Usikimbilie ndoa

Usikimbilie ndoa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,708
Reaction score
35,719
Habarini za asubuhi mabibi na mabwana na wanafunzi na watoto bila kusahau viben10,

Usikimbilie ndoa ukajua Yale matabasamu wanayoonyesha watu kwenye picha wanazopost Facebook ukajua hata ndani kupo hivyo hivyo...!!!

ndoa nyingi ndani zimeoza!!!
caption na post za Facebook na insta zisikupe hamu ya kukurupukia ndoa eti na wewe uje utupostie my dear utakutana na fuso wakati wewe ni kivitz..

unapoamua kuingia kwenye ndoa jiulize Haya maswali!!!

Je, utaweza kuziishi ndoto za mtu mwingine?

Je, uko tayari kuumia kwa ajiri ya mumeo?

Je, upo tayari muda mwingine kuziua ndoto zako na kuamua kuzipigania ndoto za mwingine?

Nikuambie tu si kila mwanaume anafaa kuwa mume wengine wanahitaji hata miaka sita mbele ili kuwa na akili za kuweza kuendesha ndoa.

Mtu anaweza kuwa na miaka 30 lakini akili yake ya kuendesha ndoa hana tofauti na mtoto wa miaka 16 hawa jifunze kuwaacha wakue!!!

Umri sio kigezo cha wewe kuwa tayari kuoa au kuolewa ndoa ni gunia la misumari linahitaji watu strong kulibeba!!

Mtu anayeweza kuchukulia madhaifu ya mwenzie kama changamoto na kuamua kuyafanyia kazi, sio kakosea kidogo tu nenda kwenu!! sijui sikutaki!! Ukiona hivyo ujue ulioa au kuolewa na mtu ambaye bado aliihitaji kuendelea kukua peke yake ili ajifunze kuipigania ndoa!!!

Wengi tunaona ndoa chungu sababu mtu anaamua kuingia kwenye ndoa na sababu zake kibao.

mwingine anashida zake anahisi akiolewa zitaisha..

mwingine sababu tu mtu wake anakazi..

mwingine hofu ya umri..

mwingine kachoka tu kakaa mwenyewe..

mwingine anataka tu apate picha za kupost eti naye kaolewa..

mwingine anataka kuwakomoa aliosema hataolewa!!!!

my dear ukianza kuitafuta ndoa kwa sababu kama hizo jua kabla mechi haijaanza ushapigwa 4-0 tukutane baada ya dakika 90.

Mi mwenyewe bado kidogo kuoa namalizia ujana[emoji6][emoji6]

Ila nkipata karembo najilipua[emoji38][emoji38]
Nawasilisha!!
 
Ndoa sio kitu cha kukurupukia,kuna ukweli mkubwa kuhusu wengi wanaokimbilia kuolewa kwa hizo sababu ulizotaja,na mioyoni mwao wengi wanakuwa bado hawajamaliza maisha yao ya kuishi peke yao,yaani inakuwa kama amekatiza sasa akiingia kwenye ndoa anajikuta anamalizia kile kiporo cha aliyobakiza,sasa hapa ndio penye balaa...
 
Kuna watu wanataka ndoa ila hawataki kuacha maisha ua usingo

Ndoa inakua ngumu balaa maana anataka starehe na michepuko na kurudi home muda atakao yeye
Ndoa sio kitu cha kukurupukia,kuna ukweli mkubwa kuhusu wengi wanaokimbilia kuolewa kwa hizo sababu ulizotaja,na mioyoni mwao wengi wanakuwa bado hawajamaliza maisha yao ya kuishi peke yao,yaani inakuwa kama amekatiza sasa akiingia kwenye ndoa anajikuta anamalizia kile kiporo cha aliyobakiza,sasa hapa ndio penye balaa...
 
Well said...ila hiki kizazi sijui kama kitaelewa
tatizo kuna kitu kinaitwa 'kupenda'

mtu anawezekana akawa akili yake bado inahitaji kukua na haiwezi ndoa, na ni mzigo mkubwa ukiwa nae kwenye ndoa, ama itabidi ujisacrifice way too much for them kwenye ndoa, ila ndio ushapenda sasa.

mnaodhani wamekosea kuoa ama kuolewa na fulani mara nyingine msishushe uwezo wao wa kung'amua mambo

huenda wanaelewa wenzi wao ni mabomu ila ndio vile washapenda na kuacha hawawezi wakaamua kujilipua na kuniingiza kwenye ndoa mradi wawe nao
 
Habarini za asubuhi mabibi na mabwana na wanafunzi na watoto bila kusahau viben10,

Usikimbilie ndoa ukajua Yale matabasamu wanayoonyesha watu kwenye picha wanazopost Facebook ukajua hata ndani kupo hivyo hivyo...!!!

ndoa nyingi ndani zimeoza!!!
caption na post za Facebook na insta zisikupe hamu ya kukurupukia ndoa eti na wewe uje utupostie my dear utakutana na fuso wakati wewe ni kivitz..

unapoamua kuingia kwenye ndoa jiulize Haya maswali!!!

Je, utaweza kuziishi ndoto za mtu mwingine?

Je, uko tayari kuumia kwa ajiri ya mumeo?

Je, upo tayari muda mwingine kuziua ndoto zako na kuamua kuzipigania ndoto za mwingine?

Nikuambie tu si kila mwanaume anafaa kuwa mume wengine wanahitaji hata miaka sita mbele ili kuwa na akili za kuweza kuendesha ndoa.

Mtu anaweza kuwa na miaka 30 lakini akili yake ya kuendesha ndoa hana tofauti na mtoto wa miaka 16 hawa jifunze kuwaacha wakue!!!

Umri sio kigezo cha wewe kuwa tayari kuoa au kuolewa ndoa ni gunia la misumari linahitaji watu strong kulibeba!!

Mtu anayeweza kuchukulia madhaifu ya mwenzie kama changamoto na kuamua kuyafanyia kazi, sio kakosea kidogo tu nenda kwenu!! sijui sikutaki!! Ukiona hivyo ujue ulioa au kuolewa na mtu ambaye bado aliihitaji kuendelea kukua peke yake ili ajifunze kuipigania ndoa!!!

Wengi tunaona ndoa chungu sababu mtu anaamua kuingia kwenye ndoa na sababu zake kibao.

mwingine anashida zake anahisi akiolewa zitaisha..

mwingine sababu tu mtu wake anakazi..

mwingine hofu ya umri..

mwingine kachoka tu kakaa mwenyewe..

mwingine anataka tu apate picha za kupost eti naye kaolewa..

mwingine anataka kuwakomoa aliosema hataolewa!!!!

my dear ukianza kuitafuta ndoa kwa sababu kama hizo jua kabla mechi haijaanza ushapigwa 4-0 tukutane baada ya dakika 90.

Mi mwenyewe bado kidogo kuoa namalizia ujana[emoji6][emoji6]

Ila nkipata karembo najilipua[emoji38][emoji38]
Nawasilisha!!
Tatizo umri.....aaaaaargh it's just a number.......hahaaaaa
 
Back
Top Bottom