Usijione Mwenye Bahati Kumpata Mwanamke Yoyote. Sababu.

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Wala usikae kujisemea “nikimpata yule maisha yangu yatanyooka”.
Wala usijisemee “ivi nampataje mwanamke yule?”.
Wala “hivi namridhishaje huyu?”. au,
“ntamfanyaje asiniache?”
Hapo unamweka kama mwanamke kama “kitu fulani inabidi nijishindie”.

Unajiweka kuwa mnyenyekevu kwa mwanamke. Na kutaka kumridhisha na kukubali kuendeshwa ili tu uwe naye. Utakua umejishusha mwenyewe kwa mwanamke, bila hata dawa.

Apo unakua umemweka juu yako hata kabla hujamwambia mambo.
Na ukiingia kwenye mahusiano naye atakuendesha na kukuchagulia siku za kufanya mapenzi. Je, unataka hilo? Kuambiwa tutafanya mapenzi tarehe 3 tu?

Hata kufanya mapenzi na mwanamke yoyote kusikufanye ujione mshindi/ mwenye bahati.
Ukiingia kwenye mahusiano ivo mwanamke atakua na nguvu juu yako.

Kwanini?
Sababu yeye ndo anakua umemweka kama mtawala wako.
Unakua kama mtoto wa kiume anayetaka kumridhisha mama yake. Hivyo, atafanya juu chini asimkasirishe mama yake na hatokua mkweli.

Namaanisha.
Unakua umemweka mwanamke kama kipaumbele chako.
Mawazo yako yote yanamfikiria yeye kama muamuzi wa mambo yako.
Kidogo tu unaanza kutunga uongo wa kumwambia, au unafikiria atakuambiaje/ atakuchukuliaje au unaogopa kumkosea na mbaya zaidi unafanya kitu usichotaka ili usinyimwe mambo ya kitandani.

Ukiona umefikia hii hatua ujue umemweka mwanamke juu yako, kwa kujua au bila kujua utakua unamtukuza. Kama vile ni Mungu wako.
.
Hata kama ni mzuri kiasi gani, usijione mwenye bahati kumpata.
Bali badilisha mtazamo. Yeye pia ni mtu na kasoro/ mapungufu na udhaifu wake.
Jiwekee kuwa je, huyu ananifaa? Tangu unaanza kumtongoza.
Hivyo, jiwekee yeye ndo ajione mwenye bahati kukupata.

Kwanini?
Sababu,
Nani atamuongoza?
Nani atakayekua anamtunza?
Nani atamvumilia kwa mapungufu yake?
Nani atamsikiliza hata kwa vitu usivyotaka?
Nani atakua anamvumilia kipindi cha hedhi?
Nani atakua anamvumilia na mudi zake zisizoeleweka?
Nani atamuheshimu utu wake na kutomdharau sababu ni mwanamke? Majibu yote ni wewe.
Hata wao wanajua. Ndo mana muda mwingine wana majaribu ili kukupima.
Je, unatambua thamani yako na kumdhibiti?
Kisha, uishi naye wewe ukiwa kiongozi, bila kuvunja haki zake.
Uishi naye kwa akili. Furahi pamoja naye.
Na akivunja mipaka yako usisite kumdhibiti/ kumwadhibu.

Lakini ukimpa nafasi yote hiyo na bado ukajiona we ndo mwenye bahati kumpata ujue umejitafutia kushushwa heshima mwenyewe.

Weka akilini mwako hili, mwanamke yupo kwa ajili ya kukuridhisha na sio kukufanya ujiskie mdogo au kukuendesha.
 
DAh sina cha kusema lkn huyu unayemuongelea hapa ni mimi kabisa. Ingawa nishaanza kufanya mabadiliko ya haraka naona matunda lkn nimepigika sana kwa huu mtazamo aisee
 
Ndoa Haina ujanja, wakati wowote inakuzingua kama hukuoa / kuolewa na mtu sahihi. Omba na shukuru sana Mungu ikiwa ndoa inakuendea vizuri
 
Back
Top Bottom