Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Ni kweli ni mzazi mwenzangu,na nampenda japo anajenga mazingira ya mimi kuipoteza familia yangu,kwa maana nyingine nyingine nisiende kuqatembelea familia yangu!!!(hapo ndo kitendawili,nawezaje kutelekeza familia yangu!!?)
Yaani na wewe unataka kabisa kuingia kwenye mtego wa hivyo wa kuiacha familia yako kizembe namna hiyo acha masihara basi kuwa greatman kweli Fanya maamuzi kwa ajili ya future ya yule unaetambua maisha yake, unatambulika kwao, wanamtambua kwenu

Kofia uliyo vaa ya u-greatman inaanza kupwaya kama utaendelea na maamuzi dhaifu kwenye issue serious ya maisha yako
 
Kitu ambacho ni maajabu kw wanaume wengi " ile ni familia yangu kiukweli ila mwanamke yule simpendi sina hisia naye kali" unawezaje kufanya kwarudiarudia na mtu usompenda kisha kumuoa kabisa?
 
Ndugu zangu,ukisikia njia panda Kali ndiyo hii!!
Mwaka 2010 niliachana na mpnz wangu nliyempenda sanaaa,ktk kipindi hicho cha mpito nilikutana na msichana mmoja mkoani huko,nikamtongoza ki-maskhara sana,(sikuwa serious kwa sababu sikumpenda kwa kweli) akakubali,nikajisemea moyoni huyu nakula then simrudii tena!

Kweli,nikamla msichana yule,(alikuwa mwaka wa kwanza Chuo cha diploma huko Mkoani),kwa uzembe wetu hatukutumia kinga,baada ya miezi kadhaa akaniambia anahisi ni mjamzito,nilishtuka kweli kwa sababu sikutaka kabisa kuwa na mtoto japo sikuchukua tahadhari kuliepuka hilo. Sikuikataa bali nilimshawishi atoe ile mimba,nikamtumia mpaka pesa ya kutolea,akakataa kabisa kuitoa na pesa yangu akanirudishia!(nikamtumia tena imsaidie kwa mambo yake mengine)

Baada ya mwaka mmoja,alijifungua mtoto anafanana na mimi sanaaa,hata kukataa isingewezekana,nikakubali kulea mtoto. Miaka miwili baadaye nikaanzisha mahusiano mengine,hayakudumu kwa sababu ya huyu mama wa mtoto wangu alikuwa karibu sana nami kimawasiliano juu ya maswala ya mtoto,jambo ambalo lilimkera mpnz wangu hiyo,akaamua kuachana na mimi!

Miaka yote hiyo tulikuwa tunakaa mbali mbali na huyo mama wa mtoto wangu,kutokana na upweke nilimuita Hugo mama wa mtoto nikae naye angalau kidogo niweze kutafuta kumpenda,then tuangalie uwezekano wa kuishi pamoja.(tulikaa kama miezi mitatu hivi kwa matazamio)

Ukweli alikuwa msichana mpole asiye na makuu,nikaamua kumtambulisha nyumbani rasmi,na kutambulika kuwa Huyo ndiye mchumba wangu!(akarejea kwao)

Baada ya mwaka mmoja,nikaenda kwa wazazi wake kuomba ridhaa ya kutambulika pia,wakanipa faini ya kumzalisha binti yao,nikatozwa kiasi fulani cha pesa,baada ya hapo ikawa rasmi pande zote mbili,japo nafsi yangu haikuwa imempenda kwa kweli!!

Mwaka 2014 mimi nilipata kazi,mkoani Tanga,yeye akapangwa Singida (yeye ni mwalimu),basi akawa ananitembelea Tanga mara kadhaa na maisha yakawa yanasonga!
Nilipoanzia kazi kuna binti mmoja alihamia akitokea mkoani Dodoma,tukawa tunasaidiana kazi pale ofisini lakini kwa kweli Moyo wangu ulimpenda yule Dada sanaaa!!(nikawa najizuia sana kuwa naye karibu ili nisijihusishe naye kimapenzi) pasipo kujua kumbe na yeye alikuwa ananipenda sana ila sikuwahi kujua!

Nikawa mwepesi sana kumzungumzia mwanamke wangu(mama mtoto wangu wa Singida) mara kwa mara namuweka profile picture kuongea naye japo ukweli sikuwa na hisia naye kabisa!!!

Kumbe yule dada mgeni alikuwa anakuwa disappointed sana kuona vile,akaomba nimsaidie kutafuta nyumba kwani hakuwa mwenyeji Tanga,nikamuunganisha na mzee mwenye nyumba yangu,akapata apartment pacha na yangu,(hapo ndipo matatizo yalipoanzia)

Tukawa watu wa karibu sana,akija mama wa mtoto wangu wanaongea pamoja na kuishi kiundugu kabisa,na baadaye akiondoka mke wangu anamsifia kuwa mke wangu ni mpole sana!

Akaanza kunisaidia kupika then tunakula wote,kwa kipindi cha kama miezi sita hivi,siku moja tukiwa tunaangalia filamu sebuleni,alionekana kuwa mnyonge sana,akanambia anaomba apumzike chumbani kwangu,nikamruhusu,ilikuwa jioni sana kama saa moja hivi,alipoingia chumbani kwangu mimi nikatoka kwenda kutafuta chakula kwa sababu hatukupika siku hiyo!nilikula huko nikarudi kama saa nne usiku,nikamkuta amelala kabisa,amevua blauzia na amevaa chupi na kanga tu!(kwa kweli nilishtuka nikajikuta kama sipo sawa hivi.

Nilimwamsha lakini hakuamka,niakaingia bafuni kuoga niliporudi alikuwa bado kitandani,nikapanda kitandani nikalala,ilipofika saa saba za usiku uvumilivu ulinishinda nikaanza kumshika maziwa,mapaja,na hatimaye tukaanza romance, na kuivunja amri ya sita!(kumbe lilikuwa kosa kubwa sanaaa)

Tukaingia kwenye mahusiano na ukawa mchezo wetu wa kila siku! Akija mama mtoto wangu ana-pretend kama hakuna kinachoendelea baina yetu,mwaka 2015 miezi ya saba nikata kuvunja mahusiano na mama wa mtoto,nilimshirikisha akaniomba aje tuzungumze juu ya maamuzi hayo,akaja mwezi wa 8/2015,alikaa mwezi mmoja,tuliongea kuhusu kuvunja uhusiano,akaongea kwa Huruma sana na mchozi mengi nikaamua kuahirisha maamuzi yangu,akaondoka!

Mwezi mmoja baadaye akaniambia anahisi ni mjamzito,(mtoto wa pili),nilisononeka sana lakini sikuwa na jinsi,ilibidi nikubaliane na uhalisia,baada ya kuondoka mke wangu tukaendelea na mchezo wetu na co-worker,mara akaanza wivu hataki niongee na mama wa mtoto wangu,nikamwambia ni bora tuachane kuliko kunipa masharti ya eti nisiongee na mpnz wangu mbele yake,na nikamwambia kuwa mchumba wangu ana mimba ya pili,hakufurahia kabisa habari hiyo akaniambia anatamani pia azae,(japo aliongea kiutani utani sana!)

Heeh,mwezi January 2016 co-worker akaniambia amenasa,khaaaa!!!!nikajaribu mbinu zangu zote kumwambia atoe,akasema hawezi kutoa kama sitaki mtoto atamlea mwenyewe,(Jamani wanaume wenzangu,usithubutu kukubali kauli hii kutoka kwa mwanamke,utajuta)

Baada ya miezi kwenda nikajikuta dilemma moja mbaya,huyu wa Tanga,nampenda sana,(sijui kama ndo limbwata au mapenzi natural,nampenda sana!) Wote wana watoto,ila wa Singida anao 2 japo simpendi sana,huyu wa Tanga ana mtoto 1 (nampenda sana,lakini kikwazo kwake ni kwamba kumbe kabla ya kuja Tanga alikuwa ameacha watoto wengine 2 huko kwao,japo hakuolewa)
Kutokana na mazingira aliyopo yule mama watoto wangu wa Singida ilibidi nimnunulie jiko la gas na baadhi ya vitu,jamaa yangu alikuwa anaenda huko nikamuomba niondoke naye kwenda Singida then nichangie mafuta!
Mama yanguuuu!huyu wa Tanga ameleta janga,maana amekuwa akinizuia nisiende Singida tangu juzi,na mimi kwa misimamo yangu nikamwambia siwezi kuacha kwenda ile ni familia yangu,akaniambia ukirudi utanikuta maiti hapa ndani kwako,nikampuuza,nimetoka kununua baadhi ya vitu narudi nyumbani nimemkuta chumbani kwangu akiwa anavuja damu nyingi,(naambatanisha picha mnisamehe wenye hisia kali kuona damu)

Amejichinja mshipa mkuu wa mkono wake wa kushoto,nimepata hofu sana kwa sababu sasa nagundua nipo na mtu hatari sana,kitendo alichofanya leo kimefanya nijutie maamuzi yangu ya mwanzo kabisa,kwanini nilikubali kukaa naye karibu na kuanza naye mahusiano!
Kitendo cha kujichinja mwenyewe si kuna siku anaweza kunivizia aniue huyu mwanamke jamaniii,nawezaje kumtoka mtu huyu katika mazingira haya,na kazini tupi pamoja kila siku!!!

Jamani ndugu zangu natamani siku zirudi nyuma nibadili mfumo wa maisha ila ndo siwezi tena,naombeni mawazo yenu ndugu zangu kwa sababu uwezo wangu wa kufikiri umekoma kabisaaa!!!
Usijutie sana kilichotokea na maamuzi yako, nachokushauri kama wewe ni mtumishi hama huko Tanga, mwachie vitu vya ndani ya nyumba/Chumba chako. Kaishi na Mkeo wa Singida, yule wa Tanga akigundua hivyo hapo baadaye hatoweza kukusumbua maana alifanya anachokijua wakati wanawake huwa wanawaza matukio ya mbali sana
 
Sasa anajichinja mkono, si angechinja koromelo kabisa kama anataka kufa kweli?

Ila wanawake bana tuna taabu sana, yaani akaona ajibebee mimba na yeye ili akumiliki mazima!! Hapo anajua ukimuacha wewe kuja kupata mwanaume wa kumuoa ni majaaliwa maana hiyo idadi ya watoto tu haitamwacha mwanaume salama atakimbia tu
 
Kwako ThaGreatman . Ndugu yangu hapo unaishi na nyoka. Ni suala la muda tu atakung'ata . Hebu jaribu kujiuliza, kama ameweza kujitendea hivyo yeye mwenyewe siku akili yake itakapomtuma kukudhuru wewe atakufanyaje? Nikipata muda ntakufundisha mbinu zakumfanya mwanamke akuchoke, akuchukie na kukuacha mwenyewe bila kukulaumu wala kujilaumu. Asante kwa leo.
Natamani kuwa mwenyewe kabisaaa!!!
Naomba nipe shule hiyo ndugu yangu,niepukane na haya majanga!
Naogopa zaidi kesho yangu kuliko niliyoyashuhudia!
 
Hahaa inachekesha na kusikitisha.

Drama kama series za telenovela au za kifilipino.
Acheni kuiga kila kitu. Yale maisha ya kwenye TV huku kwetu sio maisha halisi.

Ushauri:
Kama wewe ni muislam basi oa wake wawili. kama sivyo basi fanya mpango omba uhamisho achana kabisa na huyo mwanamke wa Tanga sababu ni hatari kama ulivyosema.
Ahsante mkuu,ila ni fundisho kubwa sana kwetu wanaume,bora angekuwa si mfanyakazi mwenzangu,lakini kwa hali ilivyo ni janga,kila siku ofisini tunakutana na wakati mwingine tunapangiwa majukumu ya pamoja!
 
Pole sana mkuu, mshahara wa dhambi ndio huo....., yaani umekuwa dhaifu sana kama mwanaume kwa kutii tamaa zako za mwili..., inakuwaje ufanye maamuzi ya kuzini na mwanamke ambaye huna malengo ya ndoa na yeye pasina hata kutumia kondom. Nina mashaka pia kama hata ulishawahi tumia hiyo zana toka uzaliwe. Kifupi nakulaumu sana kijana kwa kungonoka kizembe hivyo. Ndio lazima niseme.., Je, umecheki pia kama huna VVU? Anyway. asante kwa kutoa fundisho kwa vijana wengine ili wasiingie kwenye mahusiano kama hayo ya hatari bila utaratibu maalum.
Mkuu naogopa sana VVU,ndiyo maana nakuwa na vipimo vya kutosha,kabla sijaingia kwenye mahusiano ni lazima nicheck kwanza afya ya mhusika,lakini kwa hili nimekwama kabisa!
 
Kitu ambacho ni maajabu kw wanaume wengi " ile ni familia yangu kiukweli ila mwanamke yule simpendi sina hisia naye kali" unawezaje kufanya kwarudiarudia na mtu usompenda kisha kumuoa kabisa?
UKiwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. ... Utashangaa hilo ..ila kwa wenye akili ........
 
Back
Top Bottom