Vyovyote vile utakavyo elezea huwezi kuepuka habari ya Mungu kwenye mambo kama haya yanayohusu asili isiyo onekana kwa damu na nyama, sababu Yeye Ndiye mwanzo wa mambo yote haya, hata dhamiri yako ni shahidi wa hili labda tu uwe na uelewa mdogo juu ya mambo haya.
Sasa ukiulizwa wewe umeyatoa wapi haya unayoyasema? Utasema umesoma kwenye vitabu vya waandishi hasa wale maarufu wa nyakati hizo ama historia, lakini ujue tu wazi hata hao wanafalsafa wenu wanasoma vitabu vinavyo mwelezea Mungu huyu huyu mnayesema Mungu wa kwenye vitabu na kisha wanayaboresha mawazo yao na kuandika hivyo mnavyovisoma nyie mnaojidhania kwamba mnapata uelewa nje ya vitabu hivi vinavyo mwelezea Mungu wa kwenye vitabu.