Usijaribu kusoma kozi hizi, utakufa njaa

Bwana Yesu asifiwe wakuu..

Jamani nimeona ni vyema kutoa muongozo hasa kwa Form6 ambao mpo kwenye mchakato wa application za vyuo, kama kweli unapenda maisha yako na huna kaka wala Mama mbunge (Referee) nakuomba usisome kozi hizi.

Sociology, Political and Public Admnistration (PSPA), Public Admnistration (BPA), Conflict resolution, Mass communication(Mascom), International relation, Public relation, Law (LLB), Theology, Arabic language, Tax Management, Community development, Rural development planning etc.
NOTE:
Lengo langu si kukashifu mtu bali kutoa elimu.

Stay blessed.
Wewe una taaluma gani? Tuanzie hapa
 
Hata accounting haina dili siku hizi graduates kibao wako mtaani

atleast hata matangazo ya kaz yanaonekana hvyo unapata nafas za kuomba, ila hizo koz unaweza ona hata miez mitatu hakuna job advert na pia upande wa pili hzo koz ni ngumu kujiajiri.
 
Hivi wewee unadhani maisha ni kusoma engineering? Hapana kwanza nakwambia watu waliosoma public administration ,human resource ndio mabosi wenu ofisini nenda ofisi yoyote utakuta watu wa human resource na public administration ndio wanawaongoza ma engineer,madoctor,geologist,! Halafu ngoja nikwambie SASA kada ya human resource na public administration wana posho kibao wewe kaa sasa na mawazo yako mgando

mbna unachotolea maelezo ni tofauti na mada hajasema hzo koz hawalipwi vizuri, anasema ni koz ambazo nafas za kazi ni chache ukilinganisha na idad ya graduates waliopo mtaani.
 
Hapana kazi nyingi sana za kujiajiri,kuajiriwa ,Paralegals ,! Wizara ya sheria ajira kibao,law firms kila siku wanatafuta mawakili wakuungano Nao! Labda unajua mipango kama lsrp?
 
Hivi wewe unajua kwamba kada ya she ria inaupungufu makubwa sana ? Anglia Tanzania kuna upungufu mkubwa wa mahakimu ,majaji,mawakili, ? ,na wewe na sayansi zako hata uajiriwe huwezi kumfikia wakili ! ,Tanzania bar a kuna mawakili wasiozidi 7000 , ukilinganisha na nchi nyingine! , Tanzania kuna ucheleweshwaji wa hukumu kutokana na upungufu wa majaji na mahakimu,! Unaijua mipango wa LSRP ? SASA basi law ina uhitaji mkubwa sana

Kaka huna Hoja tatizo kwa Tz sio upungufu wa mahakama wala majaji tatizo ni accountability tu,kama kuwajibika hakuna hata tuwe na mahakama za kata hakuna kitu kabisa,uchache si hoja tunaangalia utendaji upo vp! Upatikanaji wa haki upo kwa kiwango gani! !hapo ndo tatizo Jaji anatoa hukumu mpaka simu itoke ikulu ndo atoe hukumu.
 
Hivi kwa nini waropokaji wa neno kujiajiri huwa ni wale walio kwenye ajira/ajiriwa? Unafiki huu huwa unanikera vibaya.
Nimemaliza Chuo(Computer Science) . Nikarudi kulima kijijini
Nimepata maharage na mahindi ya kutosha tu lakini bei sh.200 per kg(mahindi) na 750 maharage. Kusafirisha tani 2 za mahindi kutoka Songea hadi Dar kwenye soko ni vigumu, huwezi pata kitu! Wanaoweza ni wenye tani mia na kuendelea...
Mbolea, nguvukazi n.k hela niliyotumia haiwezi kurudi kwa bei ya hapa Songea.
Mnaosema tujiajiri tupeni na mbinu, vinginevyo ni unafiki tu kama unafiki mwingine, mbona nyie ni waajiriwa?
 
Bwana Yesu asifiwe wakuu..

Jamani nimeona ni vyema kutoa muongozo hasa kwa Form6 ambao mpo kwenye mchakato wa application za vyuo, kama kweli unapenda maisha yako na huna kaka wala Mama mbunge (Referee) nakuomba usisome kozi hizi.

Sociology, Political and Public Admnistration (PSPA), Public Admnistration (BPA), Conflict resolution, Mass communication(Mascom), International relation, Public relation, Law (LLB), Theology, Arabic language, Tax Management, Community development, Rural development planning etc.
NOTE:
Lengo langu si kukashifu mtu bali kutoa elimu.

Stay blessed.

Naomba nisaidie hapo kwenye nyekundu, inawezekanaje mtu aliyesoma hizo akakosa kazi ilhali fursa za kujiajiri kwenye hizo fani ni lukuki?

Hivi kwa nini waropokaji wa neno kujiajiri huwa ni wale walio kwenye ajira/ajiriwa? Unafiki huu huwa unanikera vibaya.
Nimemaliza Chuo(Computer Science) . Nikarudi kulima kijijini
Nimepata maharage na mahindi ya kutosha tu lakini bei sh.200 per kg(mahindi) na 750 maharage. Kusafirisha tani 2 za mahindi kutoka Songea hadi Dar kwenye soko ni vigumu, huwezi pata kitu! Wanaoweza ni wenye tani mia na kuendelea...
Mbolea, nguvukazi n.k hela niliyotumia haiwezi kurudi kwa bei ya hapa Songea.
Mnaosema tujiajiri tupeni na mbinu, vinginevyo ni unafiki tu kama unafiki mwingine, mbona nyie ni waajiriwa?
Mkuu tena wengine unakuta wamejiajiri baada ya kupata ka mtaji kwenye kuajiriwa au mtaji toka kwa familia zao. Na kama mtu atumie elimu yake kujiajiri hivi mfamasi daktari engineer hawa wataanzaje kujiajiri. Otherwise tusitumie kile tulichokipata shule tuwe wakulima na wafugaji tu sasa.
 
Kaka huna Hoja tatizo kwa Tz sio upungufu wa mahakama wala majaji tatizo ni accountability tu,kama kuwajibika hakuna hata tuwe na mahakama za kata hakuna kitu kabisa,uchache si hoja tunaangalia utendaji upo vp! Upatikanaji wa haki upo kwa kiwango gani! !hapo ndo tatizo Jaji anatoa hukumu mpaka simu itoke ikulu ndo atoe hukumu.
Yani hata hujaelewa kinachoendelea! Unajua maana ya " mlundikano wa kesi"
 
Hivi wewee unadhani maisha ni kusoma engineering? Hapana kwanza nakwambia watu waliosoma public administration ,human resource ndio mabosi wenu ofisini nenda ofisi yoyote utakuta watu wa human resource na public administration ndio wanawaongoza ma engineer,madoctor,geologist,! Halafu ngoja nikwambie SASA kada ya human resource na public administration wana posho kibao wewe kaa sasa na mawazo yako mgando

Safi Safi mueleze huyo na fikra zake za ajira in education
 
Badhani una Lengo la kupotosha wenzanko tena saana tu , au ni seme hisia zako juu ya baadhi ya coz ulizozitaji hazina uhalisia , umetaja Course ambazo ndizo za muhimu kupita zote na zenye soko haswa.

Mfano.
Community Development pamoja na Rural Dvlopment plann, hakuna coz za muhimu kama hizo . Yaani ukimaliza tu , kama malengo yako ni kuajiriwa, basi jua tayari umefaulu .

Madogo , especially ninyi wa Kike , Coz Rahisi na ambayo haitakutesa ,na ina uhakika wa kupata Kazi ni hii " Community Development " basi .

My take: Jueni Kuchuja mambo , yasememwayo JF mengi ni hisia za watu, na mengine ni malengo ya mtu mmoja mmoja, kwa namna yeye binafsi anavyojichukulia , hivyo ushauri ni mzuri , lakini jifunzeni kuchanganua mambo na kuchukua yaliyo ya kwenu. Nadhani nyote mna ndoto na malengo , hivyo jifunzeni kuishi kwa kuendana na malengo yenu.

Bora umefunguka maana huu ni upotoshaji kweli kwa mtu mwenye roho nyepesi japa tayari angekuwa kabadilisha course ila liwe na liwalo am going for Public Administration
 
Hivi wewe unajua kwamba kada ya she ria inaupungufu makubwa sana ? Anglia Tanzania kuna upungufu mkubwa wa mahakimu ,majaji,mawakili, ? ,na wewe na sayansi zako hata uajiriwe huwezi kumfikia wakili ! ,Tanzania bar a kuna mawakili wasiozidi 7000 , ukilinganisha na nchi nyingine! , Tanzania kuna ucheleweshwaji wa hukumu kutokana na upungufu wa majaji na mahakimu,! Unaijua mipango wa LSRP ? SASA basi law ina uhitaji mkubwa sana

Kwanza mimi sijasoma sayansi A-level, Pia usibabaishwe na takwimu za serkali hebu malizia kusoma kwanza hiyo Law alafu uje utoe mrejesho na si kuongea tu kwa bla bla.
 
Inaonyesha ni kiasi gani usivyojua mambo, mtu wa Public administration na PSPA wote ni human resource kama ulikua hujui content za course hizo basi chukua hii.

Tumia akili wewe. Ndiyo ninyi mnaofananisha mchungwa na mlimao, Pia ndio nyinyi mnaodhani shangazi ni mjomba wa kike,

huwezi kumpambanisha HR na political scientist kwenye post inayohitaji Human resource manager sababu vitu anavyocover HR ni vingi mno kuliko PS anayesoma kwa sehemu tu kwenye course.
 
Hivi wewe unatoa ushauri kama nani? Umefanya utafiti? Au unaongea tu aisee ,hebu weka tafiti yako na uidefend humu jamvini

Hebu acha kujitoa ufahamu wewe hili ni jukwaa huru ambalo kila mtu ana uhuru kutoa mawazo/ ushauri na lazima ucomment kwenye thread kama hupendi kwani thread haipo moja tu JF.

Lastly, hebu niambie ni nani wewe unayemuona anastahili kutoa ushauri?,
 
Back
Top Bottom