Usijisifu kumfanyia mtu ubaya mbele za watu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
18,990
42,483
Kama umepanga kulipiza kisasi kwa adui yako basi panga kimya kimya; kisasi hiko usije kuanza kuropoka maneno mabaya mbele za watu. Kuna Matukio mawili nayakumbuka.

La kwanza tulikuwa tunakunywa sehemu sasa watu wawili maadui wakaanza kuzinguana mmoja anaanza kumwambia mwenzake nitakuua wewe maneno kibao jamaa aliambiwa kesho atauwawa kweli kesho akaja anatapika damu ikaanza kusemekana aliwekewa sumu si unajua mapombe yenyewe visungura hivi tuna share peg. Ni bahati tu Alipona hakufa.

Tukio lingine bodaboda wawili wametoleana maneno machafu mmoja kamtishia mwenzake kesho hatafika kijiweni huwezi amini kesho yake yule dogo alikutwa ametobolewa macho Pikipiki wameichukua Majambazi na jamaa akafuatwa kuambiwa huenda atafuatwa na polisi ilibidi akimbie yaani hata kama huusiki na tukio maneno yako yanaweza kukuletea shida.
 
ULIMI ni kiungo laini sana kwenye miili yetu, kiungo chenye kazi nyingi mno mdomoni, iwe kula, kutafuna au kuhifadhi maji kwa muda mdomoni.

Lakini ULIMI hutumika pia kuonja vyakula au vinywaji hususani kitu ambacho mtu hujawahi kutia mdomoni.hapa niseme tu kuwa ULIMI una hila sana .

ULIMI ni kiungo kinachotumika kuchezesha maneno. ule mchezo wa maneno waweza kukupa mafanikio maana,

Kuna watu wana pesa na ukwasi wa kutosha kutokana na ujuzi wa kuchezesha maneno.

Kuna watu wana umaarufu wa hali ya juu kutokana na namna nzuri ya kuchezesha maneno, kama kuimba, kuigiza sauti za watu wengine n.k

Lakini pia wapo wanaofaidi mapenzi kutoka kwa warembo mbalimbali kutokana na kuchezesha maneno, mwanamke akija kushituka, mtu kashaliwa.

Lakini huu ULIMI ukiutumia kinyume chake, kama Utapeli, Uchonganishi, vitisho n.k,hakika utaangukia pabaya.
Chunga ULIMI wako.

ULIMI una hila sana, ULIMI huwashwa ikiwa hakuna connection nzuri Kati ya ubongo na ULIMI basi mtu hujikuta anaongea vitu hata vya Siri au visivyotakiwa na hapo ndipo huja maneno kama ubwatukaji na uropokaji.

ULIMI na MOYO ni vitu vinafanana ni viungo vidogo lakini vyenye kasoro kubwa ikiwa ubongo hautofanya kazi yake.

Sifa ya ULIMI ni kiherehere yaani umekuta watu wanabishana kuhusu siasa, mpira, na vingine vingi basi ULIMI hutamani uchangie Mada, yaani haya kipofu akisikia maneno atatamani achangie neno.

Sifa ya MOYO je?
Ni tamaa, macho yasione kitu moyo tayari ushatamani, na kama hutumii ubongo basi, huja sifa kama wizi, ubakaji, ulawiti na vitendo vingi vya kihalifu. MOYO una tamaa sana.

Fikiri kabla ya kunena,
Chunga ULIMI wako.

Fikiri kabla ya kutenda,
Linda sana MOYO wako.
 
Nakumbuka ni muda kidogo umepita nilikamatwa na trafk barabarani kwa kosa la kuendesha bila reseni,katika mzozo wa hapa na pale trafk akaniorodheshea nakosa mengine kama ma 3 hivi,nikakataa kulipa......
Wakati tunabishana akaongezeka mwingine wa kiume huyu alifika na kunivua kofia,Ile kofia(ballet) huwa inavyaliwa halafu inavutwa upande...ule upande unaovutwa huwa unatengeneza tumbo ndani ya kofia,lile tumbo hutumika kuweka bangi,sigara,unga na rizla......

Wakanipiga Pingu mojakwamoja mpaka UTUO,kesi ikawa ya bangi na sio pikipiki,nilikataa Sana kuwa zile bangi sio zangu kwamba sijui zilikotoka,nikapigwa mno,mwisho wakaja wataalamu wakanitoa siku hiohio....
Basi nilivyotoka Tu nikarudi pale kwa Yule trafki aliyenikamata,nikampiga mkwara mno mixa kumwambia tutakutana mtaani....
Baada ya siku mbili trafki aliibiwa nyumbani kwake akaibiwa na nguo zote za ndani,nilitafutwa nikakimbia maskani miezi 2..
 
Asante sana kwa kumbusho hili ndugu.

Binafsi nimejifunza the hard way kupitia hili somo hapa. Na bado ninaendelea kujifunza, neno la Mungu linasema linda sana moyo wako kuliko yote uyalindayo. If it was editable ningeongeza kusema chunga sana kinywa chako kuliko vyote uchungavyo.

#sometimeslazimayakukuteiliujifunzeakaexperienceisthebestteacher#
 
Yak‬obo ‭3:5‭-‬6‬

[5] Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

[6] Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
 
Visasi huwa nafanya Sana,

Hata January Hii Kuna fala mmoja ananisumbua Sana, nmemuonya anajifanya kichwa ngumu.

Alipaki kihasara hasara nami Nmemtia hasara kwa kumuwekea chumvi kwenye engine ya gar lake, na mpaka Sasa kalipaki TU uani anajitafuta akanunue injini mpya.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom