Usipokuwa muongo nyakati hizi lazima uumizwe

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,295
Natumaini mko shwari

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.. kwa pamoja mjibu CHAMA KIENDELEE.

Leo sitaki kuongelea katiba wala mambo ya siasa. Hapa leo ni mambo ya mapenzi tu. Nataka nitoe maoni yangu ambayo moja kwa moja ndo yatakuwa msimamo wa JF bila kujali itikadi. Nitaongelea uhalisia wa maisha na sio vinginevyo.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ninakazia kwa kusema huo ndo ukweli mtupu. Tupo kwenye nyakati ambazo jkiongea ukweli kila kitu utaishia kuingia kwenye matatizo makubwa mno. Sio kwenye siasa tu bali hata kwenye mahusiano ya kimapenzi huwa wakweli wanaishia kuadhibiwa.

Ukitaka uoe mtoto mkali lazima utumie kila aina ya hila kuficha madhaifu yako. Kwa mwanaume uongo ni nyenzo muhimu sana kuimarisha penzi. Ukiwa mkweli utaonekana unaboa na kuishia kupigwa chini kwa hoja kwamba "wewe sio type yake".

Mwanaume hakikisha hutoi nafasi ya mtoto mzuri kukuelewa kwa asilimia kubwa. Yaani mjaze matumaini tu.. matumaini 80% na hela 20%. Wanawake nao kwa sasa wako kasi sana kuwa waongo kama wanaume. Ni nadra kukuta dada wa mjini ana mtu mmoja. Wale wenye maadili mazuri huwa na wawili.

Kwenye ahadi za mwanaCCM kuna ambayo inasema "NITAKUWA MKWELI DAIMA".. ila kwenye mapenzi tunasema "NITAKUWA MKWELI INAPOBIDI"...

Nimalizie kwa kusema kwamba hakuna asiyejua mwisho wa uongo na mshahara wa dhambi ni mauti. Hivyo ukiwa mwongo usinihusishe kwasababu ni upumbavu wako mwenyewe na shetani wako.
 
Natumaini mko shwari

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.. kwa pamoja mjibu CHAMA KIENDELEE. Leo sitaki kuongelea katiba wala mambo ya siasa. Hapa leo ni mambo ya mapenzi tu. Nataka nitoe maoni yangu ambayo moja kwa moja ndo yatakuwa msimamo wa JF bila kujali itikadi. Nitaongelea uhalisia wa
Ninyi wana CCM huwa mnabebana tu hovyohovyo kwenye mbio za mwenge.Huwa mnapendana kweli au ni vilevi ndiyo huwaongoza?Nazingatia ulivyojinasibu kwamba weye ni kobe mwenye gamba la CCM.😝😝😝😝
 
Hata kwenye kutafuta papuchi lazima tuseme uongo la sivyo windo linaingia shuruba
IMG_20210627_080950.jpg
 
Natumaini mko shwari

Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.. kwa pamoja mjibu CHAMA KIENDELEE. Leo sitaki kuongelea katiba wala mambo ya siasa. Hapa leo ni mambo ya mapenzi tu. Nataka nitoe maoni yangu ambayo moja kwa moja ndo yatakuwa msimamo wa JF bila kujali itikadi. Nitaongelea uhalisia wa maisha na sio vinginevyo.
"...wenye maadili mazuri huwa na wawili"
Hii inamaanisha hata mimi nachapiwa?
 
Ninyi wana CCM huwa mnabebana tu hovyohovyo kwenye mbio za mwenge.Huwa mnapendana kweli au ni vilevi ndiyo huwaongoza?Nazingatia ulivyojinasibu kwamba weye ni kobe mwenye gamba la CCM.😝😝😝😝
Hahahahaha kwenye mbio za Mwenge kuna unafuu. Ukisikia kuna kongamano la vijana limeandaliwa na CCM mahala halafu kuwe na kulala ndo utafaidi.
 
Chama kiendelee


Mkuu usipokua muongo lazima utakua muhanga wa mambo mengi hasa kwenye mapenzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom