Usiombe mpate CEO asiyejishughulisha kusoma; mtaua kampuni

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nimegundua ipo nguvu kubwa sana katika kusoma kitu kabla ya kusaini. Nimeona Kampuni yetu ikifilisika kwa sababu tu ya CO mpya alikuwa ni mtu wazimamoto asiyejipanga kupitia anachosaini. Jamaa kasaini mkataba wenye mapungufu lukuki akiamini cabnet yake watasoma. Kabinet nalo likaamini Wataalamu wa idara wamesoma na kitu hivyo wakapitisha kwa asilimia mia. Ilipofika kwa bosi akaisaini Kama nyaraka nyingine akiwa amesimama. Leo hii alichosaini kimepunguza wateja na malalamiko ni mengi sana mtaani kwa wateja wetu

Alichofanya kawaita watu walewale waliompotosha wakae watafute Suluhu ya ghasia na kunusuru mporomoko wa Kampuni. Watu walewale badala wakae wamshauri na kwakuzingatia wanajua ana mambo mengi na Hana muda wakutafakari wakaja na propaganda kwamba wanaolalamika wametumwa na Kampuni shindani. Bosi kwakutumia dola akaagiza walinzi wa Kampuni yetu wamkamate Mkurugenzi wa Kampuni kubwa shindani waakikishe hatoki ndani ili wateja wake wanywee wakati wakiandaa propaganda zaidi.

Lakini pia kwakuwa wateja wetu wanapenda soka, kabinet ikaelekeza msemaji wa timu kubwa mtaani kwetu atoe clip akionyesha kutoridhika na baadhi ya mambo ili wateja wetu waachane na malalamiko ya mkataba aliosaini CO Kampuni kidogo itulie. Mara paap msemaji akajitokeza akatoa audio aliyotoa watu kweli wakaanza kuijadili na masaa yakazidi kwenda.

Badala kabinet litumie muda vizuri kutekeleza maagizo waliyopewa na CO wao wanakalia propaganda na kusema tusiyumbishwe na kelele zao watatulia tu.

Sijui hata kampuni yetu kama itapata mafanikio, nawaza kwenda nchi jirani nikatafute kampuni iliyo seriuos isiyoishi kwa propaganda.

Lakini narudia kosa tulilofanya nikuruhusu kuwa na uongozi usiotenga muda kusoma, wanakimbizana na malipo ya safari wakiamini walio ofisini wanatenda kumbe nao wamelala
 
Umeshaambiwa na mkabinet mmoja kuwa uende ugaibuni ambayo ni jirani kabisa na sisi ukipitie kule kigoma kunakofanyika mtifuano wa mzee wa mpili na mtoa klip.

Baada ya mtanange unavuka boda unabakia huko huko ugaibuni.
 
Hapo kwenye SPIN DOCTORS daah,ni wananchi wachache wataelewa wengi will be gone with the wind halafu ukiachana na kusign wale wenzie wanapoona kile kitabu kikubwa kikitaka kubadilishwa wanahisi watakosa maslahi yao ya miaka mingi wanajijali wachache na lile kundi dogo huku wengi wanazama they don't care.

Wameamua waendeshe kampuni na CEO amekaa wanampatia dossiers na briefings na kumdrive .Wanamwambia tulia kampuni isije kukuponyoka tunaua nyoka kichwani.OMG.
 
Naamini huwa anasoma na waliomzunguka/washauri wake wanamuhamasisha asaini.

Mambo yakivurugika anabaki njia panda kama hivi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom