Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Siasa ni mchezo mbaya umejaa unafiki wa kila aina. Ninawasikiliza wanasiasa wanavyosema Mama umejenga, Mama umetenga, Mama unakusudi jema sana.
Yote hayo ni maneno mabaya kwa maana ya kumtwisha mzigo mzito rais na kama akikosa hekima basi anaenda kuvimba kichwa na kupoteza mwelekeo.
Nawashauri wasaidizi wa Mheshimiwa Rais kupenda kutumia maneno mbadala ili asikwazwe Rais. Huyo Rais anaongoza taasisi pana yenye watu wengi walio chini yake. Sio haki kumgeuza kuwa superman anayeweza kufanya kila kitu peke yake.
Mnapokuwa mnasimfia kupitiliza labda zipo nia za upigaji kwa kumpofua macho yake ya moyoni. Lakini kama mnaweza kumsifia kama kafanikisha kila kitu yeye kwa nguvu zake binafsi na muwe na utayari wa kumwambia ukweli pindi serikali yake inapoboronga.
Majukumu anayokuwa nayo katika utekelezaji wa suala fulani la kiserikali ni hayo hayo anayokuwa nayo mambo yanapokuwa mabaya.
Mjitahidi kuweka uwiano ulio sawa mnapozielekeza sifa nyingi kwa Rais. Ili asije akawa na 'kichwa' kikubwa akajikuta anaiharibu kazi badala ya kuiweka sawa kwa faida ya Taifa letu.