Mwalimu ndo mke wako halali wa ndoa, huyo unasema sijui unahisia naye atabaki kuwa mchepuko. Na ukitaka LAANA ikufuate maisha yako yote thubutu kumwacha mwalimu wa Singida nakuambia hakuna rangi utaacha kuona chini ya jua.
Ngoja kwanza nikutoe tongotongo kitendo cha huyo wa Tanga kujikata mkono ni dalili mbaya mbele ya maisha yako ukishi naye, pili umesema ana watoto wawili. Je ulishawahi kufuatilia historia ya kuzaa na kuachana na hao wanaume? Huyo mwanamke amekuzidi akili, kitendo cha kuzaa na wewe huku akijua una mkeo ameshakusoma your strength and weakness na akaona huwa akikufanyia XYZ huwezi kubanduka. Mbaya zaidi hata ukimwacha mkeo wa Singidani hayo mapenzi yake ni sawa na nguvu ya Pepsi, yataisha tooo slowly.
Ushuri wa kijinga: Jenga mazingira ya kumwacha silent abaki kuwa mmezaa mtoto na utamlea mwanao, mwanao akikua mchukue akaungane na mkeo Singidani baada ya kutubu hiyo dhambi kwa mkeo mwalimu.
Pili, fanya juu na chini uhame Tanga either uhamie Singida kama mna ofice branch huko au uhamie kwingine jirani na mwalimu
Tatu, kwa kuwa unalia sana swala la hisia wewe uhame au mkea ahamie mkoa mwingine utakao hamia, urudishe mapenzi ya awali kwa mwalimu