Usipokuwepo, Hakuna Kilichopo!

Oltung'anyi

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
284
196
Ndio, usipokuwepo, hakuna kilichopo. Hata Mungu hayupo ikiwa wewe haupo. Ndio maana wapo wanaohoji kwamba kati yako na Mungu, nani wakwanza kuwepo.

Hoja hii inaweza kuwa na mashiko sana. Lazima uwepo ili Mungu awepo. Kwa hiyo, lazima wewe uwepo ili Mungu na kila kitu viwepo.

Ili uwepo uwepo,lazima wewe uwepo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo.
 
Kuna uwepo mwingi sana(space ni kubwa sana) na space ndo uwepo..
kwa kusema "ili uwepo uwepo lzm wewe uwepo" basi tambua huo uwepo uliopo ni mkubwa mno na mwengine upo ambapo wewe haupo na umeakaa hivyo kwa muda mrefu,sasa kama uwepo unakutegemea kwanini uwepo sehemu usipo..? uwepo haututegemei sisi bali sisi tunategemea uwepo na ndo maana tupo kwenye uwepo.
 
Ndio, usipokuwepo, hakuna kilichopo. Hata Mungu hayupo ikiwa wewe haupo. Ndio maana wapo wanaohoji kwamba kati yako na Mungu, nani wakwanza kuwepo.

Hoja hii inaweza kuwa na mashiko sana. Lazima uwepo ili Mungu awepo. Kwa hiyo, lazima wewe uwepo ili Mungu na kila kitu viwepo.

Ili uwepo uwepo,lazima wewe uwepo. Usipokuwepo, hakuna kilichopo.
Pole mkuu
 
Unamaanisha nisipokuwepo Mungu hayupo?
Au sijakuelewa ulivyomaanisha!!
Ndio maana yake mkuu. Usipokuwepo, hakuna chochote kilichopo, hata Mungu hawezi kuwepo bila wewe kuwepo. Mungu yupo kwa kuwa wewe upo. Jaribu kuonesha uwepo wa Mungu pasipo wewe kuwepo kama unaweza.
 
kuna uwepo mwingi sana(space ni kubwa sana) na space ndo uwepo..
kwa kusema "ili uwepo uwepo lzm wewe uwepo" basi tambua huo uwepo uliopo ni mkubwa mno na mwengine upo ambapo wewe haupo na umeakaa hivyo kwa muda mrefu,sasa kama uwepo unakutegemea kwanini uwepo sehemu usipo..? uwepo haututegemei sisi bali sisi tunategemea uwepo na ndo maana tupo kwenye uwepo.
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila bila shaka unajua unavyovijua na usivyovijua kwa kuwa upo. Unajua uwepo wa space na kuwa tunautegemea uwepo kwa kuwa tupo. Hakika bila wewe kuwepo, mimi sipo, wala uwepo haupo.
 
Siku tukifa ndo tutajua ukweli..nakisubiri kifo kwa hamu ili kijibu maswali haya yoote.
Nafikiri hili ni wazo zuri. Pia, unaweza kuwaza ikiwa kabla ya wewe kuwepo ulifahamu kuhusu uwepo. Sidhani kama una kumbukumbu yoyote ya kabla ya kuwepo kwako.
 
Ukitaka kuamini alichokisema jamaa hata jf isingekuwepo comments zenu zisingekuwepo hapo juu lazima jf iwepo na nyie ndo mtupie comments. Sema namimi nime mwelewa kwa mbinde
 
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila bila shaka unajua unavyovijua na usivyovijua kwa kuwa upo. Unajua uwepo wa space na kuwa tunautegemea uwepo kwa kuwa tupo. Hakika bila wewe kuwepo, mimi sipo, wala uwepo haupo.
hio ni kwako, lkn kutokuwepo sisi haimaanishi uwepo haupo.. kama uwepo umekuwepo kabla yako/yetu sote basi uwepo unaweza kuwepo hata kama hatupo.
 
Ukitaka kuamini alichokisema jamaa hata jf isingekuwepo comments zenu zisingekuwepo hapo juu lazima jf iwepo na nyie ndo mtupie comments. Sema namimi nime mwelewa kwa mbinde
wala hujamuelewa soma tena kichwa cha habari
 
hio ni kwako, lkn kutokuwepo sisi haimaanishi uwepo haupo.. kama uwepo umekuwepo kabla yako/yetu sote basi uwepo unaweza kuwepo hata kama hatupo.

Mkuu, siyo kwamba unatumia advantage ya wewe kuwepo ndio maana unaweza kueleza kuwa uwepo ulikuwepo na utaendelea kuwepo?. Kabla ya wewe kuwepo ulifahamu kuwa uwepo ulikuwepo na kwamba utaendelea kuwepo?. Nafikiri unaweza kuyasema haya kwa kuwa upo. Je, kisichokuwepo sasa kinaweza kuelezea uwepo wa sasa na uwepo ujao? Hatuoni kuwa, kwa kisichokuwepo, hakuna kilichopo?
 
Kila mmoja wetu ndio chanzo cha uwepo wake mwenyewe (bila kuwepo, huwezi kujua kama upo) na uwepo wa kila kitu. Hivyo, ni muhimu sana kutambua nguvu kuu tuliyo nayo, tujithamini na tuitumie kujenga tafsiri yenye tija tungalipo hapa duniani. Tukiona thamani yetu, ni lazima tuone thamani ya wengine maana nao wana nguvu ya namna hii iliyo na thamani sawa.
 
kuna uwepo mwingi sana(space ni kubwa sana) na space ndo uwepo..
kwa kusema "ili uwepo uwepo lzm wewe uwepo" basi tambua huo uwepo uliopo ni mkubwa mno na mwengine upo ambapo wewe haupo na umeakaa hivyo kwa muda mrefu,sasa kama uwepo unakutegemea kwanini uwepo sehemu usipo..? uwepo haututegemei sisi bali sisi tunategemea uwepo na ndo maana tupo kwenye uwepo.
Umemjibu vizuri maana bado hajui kitu na anatumia akili tu ya kawaida. Kwa Mungu hategemei uwepo wa chochote kile ili Yeye awe Mungu! Mwanzo 6:6-7. Watu wengine wamekuwa wepesi sana wa kuongea mambo wasiyo yajua, hivyo wanapotoka zaidi na kupotosha wengine wasiojua kitu!
 
ha ha ha! mkuu hapa umeingia pahala pengine! ya mungu mnayajua nyie,ndo maana hata sijamhusisha sorry kwa hilo
 
Unafikiri kuchanganya changanya lugha ili usieleweke kirahisi ndiyo utaonekana una akili.

Kwani ukifa unafikiri uhai unaisha na wewe?
 
Back
Top Bottom