Marufuku ya Bweni Shule za Msingi, Serikali imekurupuka

Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
563
1,544
Serikali imepiga marufuku kwa shule zinazotoa huduma yela bweni kusitisha kwa watoto wa shule za swali mpaka darasa la nne. Shule zemeelekezwa kufanya hivyo baada ya kumalizika muhula wa kwanza mwaka huu.

Ukiangakia ni kwamba huu ni uamuzi ambao umekee sikiasa na kihisia zaidi. Moja kati ya sababu zilizotokewa ni maadili mabaya na kukosa upendo baina ya watoto na wazazi.

Binafsi Kuna sehem nakubaliana na pengine sikubaliani. Nakubali kuwa kwa Shule za Awali sio sahihi mtoto kuwa mbali na wazazi. Na hiki ndio kipindi kizuri kujenga hayo malezi na upendo Kwa mtoto.

Katika mfumo wa maisha ya Sasa kuna mazingira ambayo unaona mtoto kuwa bweni ni salama zaidi kuliko mtaani. Hapa nitaweka sababu chache.

1. Mfumo wa utafutaji riziki
Wazazi wengi Kwa Sasa tunatumia muda mwingi tukiwa mbali na Nyumbani na wengi hulazimika kurudi Nyumbani usiku.

Wengi huchelewa katika harakati za usafiri, umbali wa maeneo ya kazi au kazi zenyewe zinhitaji kuzifanya mpaka usiku. Serikali iache kuamua kwa kufikiria kuwa wote wanao somesha shule za bweni ni watumishi wa umma. Tupo sisi bodaboda ambao tinajibana kusomeaha watoto shule nzuri.

2. Matatizo ya ndoa
Serikali ilipaswa kufanya utafiti kidogo tu kutoka kwen6 data zake juu ya ndoa zinazo vunjika na hatma ya watoto kimalezi. Watoto wengi wa watalaka hupelekwa Bweni kama kimbilio salama ambapo wazazi wote Huwa na Imani zaidi. Baada ya talaka Kila mzazi Huwa na maisha tofauti kiutafutaji hata mahusiano na kukosa ukaribu na mtoto wa mtalaka.

Kuna visa vingi vya watoto kuuwawa au kufanyiwa ukatili na mama au baba wa kambo. Ni rahisi wazazi kukubaliana mtoto aende bweni ambalo wanaamini anakua sehem salama kimalezi na kielimu.

3. Teknolojia
Mtoto kuwa mtaani inamuweka karibu zaidi na maudhui mabaya yakiyopo kwenye mitandao. Tafiti zinaonesha kuwa zaidi ya 80% ya maudhui katika mitandao ya kijamii ni maudhui ya Ngomo.

Ukizingatia hayo utaona mtoto kuwa mtaani inamuweka karibu na maovu ya mtandaoni. Huko bweni ni rahisi kufanya usimamizi wa pamoja kuliko huku mtaani. Selikali haiwezi kuzuwia.

Mitandaoni utakuta Mashoga, Wasagaji, Makungwi na namna nyingi ya maovu yakiwa yameanikwa bila udhibiti, na serikali haiwezi wala haikemei ili kudhibiti.

Tamthilia kutoka nje
Hizi ni tamthilia toka nje ambazo huoneshwa kwa kutafsiriwa kwa Kiswahili. Utakuta kila nyumba watoto wanakesha usiku wakifiatilia hizi filamu ambazo nyingi zinachukua wasatani wa miezi mitatu. Watoto wanakesha wakifiatilia hizi filamu ambazo nazo unakuta maudhui ni Ngomo na Ushoga.

Hizo ni sababu chache tu ambazo hupelekea wazazi kuamua kupeleka mtoto bweni ili angalau kumkinga na kadhia ya mtaani.

Wizara ya Elimu iache mihemko na kuiga Wakenya. Serikali ifanye utafiti na kushirikisha wadau kabla ya kufanya maamuzi ambayo yanawagusa watu. Hakuna mzazi angependa kulipa gharama kubwa kusomesha mtoto endapo serikali ingetimiza wajibu wake wa kuboresha shule za umma na kudhibiti maadili ya mitandaoni.

Maoni yangu

Shule kuanzia darasa la kwanza waruhusiwe kuwa Bweni au Wazazi wapewe fomu maalum wajaze ili kujua sababu ya kumpeleka mtoto bweni.

Tunamrudhisha mtoto mtaani aje kujifunza nini?
 
Nadhani hakukua na ulazima wa kukataza Ila
Wangekataza shule kuwalazimisha wazazi kuwaleta boarding


Kila mzazi Angejipima mwenyewe mazingira yake kuona Kama je inaulazima wa kumpeleka mtoto boding?
Haya ndio maoni yangu.
 
SERIKALI imepiga MARUFUKU Kwa shule zinazotoa huduma yela bweni kusitisha Kwa watoto wa shule za swali mpaka darasa la nne. Shule zemeelekezwa kufanya hivyo baada ya kumalizika muhula wa kwanza mwaka huu.
lea mwanao akikua kua kaiachie dunia..usizani unavyomchukulia wewe kua ni mtoto na dunia inaona ivo ivo..
 
Serikali imepiga marufuku kwa shule zinazotoa huduma yela bweni kusitisha kwa watoto wa shule za swali mpaka darasa la nne. Shule zemeelekezwa kufanya hivyo baada ya kumalizika muhula wa kwanza mwaka huu.
Point zako zote 3 ukizipima kwa undani unagundua ni kama kwamba unajaribu kuyavua majukumu ya mzazi kwenye malezi ya watoto.

Katika hali yoyote ile ya maisha mzazi anabaki kuwa ndio mwenye jukumu la msingi la kumlea mtoto wake.
Kwa mfano kuvunjika kwa ndoa bado haijaondoa jukumu la wazazi kimalezi, kila mmoja atapaswa kuendelea na malezi.

Mnapozungumzia suala la maadili, huko kwenye mabweni ndiko kunaongoza watoto wadogo kuharibika kimaadili, mtoto wa darasa la kwanza anaishi na yule wa darasa la saba chumba kimoja unafikiri anamfundisha kitu gani??

Kwa upande wangu nadhani serikali umefanya uamuzi sahihi kabisa.

WAZAZI TUKAE NA WATOTO WETU TUWAFUNZE MAADILI, TUSIWAACHIE WATOTO WENZAO KWENYE MABWENI WAKAWA NDIO WALEZI WAO.
 
Tumelalamika muda mrefu. Lingine ni hili la wanafunzi kusoma weekend, nalo wanatakiwa waliwekee mwongozo. Sababu shule hazijitambui
Hilo la watoto kusoma wikiendi nahisi ni msimamo wa mzazi tu. Binafsi hakuna mwanangu anayesoma wikiendi. Yawe maamuzi ya shule au ya kwake mwenyewe. Haendi na shule zinajua hilo.
 
Hilo la watoto kusoma wikiendi nahisi ni msimamo wa mzazi tu. Binafsi hakuna mwanangu anayesoma wikiendi. Yawe maamuzi ya shule au ya kwake mwenyewe. Haendi na shule zinajua hilo.
Sekondari nyingi za kutwa zinao utaratibu huu.
 
Sekondari nyingi za kutwa zinao utaratibu huu.
Watoto wengi wa kutwa wanaokwenda shuleni wikiendi kiukweli wanakwenda kwa ajili ya mambo yao binafsi hasa kukutana na wenza wao wa shuleni au mtaani. Sishauri umruhusu mwanao kwenda wikiendi.
 
Naunga mkono serikal yangu..! Niliwahi mpeleka mwanangu baada ya mama yake kwenda masomoni.

Kila baada ya miezi 2 naenda kumchukua mtoto anaumwa, ilikua nikifika pale mtoto amekonda mpaka mishipa ya kichwa inaonekana aisee.

Narudi nae nampeleka hospital hawaoni ugonjwa.

Kwa wakati huo nazidi kuona uchangamfu unaongezeka mara baada ya siku tatu amepona kabisa.

Ilijirudia mara tatu nikaamua kumpeleka kwa bibi yake ambako akawa salama.

Niligundua pale shule wakati wa chakula walimu hawajali nani kala nani hajala.

Pia mtoto alikua na mmba kichani as if kuoga ni shida.

Kibaya zaidi roho iliponiuma ni pale niliposhuhudia katoto ka miaka ka 3 kanaachwa pale shule na wazazi wake katoto kanalia lakini bila huruma mzazi aligeuza kisogo na kutokomea, akaitwa mtoto mkubwa zaidi yake akafika akamnyanyua mpaka bwanini huku katoto kanalia, dah aisee sie wazazi saa nyingine makatili sana.!

Shule za bwani ni hatari kwa watoto maana asilimia kubwa mashoga wanazaliwa humo mashuleni even sekondar school sio salama.
 
Serikali imepiga marufuku kwa shule zinazotoa huduma yela bweni kusitisha kwa watoto wa shule za swali mpaka darasa la nne. Shule zemeelekezwa kufanya hivyo baada ya kumalizika muhula wa kwanza mwaka huu.
We una shule ndiyo maana. Acha kuendekeza maslahi binafsi kwa kuiumiza jamii
 
Back
Top Bottom