Usiogope kupambania malengo yako, kisa uoga wa kutofanikiwa

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,114
52,848
Sasa nisikilize! Leo nitawaambia mambo kadhaa ambayo naamini yanaweza kukufanya ufahamu ni kwa namna gani kuna watu wanatake risk kwenye mabiashara yao makubwa, wewe si unaogopa! Basi poa.

Kwenye hii dunia mpaka sasa hivi hakuna mtu anayejua kutengeneza kiki kama Kanye West! Hapa kuna watu hata Kanye mwenyewe hawamjui! Inanishangaza.

Mchizi kila siku anakuwa na mambo yake. Watu wanamsema amekuwa kichaa lakini jamaa ni genius tu, anajua namna ya kupiga mapesa mengi kupitia mambo hayohayo ambayo unahisi amechanganyikiwa.

Maisha ya Kanye West sometime nayafananisha na yule Steve wa Shoo ya Family matters! Steve alikuwa nerd, dweeb lakini dogo alikuwa genius. Aligundua mambo mengi mno mpaka chombo cha kwenda mwezini, ila kishuleshule kila mmoja alimuita nerd, naye jina hilo akalikubali kwamba kweli mimi sina akili. Kila pepa alipiga A+ zaidi ya waliokuwa wakijiona wana akili.

Sasa huyo ni sawa na Kanye West. Watu wanasema jamaa ni kichaa sana lakini kitu cha ajabu kila leo anatengeneza pesa tu. Sasa kuna mambo mengi yanaendelea kwake, yametokea na yanazidi kutokea.

Mchizi akajipa ubunifu wa mavazi na viatu. Kwanza hayo mavazi ukiyaona, unasema kabisa haya siwezi kuvaa hata nishikiwe bastola, acha na hayo, viatu je? Ndiyo kabisa huwezi kuvaa, ila sasa daah! Kupitia vitu hivyo mchizi akatengeneza sana pesa.

Akaingia makubaliano na Nike. Kwa nini? Ni kwa sababu alitamani sana mzigo wake wa viatu ufike mbele zaidi. Nike akapiga pesa kupitia Kanye West, tena pesa nyingi tu. Ikamfanya Kanye West kuwa bilionea mkubwa, yaani alimzidi mpaka Jay Z.

Sasa bhana Kanye West akawa na akili fulani hivi kichwani mwake. Akawaza na kuwazua akaona mbona hawa Nike kama nawatajirisha? Mbona naweza hata kusimama mwenyewe, hivi siwezi kufanya kitu?

Alichokiwaza Kanye West wengi tunakiwaza ila mwisho wa siku hatutake risk, tunaogopa sana. Na kila anayetake risk tunamuona mjinga sana na hana akili na kwa uwezo wetu wa kufikiria wa kimasikini tunaanza kumchukia.

Mfano mzuri Harmonize. Aliamua kutake risk kutoka WCB, tukamuona mshamba, hana akili, yaani miongoni mwa wajinga tukasema ni huyo jamaa. Unaondokaje WCB sehemu ambayo kila msanii anatamani kwenda?

Kuna mambo huwezi kuyafanya mpaka utake risk, kuna sehemu huwezi kufika mpaka utake risk. Ili uwe bilionea mkubwa, hutakiwi kuwa chini ya mtu. Wewe ushawahi kusikia mfanyakazi bilionea? Labda uwe unaiba, vinginevyo utabaki ulipokuwa milele.

Sasa Kanye West akapiga hesabu zake. Akajua kabisa sasa hivi mimi ni bilionea lakini nikijitoa Nike, nitashuka sana, pamoja na kushuka, naamini kuna siku nitarudi na kuwa bilionea mkubwa tu. Akaamua kutake risk.

Sasa sikia! Wewe si unaogopa kutake risk, sasa mwenzako akafanya hivyo. Akasema anataka kufanya biashara peke yake, kama utataka kusambaza viatu vyake, wasiliana nami kwenye email hii hapa.

Sasa email alizozipokea ndizo zikampa kiburi. Akaona kama watu wengi hivi wanataka kusapoti, kwa nini nisiondoke Nike. Akaitwa na mtangazaji Noriega, akafanya interview yake ya kibabe juzikati, mazima akajitoa Nike. Kama alivyotabiri, kweli akapoteza mapesa mengi sana, akatoka kuwa bilionea mpaka milionea.

Sasa hivi ukimgoogle utaona ana utajiri wa dola milioni 400. Mwanzo alikuwa na utajiri wa dola bilioni 6. Unaona mchizi alivyotake risk.

Sasa amekuwa huru. Kwa hesabu zake zinamwambia ataingiza pesa nyingi sana, ila pesa atakazoingia zitakuwa zake kama zake. Amekwishawasiliana na maduka makubwa. Yote yanahitaji bidhaa zake, amekwishaiona pesa nje nje, na jamaa atafanikiwa kwa kuwa tayari kashajijengea jina lake, hakuna wa kumnyang’anya hata kidogo.

Kanye West angekuwa Bongo, tungemchukia. Kiuhalisia hapa Bongo hatupendi tu kuwaona watu wakitake risk maishani mwao, ndiyo maana tunasema umasikini ni laana. Yaani ukiwa masikini, hata kufikiri kwako hakuwezi kulingana na tajiri. Ukibisha kwenye hili, bisha tu.

Umasikini unaleta chuki, masimango, hasira na mambo mengi machafu. Unaweza ukajikuta unafuatilia mambo ya watu kuliko kufuatilia mambo yako. Tafuta pesa.

Kanye West ni mfano wa kuigwe. Si kila anayetake risk anafanikiwa ila kitendo cha kuthubutu tu napo ni uanaume kwa kuwa kuna wengi wameshindwa kufanya hivyo.

Mimi namuombea mafanikio yeye na wote waliothubutu kujitegemea. Hata kama wewe uliacha kazi mahali ili ufanye mishe zako, nakuombea Mungu ufanikiwe.

Haya makampuni makubwa hayataki utake risk, wanajua ukifanya hivyo utafanikiwa. Hii ndiyo sababu maofisini mabosi wanakutisha tu, eti ukiacha kazi utateseka, utapata tabu sana, sijui hivi na vile.

Bosi hataki ufanikiwe. Ukinunua gari, anachukia kwa kuwa anaona umeanza kufanikiwa hivyo utamkimbia. Nike walikwishaona Kanye West ni pesa, kitendo cha kujiondoa kwake kwao wameona kabisa jamaa kaondoka na mapesa mengi mno.

Take risk...anzisha mabiashara yako, yakianza kwenda sawa, acha kazi na nenda kayasimamie.
Screenshot_20230224-022318_1.jpg

Screenshot_20230224-022435_2.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom