Tz mbongo
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 12,228
- 6,398
Mkuu bado sijaonakuweza kuitetea hoja yako. Unachofanya ni kulazimisha tu kuwa uwepo wako ndiyo unasababisha uwepo wa vitu vingine viwepo na kutokuwepo kitu ambacho hujaweza kueleza ni kwanini hasa iwe hivyo?Ndugu, asante kwa tafakari yako. Ninafurahi kuwa unatumia muda wako kutafakari nami. Hili ni jambo zuri sana. Ninakupongeza. Nina imani nawe upo njiani kwa tafakari mpya zaidi.
Mkuu, nina swali moja fupi. Kama usingekuwepo duniani, kitu gani kingekuwepo? Endelea kulitafakari. Kama ukiwa na jibu kuwa, kwako, hakuna ambacho kingekuwepo. Swali jingine lingekuja, kwa nini sasa hivi vipo? Endelea pia kutafakari swali hili. Sidhani kama kuna jibu zaidi ya ni kwa sababu kuwa upo. Itakuwaje siku usipokuwepo milele? Hukuwepo, hivyo, hakuna kilichokuwepo, na baadae hutakuwepo, ina maana hakutakuwepo na chochote.
Ninakusoma mkuu, lakini bado sijashawishika kuwa, nisipokuwepo, bado kutakuwa na uwepo.
A kind of a theory. Ili kitu kiendelee kuwepo au hali ya mabadiliko yake iendelee kuwepo, ni lazima mtu au kitu mahususi kilichokuwa na ufahamu wa uwepo huo kiendelee kuwepo.
Kila kitu kina uwepo wake sasa haiwezekani kukosekana uwepo wako mahali kuondoe uwepo wa vitu vingine,halafu wakati mie nazungumzia yale niliyo na uzowefunayo kwa sababu ya uwepo wangu hapa duniani wewe unazungumzia mambo ya kutokuwepo ambayo sijui umepataje uzowefu wa hayo mambo?