Usiipite hii post tafadhali...hebu ichungulie

Usiipite hii post tafadhali...hebu ichungulie

Wadau mm nina umri wa miaka 26 now, nimemaliza Sheria Chuo Kikuu Mzumbe ila sijabahatika kupata kazi bado. Imetokea nimependana sana na dada mmoja ambaye ni Kaimu Mchumi wa Halmashauri fulani ya Mji, tatizo ni kwamba ana umri wa takribani miaka 35 sasa, na wkt namuapproach moja ya sababu iliyopelekea asite kunikubalia ni age difference ila at last nikafanikiwa kumshawishi...washkaji na kaka zangu wananionea wivu sana wanadai huyu dem ananilea na kuna tetesi kwamba anapata mshahara mkubwa sana coz ameajiriwa zamani na ana masters degree.

Mara nyingi nalala kwake, nimebahatika kumiliki usafiri(gari) mapema so nikiamka nampeleka kazini asubuhi then narudi zangu maskani. Juzi kati nikamuuliza kwa kumtega kwamba nataka anipe mtoto akakubali! Jana nikamwambia nataka nimuoe akakubali! Ana uzuri wa kawaida tu ila ni mstaarabu sana, muwazi, hana mambo mengi na ananiheshimu sana ingawa kanipita umri! Nafikiria kumuoa mara tu nikipata kazi, je kuna tatizo lolote hapo wajameni?

umependa ila tatizo umri na umechanganywa zaid na tabia yake njema,nakushauri oa kwan tunatafta sana wanawake wenye tabia njema km hao hatuwapati,kwan wapo adimu sana siku hiz,ila usisahau kuchunguza historia yake labda kaficha makucha au amejifunza makosa na amebadilika kwel au kweli ni mke mwema


 
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.

ila wewe!!nimecheka mbaya
kijana oa tu usiulizeulize si ulimpenda mwenyewe?sasa cha kuja kutaka tukupe uamuzi wa kuoa uyo dada uliemtaka mwenyewe na umri wake ni nini?

mie uwa siwaelewi kabisa watu dizaini yako,mapenzi ya kwako afu ukitaka kuchukua uamuzi mzito kama huu katika maisha yako eti unakuja apa jf!!apa tutakutisha tu

grow up boy!!
 
swali la busara la kujiuliza mkuu ni kwamba kwann ana umri wa miaka 35 na hajaolewa? pia kama aliwahi kuolewa kwann aliachika na hujaeleza kama ni MJANE, take care bro magonjwa mengi
 
Kwa thread hii umeonesha hujiamini na hufai kuwa na familia
'
Kama ungekua unajiamini usingekuja hapa,kusema unaonewa wivu ni dalili ya kushindana na woga ulio ndani mwako
'
Pia kelele za rafiki zako zinakuchanganya sana
'
Halafu inaonekana vitu vya huyo dada ndo vimekuchanganya zaidi maana hapa hujazunguzia chochote kuhusu hisia wala mapenzi yako kwa huyo dada
'
I feel sory for her!
 
umri si tatizo kama tu unahisi anavigezo ambavyo wewe unavihitaji kaka! ila tafakari kwa makini ndipo uchukue maamuzi!!!!
 
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.
huna adabu kweli mwambie aseme shikamoo mama;;;hiyo miaka alioandika kakuheshmu tu mkuu hao ndio vijana wetu ooh
 
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.
Mtu unaye lala naye hawezi kuwa mama yako, shangazi yako, wala dada yako !Mwanamke yeyote usiye na nasaba naye basi aweza kuwa mkeo, bila kujali umri !Hakuana mwanamke yeyote asiye na nasaba na wewe aweze kuwa na sifa za wanawake wenyewe nasaba na wewe !Umri si kitu, la msingi wakati mwingine kula jambo unaweza kosa kama vile watoto (kama mwanamke amepitisha umri wa kuzaa) kwani hata Bi Kidude ni halali kumuoa na akawa mke !Hawezi (Bi Kidude) kuwa Mama yako wala Bibi yako !
 
Kwa thread hii umeonesha hujiamini na hufai kuwa na familia'Kama ungekua unajiamini usingekuja hapa,kusema unaonewa wivu ni dalili ya kushindana na woga ulio ndani mwako'Pia kelele za rafiki zako zinakuchanganya sana'Halafu inaonekana vitu vya huyo dada ndo vimekuchanganya zaidi maana hapa hujazunguzia chochote kuhusu hisia wala mapenzi yako kwa huyo dada'I feel sory for her!
Maneno msumari !
 
Ingia uwanjani kwanza uanze kuicheza ngoma ndio ujue utamu wake. Dogo kupishana umri sio shida, ila that is too much....hapo mimi sikushauri kabisa yani 26 kwa 35?
 
Chukua jiko ww, umri ni namba tu kama namba zingine

Ni namba tu kweli ila hazipo bure, kuna kitu zinawakilisha mkuu.....hata gia namba moja na namba tano zote ni namba tu lakini zinatofautiana kiutendaji....
 
Muoe tena haraka sana umebahatika umri si tatizo simama nafasi ya mwanaume kweli mwenye mamlaka ili ushushe umri wake hapo ni kujiamini na kusimamia misingi ya maisha kama mwanaume ukikalia umri hapo atakuona huna lolote kuwa kiakili sasa.
 
Hiyo gari kanunuliwa na mwanamke huyo kaka ni gigolo mbona asiwasumbue huwa analenga wa kumtokea
 
Kumuoa hakuna tatizo ingawa kwa heshima na maadili yetu ya kiafrika, unatakiwa uwe unakumbuka kumpa "shikamoo" yake kila asubuhi maana ni dada yako mkubwa.

dahhh..nimecheka saana usiku huu..ni kicheko cha kwanza kwa ijumaa hii..you started my day
 
Gigolo wewe umefata mali zake unataka kutelezea life kwa mdada wa watu acha hizo kwanza rudisha gari ulilosaidiwa unamiliki gari kazi huna we mwizi au gigolo mkubwa wewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom