Usimkopeshe hela mtu

Mimi anayo yangu 4ml yani wakati ananifata aliniomba mtaji wa duka nikatoa kwa moyo mmoja kweli Mungu sio athumani rafiki yangu huyu amefungua biashara imekubali sana, na mipango ya kuikuza zaidi biashara ananishirikisha kila siku lakini kila napokumbusha hela yangu ni kalenda tu mpk sasa ni mwaka na nusu, inaumiza sana
 

 

 
Wewe kama unajijua ni rafiki yangu kindakindaki nikikukopa ujue sikulipi, marafiki hatukopeshani marafiki tunasaidiana.

Mfano mimi kuna rafiki ambae akinifata hata leo akaniambia nimkopeshe laki tano, kama ninayo nampa. Najua kabisa kwamba hatairudisha, ila pia najua mimi siku nikimuotea ntamkopa zaidi ya hiyo na sitalipa!😁

Kuna best yangu mmoja TV yake ilipasuka kioo, akawa hana TV. Mi nilikua na TV iko idle, akanipiga saundi nimuuzie. Tukakubaliana laki 4. Jamaa akachukua akanipa 250k. Miezi imekatika mi wala sijawahi kumkumbusha. Kuna siku nikam taimu siku najua ana hela, nikamtumia sms saa 12 asubuhi "aisee kaka nimekwama, hebu nitumie 200k chapu ntakurudishia". Jamaa si akaingia mkenge? Ikawa ndio nitolee nahisi baadae aligundua ameshapigwa so wala hajawahi kunidai😂
 
Ila tumetofautiana sana binadamu kila mtu na imani yake mimi binafsi nakopa lkn nikipata tu pesa lazm nirudishe pesa ya watu lkn kuna watu si wastaarabu kabisa wanakopa lkn kurudisha pesa matanga wabongo tubadilike aisee sio maisha mana kuna siku utapatwa na shida ukaja aibika kwa kukosa uaminifu
 
iyo huwa tunaita ngoma droo au bila bila
 

Mkuu, hakuna mtu mgumu kulipa deni, kama mtu unaeonana nae kila siku! Ni heri yule unaemkopesha anapotea mazima, siku akija kuibuka anaweza kulipa. Huyu unaeonana nae kila siku anakua anaona ah, ntampa tuu si yupo?
 
Kesi za madai hata mahakamani hazina tena ile hali ya ukali, mnaweza kumaliza nje ya mahakama na mtu akasepa
Mimi si mzuri sana kukopesha hua natoa ambayo iko ndani ya uwezo wangu
kama unamdai mtu ukampeleka Polisi ndio unapoteza kabisa, unaweza ukawa unadai milioni tano ukaishia kulipwa elfu5 kila mwezi maana lazima waangalie kipato cha mdaiwa na uwezo wake wa kulipa hilo deni
 
Yote sababu ya awamu ya kusomesha watu namba watu pesa hawana
 
Fanya kama umetoa msaada
 
Kuna demu nimemkopesha yaani kila sku ananitengenezea mazingira nmtongozee Ila nkikumbua pesa yngu ata hamu inakata...
 
Mimi kuna mbwa kanipiga 1.5 mil achilia mbali vi 50 hamsini elfu kwa ndugu jamaa na marafiki hivyo vyote nimeshasamehe ila huyu wa 1.5 mil nilishaapa sintomuacha kamwe uzuri nilimkopesha kwaa maandishi na alipo kakimbia kabisa hayupo sasa natembea na rb siku moja tutakutana ishallah .jasho la mtu halipotei hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…