Usimkopeshe hela mtu

BARUA KUTOKA UWABATA

Habari,

Umoja wa wanaume bahili Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ [UWABATA] unawataka wanachama wake waache kukupesha haraka iwezekanavyo na atakae kaidi atachukuliwa hatua kali.

MAKAO MAKUU,​

UWABATA,
CHATTLE.
 
Kopesha kwa maandishi

Usikopeshe Rafiki kizembe...urafiki utakufa na Pesa hakurudishii

Pesa ni kitu kingine man
Umenikumbusha machungu yani mana nlishaanza kuyasahau...binadamu binadamu jaman
Pesa pesa...
Huyu na ushahidi wa miamala na jumbe fupi za maneno so akijaribu kuleta janja atanitambua mimi ni nani.
Mambo yamebadilika mnooo,.
Basi tu, lakini nimejifunza sikopeshi hata iweje. Kuna taasisi za kufanya kazi hiyo
Uchoyo unawasumbueni
Ukimkopesha mtu bila dhamana unakuwa hujamkopesha bali umemfadhili.Hakuna mkopo usio na makubaliano yenye dhamana hata kama ni tsh 20000
Sikopeshi tena mtu acha tu niwe mbaya
PIGILIA MSUMARI HAKUNA KUKOPESHA PESA YAKO MPAKA UKIRIDHISHE IKIWA KWELI UTALIPWA HELA ZAKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku sio nyingi nitamfunga kaka yangu kwa sababu ya kushindwa kulipa 2m. sasa hivi hapokei simu. Nimemtumia sms nitamnyoosha na undugu ufe tu. Usikopeshe ndugu mdau
tukisema kimaandishi maana yake kuna shahidi na dhamana kama nyumba,plot nk. akishindwa kulipa unabeba kiwanja. akifa je nani atakuamini
Ukipata marafiki madoni hamna upuuz kama huo.
Kama Tala na branch walidhulumiwa , wewe je?
Take care
Kati ya vitu sipendi ni kudai au kuanza kuulizia mtu ile hela vip, asee inakera.. lkn ndio hamna namna, tuishi humo!
Acha kabisa mazoeaa ya pesa na mtu mweusi ambae lugha yake ya kwanza n kiswahili.
We ndo tapeli mwenyewe.
Wenye maduka na biashara ya m-pesa n shida kila kukicha wateja wanakopa.
Kumbe wahanga ni wengi
hongera mleta mada nimejifunza kitu
Mm kuna rafik yangu alinikopa 5,000/=mpaka leo anitafuti tena.
โ€œUsitoe kile ambacho haupo tayari kukipotezaโ€
Nikopeshe..najua wewe siyo mchoyo,
Rafiki yangu nilimkopesha pesa mwaka jana, siku zimeenda kafilisika kibiashara na sioni dalili ya. Kupata hiyo pesa yangu, roho yaniuma sana
Mtuvumilie ndugu, muendelee kutukopesha Mwenyezi Mungu atawajazia mnapotoa.
Siku hizi nakopesha wanawake tu maana huwa hawana longo longo
Njoo tukope hapa

Yna2
Mmmh.. wee mkopaji sana... na hurejeshi kitu!!
Fanya hivyo mkuu maana hapa mimi kuna watu wananidai ila nawazungusha kishenzi. Siyo makusudi lakini.
Kukopa kwa mtu? Sijawahi ila nataka kujaribu

Nishawahi kukopa branch na salary advance
Pole sana mkuu. Kaka yangu mmoja alinieleza "siku ukimkopesha rafiki yako, ni mwanzo wa urafiki kufa" Sikumuelewa mpaka siku yaliponikuta ya kunikuta. Unamkopesha mtu na hana hata aibu ya kusema alipe deni.
Branch walikuacha salama?
Yes
Nakopa nalipa, ila ukichelewesha wana zile msg zao ni noma
Nawaona wadaiwa sugu wanavyopita kimya kimya
lipeni hela za watu nyau ninyi

BARUA KUTOKA UWABATA

Habari,

Umoja wa wanaume bahili Tanzania
[UWABATA] unawataka wanachama wake waache kukupesha haraka iwezekanavyo na atakae kaidi atachukuliwa hatua kali.

MAKAO MAKUU,​

UWABATA,
CHATTLE.
Nahitaji nipate laki na 50 ,ili niache kukopa kopa Ela zenu, nichangieni Basi kwa hiari , na sio lazima, PM, Mana nipo kwenye Great depression x 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kuna watu wana moyo jamani.. kuna siku nilikua napiga stori na jamaa yangu analalamika eti kamkopesha mtu milioni 6! Jamaa anadai alikopa 15m sasa wakati anawaza cha kufanya ndio mshkaji akamuwahi kumlilia shida eti jamaa nae akaingia line. Nilimcheka sana.. Mimi ata 50,000 sijakukopesha bado.
 
Ndio maana mi sijionyeshagi..nikiwa nazo au nisipokua nazo huwez jua yan..tena zaid zaid nikiw nazo fasta nawapigia cm kuomba waniazimishe pesa woote wanaopendaga kukopa kopa..hiyo ndio defensive mechanism mana nawa alert kuwa sina kitu so wanani tenga mbali (kama ilivyo kawaida ya wabongo, mkono mtupu haulamwi)..nabaki stress free...

Wakiniona natumbua, nawambia hiz hela za mkopo ..na we si nilikupigia unikope??
 
 
ndo dawa yao hao,Yan mtu anakukopa baada ya hapo yeye anasahau kabisa kua ana deni la watu wewe kazi yako ni kumkumbushia tuu
 
Dah sisi ambao hatuna familia(Kuoa) watu wanaamini hatuna matumizi kabisa na pesa.......katika hali ya kawaida ni ngumu sana kumnyima mtu pesa hasa pale anapoweka shida zake wazi kwako
 
Rafiki yangu nilimkopesha pesa mwaka jana, siku zimeenda kafilisika kibiashara na sioni dalili ya. Kupata hiyo pesa yangu, roho yaniuma sana
Hahahaha mkiwa marafiki epuken sana kukopeshana

Bora umpe kama msaada lkn sio kukopeshana

Nasema ivi mtagombana, urafiki uishe


Mwanangu mmoja, siku ya Ijumaa, usikua wa saa sita, mwezi wa 1 mwaka jana , ananipigia simu..Oya Oyaaa Blood, naabika kaka, Nitumie Laki na ishirin ,jumatatu nakupa.


Nikamuuliza vipi?? Kuna usalama?? ..ananijibu yupo na Madem wanakunywa pombe

Yeye jamaa ni mnywaji wa pombe sanaaa yaan sanaaaaaa.



Basi nikamtumia 125 .


Mpaka Leo ,nawambia ivi mpaka leo hakuwahi nirudishia, urafiki ukapoteza mwelekeo.


Juzi ananitumia meseji...Kaka kaka ninaomba msaada wa elfu thelathin nimekwama hapa nilipo sijala.


Nikamwambia, Mwenyewe toka jana usiku Sijala kitu.


Akaisha kunijibu....Daaahh kudadeki ,siku ya kufa nyani


Namm nikamjibu..ndo ivo anakufa tu siku yake.

NB.. Toka ile 125 ,akawa anashindwa hata kujuliana hali, Leo hii amekamatwa ndo ananitafuta???
 
Bongo u-Kasuku mwingi sana haswa unapoanza kuzungumzia karatasi. Hapo lazima mtu aumie. Wachache sana wanaweza kuaminika - most of them manipulate you only to disappoint you. Hela yako bora ule Chipsi kavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ