Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Mkuu bado sijaonakuweza kuitetea hoja yako. Unachofanya ni kulazimisha tu kuwa uwepo wako ndiyo unasababisha uwepo wa vitu vingine viwepo na kutokuwepo kitu ambacho hujaweza kueleza ni kwanini hasa iwe hivyo?

Kila kitu kina uwepo wake sasa haiwezekani kukosekana uwepo wako mahali kuondoe uwepo wa vitu vingine,halafu wakati mie nazungumzia yale niliyo na uzowefunayo kwa sababu ya uwepo wangu hapa duniani wewe unazungumzia mambo ya kutokuwepo ambayo sijui umepataje uzowefu wa hayo mambo?
 
Lazima mimi niwepo kwanza, ili space iwepo. Je, una kumbukumbu yoyote ya kuwepo kwa space kabla ya kuwepo kwako? Kwa kuwa bado upo, unaweza kututhibitishia namna utakavyoendelea kufahamu kuwa kuna space mara baada ya wewe kutokuwepo?
Ni kweli mkuu bila kuwepo hatuwezi kuthibitisha uwepo.Hivi vitu vinahitaji akili kubwa kuelewa
 

Mkuu, unajuaje kuwa kila kitu kina uwepo wake. Hili umelijua wakati gani? Kabla ya kuwepo au baada ya kuwepo? Vipi siku usipokiwepo,hili utaendelea kulijua? Unafikiri hii itakuwa na maana gani kwako ikiwa hutakaa kujua tena kama kila kitu kina uwepo?
 
Falsafa ni somo lisilo na hitimisho kila mtu huwa anakuja na lwake.Thales,Permanindes,Pythagoras etc walishindwa kutoa majib sawa about existence of human being.I'm a typic sophist philosophical ideas follower.

Ni sahihi mkuu, ni suala la kutafuta kiwango cha usahihi wa fikra. Ikiwa mtu atawaza na kuona ukomo wa kile mtu alifikiri ni sahihi, basi fikra husika inaachwa ama mwenye fikra hiyo anapewa jukumu la kuendelea kuboresha zaidi fikra yake.
 
Ili kitu kiendelee kuwepo au hali ya mabadiliko yake iendelee kuwepo, ni lazima mtu au kitu mahususi kilichokuwa na ufahamu wa uwepo wa mtu, kitu au hali hiyo kiendelee kuwepo.
 
Huyu mkuu forumyangu naona ameeleza vyema kwa nini lazima kuwe na uwepo kwanza. Ameandika, ninamnukuu:

"Ni kweli mkuu bila kuwepo hatuwezi kuthibitisha uwepo......"

Ili kitu kiwepo, unahitajika uthibitisho na hakuna namna unaweza kuthibitisha uwepo wa kitu bila kuwepo. Nikikuomba uthibitishe uwepo wa Dunia kabla ya wewe kuwepo, nadhani hutaweza. Hata hivyo, mwenyewe unahoji ikiwa ninawezaje kuzungumzia kutokuwepo, kwamba ni hali isiyowezekana ilihali wewe unaona ni halali tu kuzungumzia uwepo ungali upo. Hii inathibitisha kuwa unaweza tu kuzungumzia uwepo ikiwa wewe upo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo na kamwe huwezi kuzungumzia chochote.
 
Unaona sasa hapo? Tofauti ya mie na wewe ni kwamba mimi nazungumza vitu ambavyo naviexperience kutokana na uwepo wangu hapa duniani na kumbuka kuwa unaposema mtu kuwepo au kutowepo tunakusudia uwepo wa hapa duniani,sasa wewe unazungumzia vitu vya kufikirika tu.

Kwa kuwa tunazungumzia kuwepo hapa duniani na mie kuwepo kwangu duniani najua kabisa mtu ambaye bado hajazaliwa(hayupo) hana athari yeyote kwa huku duniani,na mtu akifa huiacha dunia uwepo wake unakuwa umeondoka hapa duniani.

Sasa ni ajabu kuacha mambo ambayo unayashuhudia na kutaka kutumia mambo ya kufikirika,halafu pia uthibitisho haufanyi jambo liwepo bali uthibitisho unatoa uhakika wa kuwepo hilo jambo ni suala la kujiridhisha.

Kwahiyo mie kabla ya kuja duniani dunia ilikuwepo(nimetumia uzowefu wangu wa uwepo wa hapa duniani) hata kama nilikuwa sijui na nasingeweza kuthibitisha hilo kuwa kuna dunia.
 
Mkuu, unajuaje kuwa kila kitu kina uwepo wake. Hili umelijua wakati gani? Kabla ya kuwepo au baada ya kuwepo? Vipi siku usipokiwepo,hili utaendelea kulijua? Unafikiri hii itakuwa na maana gani kwako ikiwa hutakaa kujua tena kama kila kitu kina uwepo?
Hilo ni suala la kutokujua na hivyo haina maana kuwa hicho usichokijua hakipo kisa wewe hukijui,mie nazungumza kwa kutumia uzowefu ila wewe mkuu unazungumzia ya kufikirika yenye kupingana na uhalisia uliyopo na unataka hayo ya kufikirika yawe na athari kwenye mambo yenye uhalisia.
 

Hatuelewani! Ninasema kuwa, KUTOKUJUA KWAKO KWAMBA KITU KIPO, HAKUKIFANYI KUTOKUWEPO! UWEPO WAKO WEWE HAUFANYI KITU KISIWEPO KWA SABABU TU HUJUI KUWA KIPO!! AND THE FACT IS, WEWE UPO. USINGEKUWEPO, THAT COULD BE ANOTHER CASE. UNLESS KAMA WEWE MADAI YAKO KWA SASA NI KUWA HAUPO, WHICH IS WRONG KWA SABABU FACT INAONYESHA KWAMBA UPO!
 
Mungu (omnipotent, omniscuent, all benevolent) hayupo. Period.

Lakini ukisema usipokuwepo chochote hakipo ni logical fallacy.

Kwa sababu, usipokuwepo, kutokuwepo wewe kupo.

Ukisema "usipokuwepo hakuna kilichopo" unasahau kwamba kutokuwepo wewe kunakuwepo. Kutokuwepo wewe kukiwepo, hutakiwi kusema "hakuna kilichopo".
 
kwani aliyesema uhai unaisha nani,unaamini mungu yupo kwa kuwa upo usingekuwepo saa ngapi ungesema yupo.
 
Mshana Jr, karibia huku utoe maelezo
 
Oltunganyi, unaweza Ukanieleza chumba ni nini? Je, chumba ni kuta na paa? Au vitu vilivyomo ndani ya chumba?
Kiukweli jibu ni kwamba chumba ni empty space or nothing. Nothing can exist without nothing.
 
Tatizo ni kuwa, ukishaonesha kuwa hutoi nafasi kwa Mungu wa vitabuni, basi nawe unawekwa kwenye kundi la akili ya kawaida. Akili nzuri ni ile inayoamini kuwa kuna Mungu, haswa yule wa kwenye vitabu.
Wewe Mungu wako yupo wapi???
 
Siri ya uumbaji it's beyond human thinking. Majini, mapepo, mizimu, malaika na viumbe vingine visivyoonekana (visivyo na mwili bali nafsi) vinatuzidi kidogo kuhusu nini hasa siri ya uumbaji; vyote vinajua Mungu yupo na vinamuheshimu na kumwogopa; ila vingine vinafanya ujeuri tu sababu kiasi vinajua siri ya uumbaji.
 
Lazima mimi niwepo kwanza, ili space iwepo. Je, una kumbukumbu yoyote ya kuwepo kwa space kabla ya kuwepo kwako? Kwa kuwa bado upo, unaweza kututhibitishia namna utakavyoendelea kufahamu kuwa kuna space mara baada ya wewe kutokuwepo?
All things start with an idea.
 
Vitu vipo hata bila ya wewe kuvithibitisha.
Hata akili yako ipo japo huwezi kuithibitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…