Usiogope kuvunja miiko kama unaona imeshapitwa na wakati: Abe na NBA dhidi ya watu weusi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,864
Ni miaka ya nyuma sana, Wazungu walikaa chini na kugundua michezo mbalimbali ambayo ingewafanya kuinjoi maisha, kutengeneza pesa na kupata vitu vingine, hapo ndipo walipogundua mchezo wa kikapu (Basketball).

Ulikuwa mchezo mzuri tu, haukuwa ukipendwa sana, walikuwa wanacheza Wazungu tu, hakukuwa na mtu mweusi aliyeruhisiwa kucheza mchezo huo.

Wewe mtu mweusi ulitaka kutufurahisha kwenye lipi? Je, unaweza kucheza mchezo huu? Waliona kabisa watu weusi walikuwa ni Mizinguo, hivyo wakaweka sheria kwamba mchezo wa kikapu hakutakiwa kucheza mtu mwenye ngozi nyeusi.

Miaka ikakatika, kukatokea jamaa mmoja wa Kizungu, huyu aliitwa Abe, alichokifanya ni kutengeneza timu yake ya kikapu ya watu weusi ambao hao wangeucheza mchezo huo kwa ustadi mkubwa tu.

Kwenye timu hiyo kulikuwa na mtu kama Marcus, Goose, Pop, Clifton aliyejulikana kama Sweatwater na mwingine nimemsahau kidogo.

So hii ilikuwa timu iliyokamilika, walikuwa na uwezo wa kucheza kikapu kupita kawaida. Hawakuwa wanahitajika kwenye NBA kwa sababu walikuwa watu weusi. Abe aliwapambania, aliona kabisa vijana wake walikuwa na uwezo mkubwa mno, ilikuwa ni lazima kubadilisha sheria, watu weusi nao waanze kucheza kikapu.

Kwa ukali wao, by then mabingwa wa dunia walikuwa La Lakers, walicheza nao, mabingwa hao walipigwa vibaya na wachezaji hao wa mtaani, tena weusi.

Miaka ikasongea. Kwa namna walivyokuwa wakicheza ilikuwa ni kama Brazil kwenye soka, yaani walikuwa wakicheza ile kikapu ya mtaani, sasa iliwapa shida mara ya kwanza mpaka pale sheria zilipobadilishwa kwamba unaweza kuuchezea mpira unavyotaka kucheza.

Wazungu waliweka sheria za hovyo sana kuwanyima watu weusi kuinjoi maisha yao kwenye michezo, na Wazungu haohao wakawapa fursa watu weusi kuinjoi maisha yao kwenye masuala ya michezo.

Ubaguzi ulikuwa mkubwa mno lakini watu waliishi na kutusua humohumo. Leo unapouona mchezo wa kikapu jua ulikuwa ni kwa ajili ya Wazungu tu ila kuna watu walipambania mpaka watu weusi nao kupata nafasi ya kucheza mchezo huo.

Kwa sasa kikapu inachezwa na watu weusi wengi, wanatengeneza pesa nyingi mno. Pamoja na hayo yote, bado wataendelea kumshukuru Abe na wenzake waliokuwa kwenye bodi ya NBA ambao waliona fursa kupitia watu weusi.

Kwa kuwaangalia Sweatwater na wenzake walivyokuwa wakicheza, waliona kabisa kuna pesa mbele yao. Walipowaruhusu kucheza, ni kweli NBA ikapata mashabiki wengi na kupata pesa nyingi sana.

Abe alipendekeza mpaka kuwe na points 3, yaani mtu akirusha mpira kutoka umbali fulani, isiwe points 2 bali 3, baadaye waliipitia na kuona inafaa, wakaiingiza kwenye sheria zao.

Kila sehemu kuna sheria ila jitahidi kubadilisha sheria hizo kwa manufaa ya baadaye, kila sehemu kuna utaratibu, hii isikunyime kuingiza utaratibu wako kama tu utaona kuna manufaa kwako.

Utaratibu wa Waarabu na Wahindi wanapenda kuoana wenyewe kwa wenyewe, bro, ukipata nafasi, nenda kavunje huo utaratibu wao uchukue jiko.
 
Shukrani mkuu

Ila unge edit kichwa cha habari hakuna neno "husiogope" kwenye kiswahi bali ni "usiogope"
 
Back
Top Bottom