Serikali ya Rais Samia Haitasahaulika Wala Kufutika Katika Mioyo ya Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,218
9,645
Ndugu zangu Watanzania,

Serikali ya Rais Samia itakumbukwa kwa miaka mingi sana, itaishi katika mioyo ya Watanzania na kusimuliwa vizazi na vizazi. Haiji kupotea wala kufutika katika mioyo ya Watanzania, itaendelea kudumu na kutawala fikira za Watanzania. Itaendelea kuongoza katika mioyo ya Watanzania kutokana na alama za kudumu zilizoandikwa kwa wino wa upendo katika vifua vya Watanzania. Kila wakati itasimuliwa kwa mema mengi iliyoyafanya na kukumbukwa kwa miaka mingi sana ijayo kama tunavyoendelea kuishi na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika mioyo yetu bila kujali itikadi zetu za kisiasa au dini zetu.

Ni serikali hii ya Rais Samia kwa miaka mingi ijayo ambapo kila kijana atasimulia kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo ajira zilianza kutolewa maelfu kwa maelfu, mikopo vyuoni ilianza kumwagwa na kutolewa kwa wote wenye sifa bila ubaguzi. Ni wakati wa Samia ambapo fedha ya kujikimu ilipanda mpaka kufikia elfu kumi kwa siku na kupelekea wanafunzi kusoma kwa utulivu na kuzingatia vyema masomo. Ni serikali hii itakumbukwa na mamilioni ya vijana kuwa ni wakati wake aliwapa vijana tabasamu, furaha, na matumaini ya kupata ajira na kujiajiri kwa wepesi kutokana na mazingira mazuri ya kibiashara, hasa baada ya kuweka utaratibu wa kutokulipa mapato katika mwaka wa kwanza wa biashara ili kutoa nafasi ya kukua kimtaji.

Ni serikali hii itakayosimuliwa na wakulima kuwa ni wakati wa Rais Samia walipofutwa machozi, walipopewa heshima wao na sekta ya kilimo. Ni wakati wa Rais Samia ambapo kilimo kilianza kuwa kimbilio la watu wote wakiwepo wasomi. Itasimuliwa na wakulima kuwa ni wakati na utawala wa Rais Samia ulipokigeukia kilimo na kuweka mikono yake kwa kuwekeza mabilioni ya pesa ili kuwainua migongo yao wakulima iliyokuwa imeinama na kupinda kutokana na dhoruba za jembe pasipo kupata wala kufaidika na jasho lao, mpaka Mama Samia alipokuja kama mkombozi wao na kutoa nuru katikati ya giza totoro katika kilimo.

Itasimuliwa kwa vizazi vijavyo na wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo biashara nyingi zilifunguliwa, wafanyabiashara wakifanya biashara kwa amani na utulivu, maafisa wa TRA walikuwa marafiki zao na watu wa kutoa ushauri wa kitalaam hususani unaogusa masuala ya kikodi. Itasimuliwa ni wakati huu ambapo wafanyabiashara walianza kutunza pesa zao benki badala ya kwenda kufungia majumbani mwao au chini ya magodoro kwa hofu, kwa kuwa ni wakati huu walikuwa na imani na Rais Samia na serikali yake na hawakuwa na wasiwasi wa kuchotewa pesa na mtu yeyote pasipo utaratibu wa kisheria na kibenki.

Wazazi watasimulia kwa watoto na wajukuu zao kuwa ni wakati wa serikali ya Rais Samia ambapo elimu ikawa bure hadi kidato cha sita na kuwafanya watoto wao kusoma hadi vyuo vikuu bila kujali hali zao za kiuchumi kuwa duni, kwa kuwa mzigo wa ada ulikuwa umebebwa na serikali ya Rais Samia. Itasimuliwa na wazazi kuwa ni wakati wa Rais Samia watoto na vijana wengi walisoma kwa bidii kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea na kujifunzia pamoja na soko la ajira kuwa lenye kuleta matumaini kwa vijana wao.

Ni serikali hii ya Rais Samia itakumbukwa na kusimuliwa na watumishi wa umma kwote nchini kuwa ni wakati huu ambapo walianza kupata morali ya kazi na kujituma kazini. Ni wakati huu ambapo walianza kujiona kuthaminiwa mchango wao katika maendeleo na ukuaji wa uchumi. Ni wakati huu ambapo ajira serikalini ilikuwa ni kazi ya heshima katika kulitumikia taifa badala ya kuonekana kama utumwa na gereza, kwani ni wakati huu ambapo viongozi waliwaheshimu na kuwatia moyo katika utendaji kazi wao. Ni wakati huu ambapo walianza kupandishwa madaraja, nyongeza ya mishahara, kupewa posho ya kazi kulingana na majukumu ya mhusika, n.k.

Serikali ya Rais Samia itasimuliwa na Watanzania kuwa ni wakati wa Rais Samia ambapo kwa mara ya kwanza rais wa nchi, Mwenyekiti wa Chama Tawala katika historia ya taifa letu, alihudhuria siku ya Wanawake Duniani kwa kujumuika na akina mama kutoka chama kikuu cha upinzani CHADEMA. Itasimuliwa ni wakati huu ambapo hakukuwa na uhasama wa kisiasa, Watanzania walianza kuishi kwa upendo, mshikamano na umoja wa hali ya juu sana kwa kushirikiana katika shughuli zote za kijamii.

Serikali hii ya Rais Samia itasimuliwa kuwa ilisimama imara katika kipindi ambacho majirani zetu walifikia hatua ya kushindwa kulipa mishahara watumishi wake wa umma. Ilihali hapa nchini, serikali yetu ilikuwa inaendelea kuwahisha zaidi mishahara kwa watumishi wa umma pamoja na kutoa maelfu ya ajira kwa vijana.

Serikali ya Rais Samia itakumbukwa na mamilioni ya Watanzania kwa kutuvusha kipindi kigumu cha ugonjwa hatari wa COVID-19 pamoja na vita ya Ukraine, uliyopelekea mfumuko wa bei duniani kote, hasa kwa bidhaa muhimu na kupelekea mdororo wa uchumi. Lakini ni kwa ushupavu wa Rais Samia na serikali yake, alisimama imara na kuchukua hatua za makusudi kwa kutoa mabilioni ya ruzuku katika mbolea kiasi cha bilioni mia moja hamsini, pamoja na kutoa ruzuku ya bilioni mia moja kila mwezi katika nishati ya mafuta. Jambo ambalo nchi jirani zilishindwa kufanya hivyo na kupelekea kulia na kuteseka kwa wananchi wao. Huku Tanzania tukiwa Tumesaidiwa na serikali yetu kupunguza makali ya mfumuko wa bei.

Ni serikali hii ya Rais Samia itakumbukwa kwa kutoa uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na uhuru wa mahakamani. Ni wakati huu itakumbukwa na Watanzania kuwa kila mmoja alijiona fahari kuzaliwa Tanzania na kila mmoja alijiona anayo nafasi ya kutimiza ndoto zake, lakini pia kila mmoja alijivunia mafanikio yaliyopatikana na kujiona ni sehemu ya mafanikio hayo.

Kila mmoja atasimulia kuwa ni wakati wa serikali ya Rais Samia ambapo ilikuwa mali ya Watanzania, serikali ikawa kwa ajili ya kuwatumikia watu, kuwasikiliza watu, kufanya maamuzi yenye maslahi kwa wengi, kupitisha sheria zenye afya kwa watu na tija kwa taifa letu. Ni wakati ambapo Watanzania walipewa nafasi ya kusikika sauti zao na kupewa majibu ya kina.

Kwa hakika, serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia haiji kufutika wala kusahaulika katika mioyo ya Watanzania kwa miaka mingi sana ijayo. Itaendelea kusimama kama rejea nzuri na kwa mambo yote mema katika taifa letu. Majina ya viongozi wake yataandikwa katika kuta za mioyo ya Watanzania kwa wino wa dhahabu.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Jingajinga fulani
JamiiForums-1659793415.jpg
 
Ndugu zangu watanzania,

Serikali ya Rais Samia Itakumbukwa kwa miaka mingi Sana,itaishi katika mioyo ya watanzania na kusimuliwa vizazi na vizazi, haiji kupotea Wala Kufutika Katika Mioyo ya watanzania, Itaendelea kudumu na kutawala Fikira za watanzania, do na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Kwa kweli kuna watu wanajua kusifia! Ila wewe wewe mwenzetu umezidi.

Maana hata mhusika akisoma hii habari yako, atagundua mapema sana ya kuwa wewe ni zaidi ya chawa.
 
Kwa kweli kuna watu wanajua kusifia! Ila wewe wewe mwenzetu umezidi.

Maana hata mhusika akisoma hii habari yako, atagundua mapema sana ya kuwa wewe ni zaidi ya chawa.

Kwa kweli kuna watu wanajua kusifia! Ila wewe wewe mwenzetu umezidi.

Maana hata mhusika akisoma hii habari yako, atagundua mapema sana ya kuwa wewe ni zaidi ya chawa.
Kwa kazi kubwa na ya kutukuka aliyoifanya mh Rais wetu na serikali yake ndani ya muda mfupi kiukweli mama Anastahili pongezi ,Anastahili kuungwa mkono,kupewa faraja, ushirikiano na kutiwa moyo,Anastahili kupewa heshima ya kipekee kabisa.

Rais Samia kaleta Tabasamu,furaha na matumaini katika mioyo ya watanzania,kaleta nuru na mwanga kila eneo,kaleta morali kwa watu wote na kawafanya watanzania waone wanayo fursa na nafasi ya kutimiza Ndoto zao katika ardhi ya Tanzania,Ni mama yetu Rais Samia na serikali yake ambapo Sasa Tanzania Ni kimbilio na chaguo namba moja la wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kutoka Mataifa mbalimbali.

Rais Samia Ni Nyota ya matumaini katikati ya Giza.
 
Wewe unafikiri mimi ni Mfugo wa Samia kama wewe?
Mimi siyo mfugo Bali Ni mtanzania mzalendo ninayeunga mkono serikali iliyopo madarakani chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mama Samia , kutokana na kazi kubwa iliyofanywa ndani ya muda mfupi iliyoleta matumaini , Tabasamu , matumaini na nuru katika maisha ya watanzania.
 
Mimi siyo mfugo Bali Ni mtanzania mzalendo ninayeunga mkono serikali iliyopo madarakani chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais wetu mama Samia , kutokana na kazi kubwa iliyofanywa ndani ya muda mfupi iliyoleta matumaini , Tabasamu , matumaini na nuru katika maisha ya watanzania.
Unaunga mkono serikali iliyojaa wezi? rejea ripoti ya CAG Kichere.
 
Back
Top Bottom