Mkulima wa nyanya usitupe nyanya zako zilizo kosa soko fanya hivi kuziongezea thamani

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Wakulima wengi wa nyanya wanapata hasara kutokana na kuzalisha nyanya ambazo zimezidi mahitaji ya soko au Sababu nyingine ni uhaba wa masoko ,Kiasi kikubwa cha nyanya zinaoza shambani au sokoni ni kwa sababu wakulima wengi hawana/hawajui jinsi ya kuhifadhi nyanya zao

Kwa utafiti wangu usio rasmi nimebaini Wakulima wengi wanapoteza zaidi ya nusu ya nyanya zinazozalishwa.

Hasara kubwa wanaipata Kipindi Cha msimu wa mavuno , nyanya nyingi zinaharibika kwa kusubiri wanunuzi na zingine zinaharibika tu kutokana asili ya zao lenyewe lilivyo(laini) hivyo inawalazimu wakulima wengi kuuza kwa bei ya hasara wengine wanazitupa kabisa kwa kukosa wateja.

Sasa Njia nzuri ya kuzihifadhi na kuongeza thamani nyanya zako zilizoharibika (sio kuoza) na ambazo zimekosa soko ni kuzifanya kuwa unga (tomato powder).

Njia hii ni nyepesi Wala haiitaji gharama kubwa , unachotakiwa kufanya unazikatakata nyanya zako kisha unazianiaka juani, baada ya kukauka utazisaga kwa blenda au kwa kutumia kifaa chochote ilimradi iwe unga

kutengeneza tomatoe powder inasaidia kupunguza upotevu wa nyanya baada ya mavuno lakini pia inasaidia kendelea kutumia nyanya nyakati za uhaba wa nyanya,

hivyo ni wazo Bora pia ukiamua kufanya kibiashara , na uzuri ni kwamba tomato powder ikihifadhiwa vizuri inakaa kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita kwahiyo kazi kwako mkulima ulifanye kuwa wazo kamili au ulitume pindi nyanya zikishindwa kutoka sokoni.
IMG_20230831_165714.jpg

screenshot_20230831-183313-png.2734710
 
Attachments

  • Screenshot_20230831-183313.png
    Screenshot_20230831-183313.png
    83.9 KB · Views: 50
Huo muda sasa, halafu hata kutengeneza hicho kichanja wengi wataona ni gharama kubwa hivyo ni bora wapate hasara na kulima tena
Kichanja hakina gharama mkuu ukizingatia upatikanaji wa meterial ni mwepesi na bei nafuu,ni kazi ambayo unaweza kuifanya hata mwenyewe bila kumlipa mtu au kama utakosa muda wa kufanya cost yake still ni ndogo .

Labda kama hayuko interested lakini ni Njia nzuri sana ya kuongeza thaman yanya zako
 
Binafsi nimekuelewa na ntafanyia kazi. Tena hii sisubir nyanya zikose siko ntaanza na hzihizi.
Asante kwa kunielewa mkuu, Mimi sifanyi kilimo hiki ila naona jinsi wakulima wengi wanavyoteseka kwa kupoteza mazao hasa ule msimu wa nyanya unakuta tenga la linauzwa kwa ya hasara ,

Mimi pia nataka nianze kufanya hivyo , ila nakushauri anza kidogo kidogo usikilizie soko lake
 
Wazo zuri sanaa,hili Nyanya huwa adimu muda flan na mudaziakua nyingi kuliko mahitaji sokoni.
Wenzetu masoko yao ni ya uhakika na wana technology ya kuzihifadhi yanya kwa ajili ya kutumia kipindi Cha uhaba ,kwahiyo wakulima wanazalisha kulingana hitaji la soko na ikitokea uzslishaji umekuwa mwingi basi nyanya zinahifadhiwa.

Lakini sisi huku kipindi Cha mavuo mazao Yanakuwa mengi hitaji la soko dogo na hatuna sehemu ya kuhifadhi kusubili soko, hapo ndio kilio Cha wakulima wa nyanya kinakuja mkulima anaona Bora auze kwa ya hasara.
 
Ni idea nzuri lakini ni wangapi wananunua powder?
Ushauri mzuri ila nafikiria pia kama wakitengeneza tomato paste au chopped kwa kuzihifadhi kwenye makopo
Ila kama gharama ni kubwa wanaweza kutafuta soko la viwanda vya nyanya kama vipo
 
Hiyo idea yako haitekelezeki kwa mazingira ya Tanzania kuna wadau kibao walikuja na miradi kabisa iliokua inafadhiliwa kutoka nadhan n usa kama sio Uk wakagawa na mashine za kukaushia lakini bado walichemka.

Ukisema watu waanike kienyeji utaishia kulisha watu sumu kuvu.
 
Hili ni wazo zuri,swali ni kuwa je ukiuza hiyo Tomatoe powder itanunulika...?
Hapo ni wewe tu sasa kufanya marketing strategy nzuri kwasababu ni bidhaa ambayo haijazoeleka na wengi ila kwenye ubora na efficiency ni sawa tu matumizi ya nyanya za kawaida, kwahiyo hapo hautauza kitu Cha tofauti ni nyanya tu zilizo kwenye muundo wa unga.

Yani hapo ni kudeal na kitu kinaitwa 4 Ps product, price, place and promotion.
-product, hapa ni kuchagua nyanya ambazo hazijaharibika ili upate products nzuri
-price, Select bei rafiki kwako na kwa wateja
-place Wateja wako wanaweza kuwa wamama ntilie au wamajumbani
-promotion
.Kwakuwa ni bidhaa mpya kwa wengi ifanyie promotion ya kutosha

Mimi na amini hakuna kitu ambacho hakiwezekani ni kufocus tu
 
Hiyo idea yako haitekelezeki kwa mazingira ya Tanzania kuna wadau kibao walikuja na miradi kabisa iliokua inafadhiliwa kutoka nadhan n usa kama sio Uk wakagawa na mashine za kukaushia lakini bado walichemka.

Ukisema watu waanike kienyeji utaishia kulisha watu sumu kuvu.
Biashara ni pamoja na kuangalia wenzio wameshindwa wapi ,hao walifeli pengine labda kwenye masoko nadhan ukiwekwa mkakati mzuri unaweza kuvuka mbele zaidi ya waliko inshia wao.
 
Hapo ni wewe tu sasa kufanya marketing strategy nzuri kwasababu ni bidhaa ambayo haijazoeleka na wengi ila kwenye ubora na efficiency ni sawa tu matumizi ya nyanya za kawaida, kwahiyo hapo hautauza kitu Cha tofauti ni nyanya tu zilizo kwenye muundo wa unga.

Yani hapo ni kudeal na kitu kinaitwa 4 Ps product, price, place and promotion.
-product, hapa ni kuchagua nyanya ambazo hazijaharibika ili upate products nzuri
-price, Select bei rafiki kwako na kwa wateja
-place Wateja wako wanaweza kuwa wamama ntilie au wamajumbani
-promotion
.Kwakuwa ni bidhaa mpya kwa wengi ifanyie promotion ya kutosha

Mimi na amini hakuna kitu ambacho hakiwezekani ni kufocus tu
Unrealistic
 
Ni idea nzuri lakini ni wangapi wananunua powder?
Ushauri mzuri ila nafikiria pia kama wakitengeneza tomato paste au chopped kwa kuzihifadhi kwenye makopo
Ila kama gharama ni kubwa wanaweza kutafuta soko la viwanda vya nyanya kama vipo
Viwanda na masoko vipo mkuu shida inakuja wakati wa mavuno uzalishaji unakuwa mkubwa kuliko mahitaji sasa shida inarudi kwa wakulima wanauza kwa kiwango kidogo kilicho baki wanakuwa Hawana pa kupeleka ,hivyo badala ya kudump bidhaa zilizo kosa soko basi ni Bora mkulima afenye hivi hili kuepuka hasara ndio hoja yangu mkuu
 
Back
Top Bottom