Usipojua kutafuta, utatafuta sababu ya kutokutafuta

Usipojua kutafuta, utatafuta sababu ya kutokutafuta

Bwana Bongo

Senior Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
167
Reaction score
239
#Porojozabongo

"Usipojua kutafuta, utatafuta sababu ya kutokutafuta."

"Unaelewa hiyo methali?" anauliza bongo, akiinamisha kichwa katika draft

"Bado naitafakari," akajibu mgogo, akimtazama bongo

"Hii ni porojo za bongo kaka," Bongo akaendelea, "Ina maana, ukikaa tu bila juhudi, mwisho utajikuta ukihangaika kujua kwanini huna."

"Aaah... kumbe ndo maana jana niliamka njaa, nikaanza kujiuliza maisha haya yananipeleka wapi."

"Usiulize kaka, jibu lipo kwenye bidii."

"Kwahiyo?"

"Kama hujui kutafuta, utaishia kutafuta sababu ya kutokutafuta."

"Yaani utajua kupitia uchungu."
 
Umenena ukweli mkuu.

"ukishindwa kujiandaa, unajiandaa kushindwa"

"ukishindwa kujituma kwenye mambo yako, utatumwa na wanaojituma kwenye mambo yao"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom