Usimamizi wa mirathi

Mkuu kama kuna kiwanja tu, hapo mna eza kubaliana kwa maandishi kuwa mmiliki ni Huyu na huyu.

Maana Kuna mirathi ya kisheria na Ile ya zamani..

Kama Kuna pension, nyumba, mna fata utaratibu tu
Ni kweli mzee haukuacha vitu vingi sana ni just mashamba na nyumba

Tunahitaji kutambulika kisheria kwakuwa tunataka kuwa na mfuko(bank) ya familia kwa ajili ya kuhifadhi rasilimali pesa za familia sasa kule hawatoi account mpaka msajiliwe na kusajiliwa ni mpaka muwe na msimamizi wa mirathi

NB: hatutaki kuuza wala kugawana tunataka kutambulika kisheria ili tuweze na kukopa fedha bank n.k
 
Nenda mahakamani ya mwanzo , ukifika pale wapo wale waheshimiwa yaani wapo tu, mwombe mmoja pembeni uongee naye akushauri, hope utamwachia ya ku brash viatu
Ahsante mkuu nitafuata ushauri wako japo nipo mbali na halmashauri husika
 
Mkuu, mzigo huu hapa
Mkuu samahani hivi kama mnaomba usimamizi wa mirathi kwa ajili ya kuuendeleza kuna haja ya kuwa na KATIBA ya wanafamilia?
 
Usimamizi wa mirathi kwa ajili ya kuuendeleza ndio ipoje mkuu? Fafanua
 
Means hatugawani wala kuuza
Hakuna mirathi ya hivyo. Ni sharti na lazima, Msimamizi kufunga mirathi ndani ya muda kwa kugawa mali kwa warithi. Hakuna usimamizi wa kila siku..mwisho wa usimamizi ni miaka 2-3, sasa unaendeleaje kusimamia mali isiyogawanywa wakati muda wako wa usimamizi umeisha??

Hizo mnazotaka kukaa nazo bila kugawa ndio mirathi zinazoleta shida mbeleni. Kama mali ina faida na ikiuzwa mnaona itapotea, gawaneni asilimia na muiendeshe kama partners (wabia).
 
Hapa labda uelewa wangu mdogo ila nahisi sio kila mirathi lazima igawanywe au iuzwe wakati wanandugu tunaelewana na tuna skills za kuikuza na kuiendeleza

Huko kugombana hata wanandoa wanagombanaga tu na maisha yanasonga
 
Unaenda mahakamani na ivyo viambata Kisha utapewa fomu mbili moja ya kuomba kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi na nyingine ya wadhamini utazijaza, iyo ya kuomba kuteuliwa kuwa msimamizi utairudisha ikiwa imeambatanishwa na passport size za wanufaika, nikiimaanisha watoto wa marehemu, mume/mke. Kisha taratibu nyingine utapewa uko uko
Ila uwe umesha settle disputes na ndugu zako kama zilikuwepo kama hukufanya hivyo jiandae kuwekewa mapingamizi na ukoukosa huo usimamizi wa mirathi.
 
Hakuna mirathi ya hivyo. Ni sharti na lazima, Msimamizi kufunga mirathi ndani ya muda kwa kugawa mali kwa warithi. Hakuna usimamizi wa kila siku..mwisho wa usimamizi ni miaka 2-3, sasa unaendeleaje kusimamia mali isiyogawanywa wakati muda wako wa usimamizi umeisha??

Hizo mnazotaka kukaa nazo bila kugawa ndio mirathi zinazoleta shida mbeleni. Kama mali ina faida na ikiuzwa mnaona itapotea, gawaneni asilimia na muiendeshe kama partners (wabia).
Kwamba ni lazima kugawana hapo mkuu sijaelewa kwanini tugawane wakati tuna miongozo ya kuiendeleza na uongozi ndani ya familia upo

Mfano tuliachiwa nyumba zikiwa hazijaisha vizuri tukazimalizia asaivi zinajiendesha

Tunataka tusajiliwe kama kikundi ili tupate mfuko wa kuhifadhi pesa wa familia(banks) lakini pia tuweze kukopesheka na banks
 
Hapa labda uelewa wangu mdogo ila nahisi sio kila mirathi lazima igawanywe au iuzwe wakati wanandugu tunaelewana na tuna skills za kuikuza na kuiendeleza

Huko kugombana hata wanandoa wanagombanaga tu na maisha yanasonga
Ni uelewa mdogo ulionao mkuu. Maana ya mirathi ni kurithi mali za marehemu. Sijui kama inawezekana kurithi kitu ambacho bado kinaendelea kuwa cha marehemu.

Mirathi nyingi zipo za hivyo, watu hawafungi, na wala hawaigawanyi mali. Ni makosa, na mahakimu walipaswa kuzikataa fomu za hesabu za mali zinazokuja kwa namna hiyo.
Sasa Jaji Mkuu wa Tanzania, kwa Dar alitoa maelekezo kuwa mtu anapofungua mirathi pale Temeke One Stop Centre aache cheti halisi cha kifo kwenye jalada la mahakama na atakipata pale atakapofunga mirathi. Na sio hivyo tu, bali kila mwezi msimamizi afike mahakamani kueleza amefika hatua gani katika usimamizi wake.

Kiuhalisia, ukiona watu hawagawi mali na wanataka ibaki kama ilibyo ujue hapo ama kuna watoto wa mama mbalimbali na wengine wanaogopa mali ikiuzwa wao hawataweza kupata kitega uchumi kingine ama watu wanataka tu kukomoana.
 
Mfano tuliachiwa nyumba zikiwa hazijaisha vizuri tukazimalizia asaivi zinajiendesha
Ndio mirathi sumbufu hizo. Mkifa nyie watoto wa marehemu, wajukuu wanakuja wanaanza kusumbua, na uzingatie hamfi wote siku moja.

Sasa mfano huohuo, nyumba hazijaisha. Mmezimalizia kwa fedha ipi?? Mmetoa mifukoni mwenu au fedha ya marehemu?

Kulikua na ulazima gani sasa wa kufungua mirathi wakati mngeweza kuendelea tu na maisha kama mlivyoachwa na marehemu??
 
Mkuu mali alizoacha marehem nyingine ni asset kama vile fremu na maduka na yote yanafanya kazi, nyumba ya kupangisha na ina wapangaji kwaiyo huwa zinajiendesha zenyew

Hatugombani bali tunataka msimamizi wa mirathi atambuliwe ili tupate usajili kamili kutuwezesha kupata mikopo lakini pia kutunza pesa katika bank ya kikundi au familia

Lakini pia nina swali la nyongeza, hivi bakharesa ni ukoo au ni mtu mmoja? Mm binafsi nahisi succession ya miradi inawezekana bila kuwa na akili za kugawana na kila mtu kuanza upya wakati mzee alipambana kufika pale alipofika
 
Ni uelewa mdogo ulionao mkuu. Maana ya mirathi ni kurithi mali za marehemu. Sijui kama inawezekana kurithi kitu ambacho bado kinaendelea kuwa cha marehemu.

Mirathi nyingi zipo za hivyo, watu hawafungi, na wala hawaigawanyi mali. Ni makosa, na mahakimu walipaswa kuzikataa fomu za hesabu za mali zinazokuja kwa namna hiyo.
Sasa Jaji Mkuu wa Tanzania, kwa Dar alitoa maelekezo kuwa mtu anapofungua mirathi pale Temeke One Stop Centre aache cheti halisi cha kifo kwenye jalada la mahakama na atakipata pale atakapofunga mirathi. Na sio hivyo tu, bali kila mwezi msimamizi afike mahakamani kueleza amefika hatua gani katika usimamizi wake.

Kiuhalisia, ukiona watu hawagawi mali na wanataka ibaki kama ilibyo ujue hapo ama kuna watoto wa mama mbalimbali na wengine wanaogopa mali ikiuzwa wao hawataweza kupata kitega uchumi kingine ama watu wanataka tu kukomoana.
Tupo mtu tano wote wa mama mmoja na wote tunajiweza kila mtu na mambo yake ndio maana tumeweza kuendeleza japo kwa uchache tunahitaji tu kutambuliwa ili kufikia malengo
 
Mkuu mali alizoacha marehem nyingine ni asset kama vile fremu na maduka na yote yanafanya kazi, nyumba ya kupangisha na ina wapangaji kwaiyo huwa zinajiendesha zenyew

Hatugombani bali tunataka msimamizi wa mirathi atambuliwe ili tupate usajili kamili kutuwezesha kupata mikopo lakini pia kutunza pesa katika bank ya kikundi au familia

Lakini pia nina swali la nyongeza, hivi bakharesa ni ukoo au ni mtu mmoja? Mm binafsi nahisi succession ya miradi inawezekana bila kuwa na akili za kugawana na kila mtu kuanza upya wakati mzee alipambana kufika pale alipofika
Bakhresa ni kampuni. Pale watu watagawana hisa sio mali za kushikika. Au huenda tayari hata watoto wana hisa kwenye kampuni.
 
Nimekuelewa mkuu ntafuata ushauri wako patakapobidi. Mungu akubariki
 
Habari wanajamii, natumai mko njema.

Naomba kujuzwa hatua za kufuata ili kufungua file la usimamizi wa mirathi. Kwa maana vitu gani vinahitajika ili kuweza kuwa msimamizi na wapi anatakiwa kwenda alieteuliwa kuwa msimamizi ili kutambulika kisheria.

Natanguliza shukrani
Taratibu za Mirathi kwa ujumla zina anza na KIKAO CHA UKOO

Kikao cha ukoo kinahusisha mke/mume wa marehemu, watoto, wazazi wa marehemu na ndugu wa karibu wa marehemu na watu wengine muhimu wanye kujua kuhusu maremu nk

Ili kikao kiwe rasmi kitakua na mwenyekiti na katibu ambaye atahakikisha maamuzi ya kikao yanaandikwa kwenye MUKTASARI WA KIKAO CHA UKOO na wajumbe wote wa kikao watasaini kukubali maamuzi ya kikao

Mambo MUHIMU kimahakama yanayotakiwa kuwepo kwenye Muktasari wa Kikao cha Ukoo ni

FAMILIA YA MAREHEMU
kikao kitawatambua mke/mume na watoto wote wa marehemu.. hawa ndio beneficiaries

MALI ZA MAREHEMU
kikao kitazitambua na kuziorozesha mali zote za marehemu

MSIMAMIZI WA MIRATHI
Kikao kita mteua msimamizi wa mirathi ya marehemu

Baada ya hapo aliyeteuliwa kuwa maimamizi wa Mirathi atakwenda mahakani sasa kufungua shauri la mirathi ili sasa mahakama imteue rasmi kuwa msimamizi(Taratibu zaidi atapewa mahakamani, ila ni lazima awe na muktasari wa ukoo na cheti cha kifo)

Ikumbukwe kwamba kikao cha ukoo kina mpendekeza msimamizi kisha mahakama ina INAMTEUA RASMI kuwa msimamizi ikiwa hakuna pingamizi

Baada ya mahakama kusikiliza shauri na kumteua rasmi msimamizi atarudi kwa familia ya marehemu kusikiliza matakwa yao
Je wanataka kugawana?
Je hawagawani ila usimamizi utakuaje nk nk
Mchakato utakao kubaliwa na familia ya marehemu ndio msimamizi ATAUSIMAMI

So
Kuna mchakato wa kutuliwamsimamizi
Na kuna mchakato wa nini kifuate
 
Back
Top Bottom