Usindikaji na uhifadhi wa nyanya kwa matumizi ya baadae

Ona Sasa

Member
Jul 2, 2009
65
11
Kumekuwepo na utaratibu wa wakulima wetu kulima zao hili kwa pamoja, hii inatokana na hali ya hewa ya mahali husika pamoja na utaratibu wa watu kufanya kama wengine. Hali hii husababisha zao la nyanya kushuka ghafla bei sokoni kutokana na wingi wa nyanya.

Tumeshuhudia watu wakipata hasara kubwa bila kutalajia na hii inawaingiza wadau wengi kuanzia kwa mkulima mwenyewe, mlanguzi,mnunuzi wa jumla na mnunuzi wa rejareja na pia haishii hapo bali hata majumbani unakuta mlaji ameweza kununua nyanya nyingi kwa bei rahisi lakini hana ujuzi wa kuzihifadhi matokeo yake zinaharibika.

Sote tu mashuhuda kwamba, baada ya muda mfupi nyanya zinatoweka sokoni na zikipatikani zinakuwa hazishikiki bei zake , hivyo kuwafanya waagizaji wa nyanya za makopo kutoka nje kufanya kazi yao, ukizingatia hizo nyanya za makopo sio nyanya halisi kama ile inayotoka shambani au hii ambayo tunaelekea kujfunza kuhifadhi yenye kila aina vitamin za kutosha.

Tukiwa tunaelekea kwenye Tanzania ya Viwanda na huimarishaji wa uchumi wa ndani na kukuza pato la kila mwananchi na taifa kwa ujumla, tumeona kuandaa.
Piga 0756 41 95 49 Kupata kitabu

Usindikaji wa Nyanya Booklet.jpg
BxV_h2EfQDuKeIRYZzoBgeMGhfF9LvxjxryWpinIiz4g73Skkrp3yiL5bEWxYMN14vkimG-TwfIxNN7U_2X69MICNUc-4l...jpg
DklyvvlASzVQKejYBaFfD0Jd9f4rv5J7PTs_EWXSE6rBd2T1_UXmwfu-Qy_4WGHRxmIPz1m6ToGLlNAEN8SJ-AtOfIcZpt...jpg


 
kitabu kimeainisha njia ngapi za kuhifadhi?

NYANYA unaweza kutengeneza pombe?
 
Hiki kitabu kina ufafanuzi wa hatua kwa hatua ukiambatana na picha kuhusu kusindika na kuhifadhi nyanya. Katika hiki kitabu kuna taarifa ambazo zitamfanya mjasiliamali kuelewa zaidi kwa sababu ni njia rahisi na mazingira ni rafiki kwa kila mtu ambaye angependa kujua kuhusu uhifadhi wa nyaya kwa muda mrefu.

Tutaonyesha kwa ufasaha na kiundani njia kuu tatu za kusindika na kuhifadhi nyanya; kwa kuzitaja majina ni :

  1. UTAYARISHAJI WA NYAYA NZIMA ILIYOMENYWA NA KUHIFADHIWA (Whole peeled tomato preserves)
  2. NYANYA ILIYOSAGWA(Juisi Nzito ya Nyanya) NA KUHIFADHIWA (Tomato pulp preserve) na
  3. NYANYA ILIYOKAUSHWA NA KUHIFADHIWA (Solar dried tomato preserves)
Hii pia itawasaidia wakufunzi ambao wanaendesha mafunzo yao kwa vikundi mbali mbali vya wajasiliamali, wakulima wadogo na wa kati ambao wamekuwa katika matatizo ya kulazimika kuuza nyanya kwa vyama au wafanyabiashara yaaani walanguzi kwa bei za kutupa kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuhifadhi kilichosazwa. Hivyo basi mafunzo haya ni muhimu pia kwa wafanya biashara walanguzi ambao wakifikisha nyanya zao sokono wanakuta bei ni tofauti na kilichotarajiwa na kujikuta wameingia hasara na kushindwa kulipa hata madeni yao kama wamechukua mikopo kutoka taasisi mbali mbali za kifedha.



Kitabu hiki kitakuwa na picha nyingi kwa madhumuni ya kurahisiha kuleta uelewa hasa kwa baadhi ya hatua za usindikaji zinavyoendelea. Hivyo basi mtumiaji atakuta picha na chini yake maelezo ni nini kinafanyika. Unaweza kuona mazingira tofauti ya picha ambayo si kama ya kwako, lakini vitu vyote vinavyotumika vinapatikana sehemu zote katika jamii zetu
 
Back
Top Bottom