Usijaribu kusoma kozi hizi, utakufa njaa

Usijaribu kusoma kozi hizi, utakufa njaa

Ukweli mtupu hata kama unauma. Nampongeza mleta mada kwa kutupa elimu ya bure hapa JF. Ushauri wa bure kama wewe umesoma Arts haraka sana Apply kozi za Education kuepuka msoto wa kitaa.
 
Sasa watu wa art wasome kozi gani ?,toeni sasa na elekezo na sio kukataza tu

Sent from my iPhone using JamiiForums app
Suluhisho la uhakika na la haraka kwa waliosoma masomo ya Arts kwa sasa ni kusoma course za Education vyuoni. Tofauti na hapo wajipange kula msoto mkali sana kitaa. Tuko nao wengi kitaa wanatamani warudi vyuoni wapewe boom ili wasukume maisha.
 
Nashindwa kuamini kwasababu Kaka yangu kamaliza PSPA mwaka 2012 pale mlimani na anapata kazi rasmi mwezi wa 8/2012, na mwaka jana 2013 may akapata kazi nyingine na maisha yako sawasawa. Dada yangu alimaliza Law akapiga school of law now ni mtu tofauti.
NB: Chagua course unayoipenda utafurahia maisha ya chuo na utajua namna ya kufungua nafasi za ajira na kujiajiri.
 
Bwana Yesu asifiwe wakuu..

Jamani nimeona ni vyema kutoa muongozo hasa kwa Form6 ambao mpo kwenye mchakato wa application za vyuo, kama kweli unapenda maisha yako na huna kaka wala Mama mbunge (Referee) nakuomba usisome kozi hizi.

Sociology, Political and Public Admnistration (PSPA), Public Admnistration (BPA), Conflict resolution, Mass communication(Mascom), International relation, Public relation, Law (LLB), Theology, Arabic language, Tax Management, Community development, Rural development planning etc.
NOTE:
Lengo langu si kukashifu mtu bali kutoa elimu.

Stay blessed.

Seneta01 njoo huku.
 
Sasa kwa mjibu wako ni kozi zipi zinatakiwa zisomwe ili watu wasife njaa
 
tangu la saba mtu anakimbia hesabu atasoma nini kama sio sociology? ila kwa wanaosoma hizo kitu inabidi kuhakikisha G.P.A si chini ya 4.0 hapa nafuu
 
Sasa watu wa art wasome kozi gani ?,toeni sasa na elekezo na sio kukataza tu

Sent from my iPhone using JamiiForums app

Atleast mtu wa Arts asome, Logistic and transportation management, Education, Law enforcement, Procurement and logistic management,

Hapo itamsaidia atleast kwenye soko la ajira.
 
mkuu hii course uzuri wake ni nini?

Hiyo kozi ni nzuri sana pia ni miaka michache imepita tangu waanze kutoa degree zake pale NIT, pia mkopo ni 100% na ni priority course kiongozi. Hope so hata kwenye soko la ajira haina ushindani sana.
 
Nashindwa kuamini kwasababu Kaka yangu kamaliza PSPA mwaka 2012 pale mlimani na anapata kazi rasmi mwezi wa 8/2012, na mwaka jana 2013 may akapata kazi nyingine na maisha yako sawasawa. Dada yangu alimaliza Law akapiga school of law now ni mtu tofauti.
NB: Chagua course unayoipenda utafurahia maisha ya chuo na utajua namna ya kufungua nafasi za ajira na kujiajiri.

Basi huenda kaka yako ana referee au ni bahati yake tu, Anfanya kazi gani now isije kuwa anatembeza vyombo na arovera za Forever living na PSPA yake.
 
hapo masscom ni shida sista mmoja alipiga hiyo kozi duu alichakaa mtaani hadi akili ya kwenda jeshi ilivyokuja saiv anapiga mpunga mrefu hatar
 
Nashindwa kuamini kwasababu Kaka yangu kamaliza PSPA mwaka 2012 pale mlimani na anapata kazi rasmi mwezi wa 8/2012, na mwaka jana 2013 may akapata kazi nyingine na maisha yako sawasawa. Dada yangu alimaliza Law akapiga school of law now ni mtu tofauti.
NB: Chagua course unayoipenda utafurahia maisha ya chuo na utajua namna ya kufungua nafasi za ajira na kujiajiri.

Kaka yako,Dada yako eeeh mnelekea kwenu wote ni wasomi,wewe je umesomea nn?....maana naona kuna using hapa katikati
 
Si kweli.

Ni tatizo la utawala wetu...chanzo kikuu ni udhaifu wa serikali ya JK.

Mfumo wa utawala- kigezo cha kupata kazi si elimu au kozi bali ni tabaka la wafanyakazi/watawala??

Ikiwa una mtu wa kukuunganisha basi waweza kufanya kazi yoyote kwa elimu ya kozi yoyote.

Kufanya kazi yoyote kwa elimu ya kozi yoyote? Nyie ndiyo mnaoweka watu wa sociology kwenye uhandisi wa barabara.
 
Njooni tufuge kuku,hivi kufuga kuku kunahitaji degree au diploma? unapata mafunzo kidogo ya ujasilia mali unasonga mbele,najua wengi wataulizia mtaji,nami najibu ulipata wapi mtaji wa kusoma? utasema nilisomeshwa, aliyekusomesha hawezi kukunyima msaada wa kujikwamua kimaisha kama una wazo chanya,labda unasema aliyenisomesha amekufa,nami nakuuliza nani yatima kati yako uliyehitimu masomo na kitoto kisichojua hata kikiambiwa mzazi wako kafa kinacheka hakielewi,Ebu funguka macho kutoajiriwa siyo kufa.Tafuta la kujishughulisha nalo
mengine yatafuata.Wengi kinachowaponza ni aibu,acha aibu kijana piga kazi halali inayoonekana mbele yako

hakuna kazi utakayofanya ikuingizie kipato ishushe elimu yako,msomi ni msomi hata akikaanga chips atazikaanga kisomi, Changamka acha kulala.
 
Back
Top Bottom