muhomakilo jr
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 15,873
- 14,824
Nimekusoma kwa nguvu ya tano Wakili Msomi..
Mkuu Pressure Na Majungu Kazini huwezi Kuviepuka Especially Tanzania,cha Msingi ni Kutafuta Namna bora ya Kupunguza Pressure,Na Jitahidi Upande wako usimpige MTU jungu....Penye Riziki hapakosi Fitina,Unaweza hata Ambiwa kuwa Ohh Kazi Umepewa,Mara Huna qualifications,Au tuu Mchango wako Kazini Bosi zako wasiutambue....ila Nasema Pigs Kazi,MUNGU huwa Hamtupi mja wake,jiendeleze Kwenye hiyo Fani tumia Fursa Kujifunza Kwenye Eneo lako,jenga Tabia ya Kupuuza na Kusamehe...hapa lazima pia Uwe Unamuomba MUNGU.Mi niliacha kazi kiwanda kikubwa cha bia kwa ukiritimba mwingi, majungu, kutiana presha. Siku naacha kazi kwa mshahara ule hakuna alie amini.
Niliingia kitaa na kamtaji kangu na kuanza kupiga ruti za Nairobi kupeleka mali na kurudi na mali.
Mambo yakaenda sawiaaa.
Japo sasa mziki wa magufuli nausoma vzr, nishapigika sana na TRA. Nafikiria kutafuta kazi tena, sasa sijui nitapata ya mshahara ule?
Hongera sana Sana MkuuHabari zenu wana JF? Ni matumaini yangu kila mmoja wetu hapa ameweza kuiona siku ya leo. Bila shaka ni jambo la kushukuru sana maana siyo wote waliolala jana na wameamka leo.
Bila kupoteza muda ngoja niende kwenye hoja ya msingi. Ni kwamba Mwana JF usipende kung'ang'ania kazi inayokuletea maumivu na mateso mengi na kila ukijitahidi mwisho wa siku unaambulia tu maumivu bila hata kuona faida ya hiyo kazi.
Ngoja niwape historia fupi ya maisha yangu kielimu. Ni kwamba nilisomea ualimu katika chuo fulani hapa Tz. Baada ya kumaliza niliajiriwa hapa jijini Dar. Pamoja na kuwa mwalimu maisha yalizidi kuwa magumu sana mpaka ikapelekea nikate tamaa. kwa sababu kila nilipopata mshahara watumiaji walikuwa wengi sana mfano nyumbani kwetu walitaka hela, hela ya nauli kwenda kazini, Hela ya kununua chakula, Hela ya kunununua nguo na kodi ya nyumba etc.
Hivyo basi, nilijikuta nachukia jiji la Dsm na kazi ya ualimu kutokana na adha nilizokuwa nakumbana nazo. Ingawa niliendelea kumuomba Mungu asaidie maisha yangu yawe mazuri lakini niliishia kuwa mkopaji mkubwa na hatari katika maduka ya mtaani kwangu. kitu kilichopelekea kuchukiwa kwa sababu ya kutolipa madeni. Nilikuwa sifanyi hivyo kwa kupenda bali ukata ndiyo uliyoniandama kwa kiasi kikubwa.
Pia kutokana na hali kuwa ngumu nyumbani kwetu yani kwa wazazi wangu walianza kuniona kama nina roho mbaya maana walipoomba hela nikawanyima walinilaumu sana bila kujua kwanini wananyimwa hela.
Hali ilizidi kuwa mbaya sana mpaka pale nilipokutana na rafiki yangu pale Posta ya zamani nikiwa nimechoka sana nimekuwa kama zee la miaka kwa sababu nilikuwa navaa mibwanga ya nguo kama pepekale na viatu vimelika kisigino kama mtu aliyetoka kijijini jana kuingia mjini.
Ilibidi tukae sehemu tuongee kidogo ingawa alinishangaa sana kwa ile hali. katika kumpa mchakato mzima kuhusu maisha nayopitia alisikitika sana na akanishauri niachane na fani yangu ili nihamie kwenye fani yake kwa kunihakikishia kuwa hakika nitaishi maisha mazuri sana.
Rafiki yangu alikuwa ni Wakili na alikuwa na maisha safi sana. Hivyo basi alinishauri nianze kusoma fani ya sheria mara moja. Ilibidi nijiunge na Open University nikaanza kuchimbua madini na vitu vingine akiwa ananisaidia yeye.
Mwisho wa siku nikahitimu masomo yangu akanipa ajira kama Legal officer katika LAW FIRM yake. baada ya miezi sita akaniambia nifanye taratibu za kuwa wakili baada ya kuona nimeanza kuwa smart katika fani ya sheria.
Nilifanya taratibu zote za kuwa wakili na nikawa nimekubaliwa na kikaapishwa mara moja. Hivyo niliendelea kupiga kazi katika LAW FIRM nikiwa kama ASSOCIATE ADVOCATE. Kiukweli nilianza kushuhudia maisha yanabadilika kwa kiwango kikubwa kwa sababu hela niliyokuwa napata katika fani yangu ilikuwa ni mara kumi ya hela niliyoipata kwa muda huo na mpaka sasa hivi katika fani hii ya sheria.
Kiukweli maisha yalibadilika mpaka wote walionizunguka na walionitegemea walikuwa hawaamini kabisa. Hivyo basi ilipelekea kuendesha maisha yangu vizuri sana bila wasiwasi wala kubahatisha.
Mwisho, Fanya uamuzi sahihi using'ang'anie unachokifanya wakati kinakupa mateso na huenda hiyo kazi ndiyo chanzo cha umasikini wako. Badilika kwanza wewe hakika utakuwa mtu yeyote hapa duniani. Sina nia ovu yoyote wala kuleta dharau kwa mtu yeyote.
"BADILIKA WEWE KWANZA, KUTOBOA KATIKA MAISHA NI SUALA RAHISI SANA"
Siyo kwenye ualimu. Utakula vumbi chaki weee. Ukianzsha twisheni utakula vumbi pia na wanafunzi 10,20Mkuu Pressure Na Majungu Kazini huwezi Kuviepuka Especially Tanzania,cha Msingi ni Kutafuta Namna bora ya Kupunguza Pressure,Na Jitahidi Upande wako usimpige MTU jungu....Penye Riziki hapakosi Fitina,Unaweza hata Ambiwa kuwa Ohh Kazi Umepewa,Mara Huna qualifications,Au tuu Mchango wako Kazini Bosi zako wasiutambue....ila Nasema Pigs Kazi,MUNGU huwa Hamtupi mja wake,jiendeleze Kwenye hiyo Fani tumia Fursa Kujifunza Kwenye Eneo lako,jenga Tabia ya Kupuuza na Kusamehe...hapa lazima pia Uwe Unamuomba MUNGU.
Mkuu nimezungumzia kazi kwa ujumla sio ualimu tuu nimezungumza GENEARL...Siyo kwenye ualimu. Utakula vumbi chaki weee. Ukianzsha twisheni utakula vumbi pia na wanafunzi 10,20
Maisha yakikusaliti unajikuta unakuwa mtaalamu kila eneo mkuu.Hongera sana Sana Mkuu
Ulisomea Combination Gani A-Level?
Pia Ni Somo Kuwa unaweza Kufanya Kazi yeyote na ukaifanya Vyema sana sana Hata Kama Hukuisomea
Au Uka Diversify Masomo!
Mkuu umepotea sana sana MkuuSasa mimi niliyeishia form 4 na sasa ni mbeba maboksi nina options gani mimi?
Life sucks man.
I have a dead-end job. I'm not smart.
*** it.