Usimpeleke mwanao shule za bweni

Usimpeleke mwanao shule za bweni

Siko hapa kukupangia namna ya kuishi na familia yako, ila naomba nikushauri kitu;

kumpeleka mwanao akaishi bweni kwanza ni ulimbukeni, kama mtoto ana akili, hata akisoma day atafaulu tu.
wapo wanaosoma wakiwa boarding awali mpaka form4.. na bado wanafeli!

hasara kubwa anayoipata mtoto ni kukosa malezi ya wazazi. Mtu aliesoma katika mazingira hayo, hata ukubwani utamjua tu!

sasahivi tuna vijana mpaka wazee wa hovyo sana lakini cha ajabu ni wasomi (walikosa malezi ya wazazi)

tunawapa wanawake lawama za kila rangi kumbe sio wao bali "walikosa malezi bora ya wazazi": binti wa for4 & std7 alielelewa na wazazi ni bora (anaweza kuwa mke bora) kuliko degree holder aliekulia boarding kipindi chote cha makuzi yake

kuna msemo huu:- "asiyefunzwa na wazazi dunia itamfunza"

umekosa nini mpaka mwanao ukamkabidhi mikononi mwa walimwengu wamfunze?

Kaa karibu na mwanao kwa faida yake, huko mbele kuna hatari.

NB. Nazungumzia watoto under18
Ni ujinga usio kifani kumpeleka mtoto wa shule ya msingi bweni.Ni upuuzi upuuuziii ban upuuuuuuuziiiiiii!
 
Na bora tabia mbaya zote ila USHOGA NA USAGAJI huko wengi ndiko wanakojifunzia
 
Siko hapa kukupangia namna ya kuishi na familia yako, ila naomba nikushauri kitu;

kumpeleka mwanao akaishi bweni kwanza ni ulimbukeni, kama mtoto ana akili, hata akisoma day atafaulu tu.
wapo wanaosoma wakiwa boarding awali mpaka form4.. na bado wanafeli!

hasara kubwa anayoipata mtoto ni kukosa malezi ya wazazi. Mtu aliesoma katika mazingira hayo, hata ukubwani utamjua tu!

sasahivi tuna vijana mpaka wazee wa hovyo sana lakini cha ajabu ni wasomi (walikosa malezi ya wazazi)

tunawapa wanawake lawama za kila rangi kumbe sio wao bali "walikosa malezi bora ya wazazi": binti wa for4 & std7 alielelewa na wazazi ni bora (anaweza kuwa mke bora) kuliko degree holder aliekulia boarding kipindi chote cha makuzi yake

kuna msemo huu:- "asiyefunzwa na wazazi dunia itamfunza"

umekosa nini mpaka mwanao ukamkabidhi mikononi mwa walimwengu wamfunze?

Kaa karibu na mwanao kwa faida yake, huko mbele kuna hatari.

NB. Nazungumzia watoto under18
Nakubaliana na wewe kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumpeleka mtoto boding shule za msingi ni mbinu ya wazazi kukwepa majukumu ya malezi kwa mtoto. Umri huu (miaka 0-14) mtoto anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa wazazi na si mtu mwingine. Kwa level ya sekondari mtoto kukaa bweni si vibaya
  • Ndio maana Kenya wamefuta huo ujinga wa boarding kwa primary education. Niliwaona hoja za CS wao, wapo vizuri.
  • Tz limbukeni; biashara zitakwamisha.
 
Najivunia kusomea boarding school tena boys tu nikiwa na miaka 14. Hakika nimemiss hekaheka za kutufunza na kutupa malezi yaliyojazia yale ya wazazi. Hakika Popote ulipo Mwalimu Laban Kansimba na timu yako ya Nyakato Sec ya bukoba kongole sana. Ukimpeleka mtoto shule ya boarding kwa mentality ya kuiga ujinga na kufuata mkumbo hakika atauiga kweli. Boarding haina shida shida ni wewe mzazi na huyo mwanao
Hujamuelewa mtoa mada anazungumzia boarding kwa watoto wa primary. Miaka 14 umekuwa tayari.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
kama Una muda wa kukaa na mtoto muache day Ila harakati za maisha siku hizi zimefanya watu wengi kukosa muda wa kumfatilia mtoto tabia na maendeleo yake kielimu. Kama Una huo muda ni mara Mia ukae Naye. Ila kama huna muda mpeleke boarding. Ile ratiba Tu ya shule ni minyoosho tosha, jioni prepo na usiku prepo, vp nyumbani unaweza kuzisimamia hizo prepo? English speaking akiwa shule ni muda wote asubuhi, mchana na usiku hivyo anawahi kumaster lugha kuliko wa day, Kama kuna vitu hajaelewa ana muda wa kutosha kushirikiana na wenzake akaelewa.

kimsingi mzazi Pima faida na madhara uamue maanake nyumbani kama Una muda kuna malezi, shuleni kuna elimu japo zipo shule hata malezi wapo vzr pia. Angalia mazingira ya nyumbani, uwezo wa darasani wa mtoto, tabia yake vitakusaidia kufanya maamuzi
 
Back
Top Bottom