😅😅hapo sawa kila la kheriNitakua tayar ni mzee na nimechoka kuishi kwa amani.
Aiseeee sawaUsiku ni alama ya utambuzi kati ya mtu anayeishi katika Comfort zone na yule aliye katikati ya vita ya kubadili sura ya maisha yake na majina ambayo alishaitwa na mengine yakisubiri wakati yaje zamuni.
Safiii kaka piga kaziSababu moja wapo ni hiyo, sasa ni saa saba na robo ndio nagusa godoro tokea ile saa 11, masaa manne yajayo niwe nimeamka tena!
Mazoea yanakua na sababuWengine ni mazoea yashakua...
Heh madhabahu gan binti😅😅Ndio nashuka madhabahuni sasa!
So wewe upo jeshini😅Jeshini wana kauli wanasema "ukilala unalaliwa"
Tunakesha usiku kwa sababu ya mwingiliano wa majukumu ya kimaisha, changamoto za kisaikolojia, na mabadiliko ya teknolojia yanayovuruga mfumo wa asili wa miili yetu.Kwa nini huwa unachelewa kulala?
Kawaida siku inapoanza kwa kuchomoza kwa jua, watu wengi huanza pilika za kutafuta riziki na kutimiza majukumu yao ya kila siku
Wengine huenda kazini, vibaruani, mashambani, sokoni, huku watoto nao wakielekea shuleni
Kwa kifupi, siku huwa imejaa shughuli nyingi zinazochosha mwili na akili
Usiku kwa kawaida huchukuliwa kama muda wa kupumzika na kurejesha nguvu baada ya uchovu wa mchana, isipokuwa kwa wale wanaofanya kazi za usiku
Hata hivyo, pamoja na uchovu wa kutwa nzima, kuna watu wengi ambao hupata shida ya kulala
Mwili unaweza kuwa umechoka, lakini usingizi usije😢
Moja ya sababu kubwa ni msongo wa mawazo
Hofu kuhusu kesho, changamoto za kiuchumi, madeni, kutokuwa na uhakika wa maisha ya baadaye, matatizo ya kifamilia au kimapenzi vinaweza kuifanya akili ishindwe kutulia
Wengine hukosa usingizi kwa sababu ya maumivu ya ugonjwa au changamoto nyingine za kiafya
Pia kuna suala la matumizi ya simu na mitandao ya kijamii
Watu wengi hujikuta wakitumiq simu kwa saa nyingi usiku bila kutambua kuwa muda wa kulala umeshapita
Wataalamu wanashauri mtu mzima apate angalau saa 7 hadi 8 za usingizi kwa siku, lakini kwa baadhi ya watu hilo limekuwa jambo gumu sqna
Mimi binafsi niliwahi kupitia kipindi cha kukosa usingizi kiasi kwamba nilikesha usiku mzima bila hata kusinzia
Hadi leo sijawahi kurudi kuwa na usingizi mzuri kama nilivyokuwa nao zamani,
Nilikua nalala kiasi naweza kunyanyuliwa na kutolewa njee nisijue saivi mtu akitema mate nasikia 😅
hata nikiacha kutumia simu na kuzima mwanga bado usingizi hauji kwa urahisi
Je, wewe mdau, ni nini hasa hukufanya uchelewe kulala?
Ni mawazo mengi, changamoto za maisha, matumizi ya simu, au kuna sababu nyingine?
Unalala usiku wa manane, alfajiri, au mapema kama inavyoshauriwa? 🤔
ShesRise_1 😴😴
SahihiTunakesha usiku kwa sababu ya mwingiliano wa majukumu ya kimaisha, changamoto za kisaikolojia, na mabadiliko ya teknolojia yanayovuruga mfumo wa asili wa miili yetu.
Ingawa usiku uliumbwa kibaolojia kwa ajili ya kulala na kuufanya mwili ujijenge upya, mwanadamu wa sasa anakabiliwa na mambo mengi yanayomfanya aendelee kuwa macho.
Safii piga kaziNipo namalizia kazi fulani ya watu then nilale
Nikichoka nitakutumia uikamilishe 🤗Safii piga kazi
Mie tena tuseme AmenNikichoka nitakutumia uikamilishe 🤗
🙏🙏Mie tena tuseme Amen
Itajua mwenyewe sisi kwetu furaha teleInasikitisha sana
Ahaaa kumbe sawa mkuu asanteHayo ni maisha ya kukariri tu. Ni sawa na tulishakariri kuwa lazma mtu anywe chai au uji asubuhi. Kulala sio lazima ulale ucku ndugu yangu na ndio maana watu wanakosa ucngizi ucku coz mda mwili ulihitaji ulale ulikuwa unapambana na matv au tusema kazi. Na ndio maana watu sasa hivi bp ni nje nje, sukari ni ya kufikia.
Mfano umetoka kazini saa12 upo nyumbani unaweza ukaoga ukala hadi saa 4 uamke ule ukae hadi saa sita ulale tena hadi saa11 uamke ujiandae kwenda kazi na sio kuzoeasha mwili ati by saa nne tano upo kitandani na mchana mwili ulikuhitaji uupumzishe ukaenda kula makonyag na washkaji.
Unaweza kuishi maisha ya kiafya ukitaka mfano asubuh badala ya chai kula matunda kama mgonjwa, mchana kula heavy meal afu jion kunywa chai ulale na utalala tena vizuri sana tena usingizi mzito. Ikifka sa kumi na moja ile umeamka kunywa uji uende kutafta riziki na kuhusu kulala ukiamua unaweza usilale had pale mwili utahitaji kulala wenyewe.