nilipata umeme masaa nane baada ya kununua luku kwa mpesa toka saa tatu asubuhi mpaka kumi na moja na nusu, DSTV ndio usithubutu, nilikosa mechi ya Atletico Madrid na Barca, ilifunguka kesho yake jioni, sina hamu na hawa jamaa kabisa, ila kwa Tigo Pesa inaitika hapo hapo.
 
Kamanda nunua kwa tigo pesa Ni hapohapo unapata.....mpesa washazeeka, tumeacha siku ngingi, Ni majanga
 
Wakuu yaliyo nikuta leo ni majanga kweli nimerudi home LUKU imekata nikshauriwa ninunue kwa tiGo pesa nikawapuuza wadau nikaamua kununua m- pesa mpaka sasa ni saa zima linakatika sijapata umeme. Nasikilizia tu giza totoro.
Unachosema ni sahihi kabisaaaaaaa! Mimi nilinunua umeme tsh 15900 mwezi wa nne mpka leo sijaona mwanga wala nini mpaka mnilipoenda kwa wakala anae uza luku akaniuzia tena ndo nikapata mwanga.
 
Sio m pesa tu. usitumie VODACOM kabisa. ni majambazi wa mchana. Hebu jaribu kununua kifurushi cha wiki uone mchezo wa voda.
 
Sio m pesa tu. usitumie VODACOM kabisa. ni majambazi wa mchana. Hebu jaribu kununua kifurushi cha wiki uone mchezo wa voda.

Voda Ni Mtandao Hovyo Sana Mi Leo Nimenunua Kifurushi Eti Nusu Saa Nzima Hawajaniunganisha
 
Wakuu yaliyo nikuta leo ni majanga kweli nimerudi home LUKU imekata nikshauriwa ninunue kwa tiGo pesa nikawapuuza wadau nikaamua kununua m- pesa mpaka sasa ni saa zima linakatika sijapata umeme. Nasikilizia tu giza totoro.
halafu hata kama ulikatwa sevice charge kwa kununua LUKU kwa namna nyine, nao wanakata
 
Najuuta kuwafaham MPESA na Luku, nimenunua umeme tokea asubuh mpk saiv naandika saa mbili usiku bado haujaja. Imenibidi nimuombe jirani yangu aninunulie kwaTigo pesa yake fasta hata dakika haijapita nimepata. Voda nawahama rasmi kesho.
cc Vodacom Tanzania
 
Last edited by a moderator:
tiGO pesa kitendo cha kucomfirm tu .. tayari umeme nao hapohapo unatumwa . hauchelewo hata sekunde 1.
 
Sijawahi kupata hilo tatizo na mara zote na nunua kwa Mpesa
 
Back
Top Bottom