Oltung'anyi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 284
- 196
- Thread starter
- #101
Unaona sasa hapo? Tofauti ya mie na wewe ni kwamba mimi nazungumza vitu ambavyo naviexperience kutokana na uwepo wangu hapa duniani na kumbuka kuwa unaposema mtu kuwepo au kutowepo tunakusudia uwepo wa hapa duniani,sasa wewe unazungumzia vitu vya kufikirika tu.
Kwa kuwa tunazungumzia kuwepo hapa duniani na mie kuwepo kwangu duniani najua kabisa mtu ambaye bado hajazaliwa(hayupo) hana athari yeyote kwa huku duniani,na mtu akifa huiacha dunia uwepo wake unakuwa umeondoka hapa duniani.
Sasa ni ajabu kuacha mambo ambayo unayashuhudia na kutaka kutumia mambo ya kufikirika,halafu pia uthibitisho haufanyi jambo liwepo bali uthibitisho unatoa uhakika wa kuwepo hilo jambo ni suala la kujiridhisha.
Kwahiyo mie kabla ya kuja duniani dunia ilikuwepo(nimetumia uzowefu wangu wa uwepo wa hapa duniani) hata kama nilikuwa sijui na nasingeweza kuthibitisha hilo kuwa kuna dunia.
Mkuu, ninafurahi kuwa bado tupo pamoja. Maelezo yako yanasisitiza umuhimu wa wewe kuwepo. Hiki ndicho kiini cha mada, kwamba uwepo wako ndio unaosababisha kila kitu kiwepo. Unashuhudia mambo (ya duniani) kwa kuwa upo. Hakuna namna unaweza kushuhudia mambo (ya duniani) usipokuwepo. Je, tuisemee vipi hali ya wewe kushindwa kushuhudia mambo ya dunia milele katika hali yako ya kutokuwepo milele?