Nimemnyoosha landlady, haamini kilichotokea

Nimemnyoosha landlady, haamini kilichotokea

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
1,077
Reaction score
1,581
Huyu mama anasumbua sana unapokaribia muda wa kulipa rent. Hashindwi kupiga simu Saa Kumi Alfajiri, na kutuma SMS nyingi kama mvua hata kabla muda haujaisha anakukumbusha kulipa pesa.

Na kwenye mkataba ameweka masharti, kipengele namba (5) "Ukiona huna pesa ya pango ijayo, ondoka kwenye nyumba yangu, usizidishe hata siku Moja, tutakerana".

Wiki hii alisafiri, na leo tarehe 20/08, nd'o siku ya kulipa rent.
Mimi niliitisha Kirikuu tangu juzi, nikahamisha vitu vyote na nikamlipa mtu akafanya usafi nyumba yote.

Sasa leo amekuja na watu wa vikoba vyao, amewahakikishia pesa ipo, na anawapa cash (kwa kuwa mimi sijawahi kujitetea, ifikapo tarehe husika nampa pesa yake, hivyo akawa na uhakika).
Hajanikuta, kapiga simu kuulizia hela akiwa ameweka loudspeaker.

Nikamwambia "Nimeona kuwa sina pesa ya pango ijayo, hivyo nimezingatia sharti namba (5) la mkataba wetu. Nimeshahama tangu juzi, funguo anazo binti yako."

Kwa pembeni, nikasikia akina mama wenziye wakisema, "yaani leo toa pesa, au tunasafisha sebule yote, kama ulivyomfanyia Mama Lily mwaka jana".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom