Usifikishe Miaka 60 Bila Kufanya Haya 6

Usifikishe Miaka 60 Bila Kufanya Haya 6

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
749
Reaction score
1,741
Wengi wanapenda kuiongelea miaka 40 Ila Mimi nitakuwa tofauti kidogo
šŸ‘‡
KABLA HUJAfikisha MIAKA 60, HAKIKISHA UMEFANYA MAMBO HAYA 6:

1. Jenga nyumba yako.
Hata kama ni ya vyumba viwili, kuwa na makazi yako mwenyewe kunakupa utulivu, heshima na usalama wa maisha unapostaafu.

2. Weka akiba ya fedha.
Usisubiri upate kipato kikubwa ndipo uanze kuweka akiba. Hata kiasi kidogo unachoweka mara kwa mara kinaweza kuwa msaada mkubwa baadaye.

3. Kuwa na biashara au chanzo cha ziada cha kipato.
Usitegemee mshahara pekee. Biashara, kilimo au uwekezaji unaokuingizia kipato hata kidogo unaweza kukusaidia kuishi kwa utulivu.

4. Pata bima ya afya.
Afya ni mtaji wa maisha. Bima ya afya hukusaidia kupata matibabu kwa urahisi na kupunguza gharama kubwa zisizotarajiwa.

5. Wasomeshe watoto wako ikiwa umejaliwa kuwa nao.
Elimu ni urithi bora unaoweza kuwaachia watoto wako. Wape nafasi ya kujifunza na kufikia ndoto zao.

6. Weka malengo na ishi kwa amani na watu.
Kuwa na malengo yanayokuongoza maishani, fanya kazi kwa bidii, na jenga mahusiano mazuri na watu. Heshima, upendo na mshikamano ni sehemu muhimu ya maisha yenye mafanikio.

Maisha ni safari ya maandalizi. Anza leo kujenga kesho yako, kwa sababu kila hatua ndogo unayochukua leo inaweza kuleta tofauti kubwa baadaye.
 
Miaka 60 ni mingi sana kibongo bongo......Nadhani ukifika 35 uwe ushajenga nyumba maana ukianza kusomesha ngumu sana kujenga ,kodi zinaumiza sana!
 
Miaka 60 kwa mwanaume bado sana n'gombe hazeeki maini ila angalau uwe umejiweka vizuri
 
Yaani mitandaoni kila mtu ni life coach! Ukifungua huku do this,don't do that,ukifumgua kule don't eat this don't eat that! Nawaonea huruma vijana wasio na roho jasiri.
 
Maisha yana full of surprises, kuna wanaoweza kuachieve vyote ulivyosema lakini kwa wengine ni kizungumkuti, kila mtu na fungu lake
Yeah Man sio kila mtu ata_achieve wengine wapo kusaidia wengine kuachieve.

Though inauma if you have nothing to proud off.
 
Miaka 60 ni mingi sana kibongo bongo......Nadhani ukifika 35 uwe ushajenga nyumba maana ukianza kusomesha ngumu sana kujenga ,kodi zinaumiza sana!
Upo sahihi, nakubaliana na wewe Lakini si unajua bongo nyoso? Sasa ushafika 40+ Lakini bilabila😁 ufanyeje ujinyongee???
 
Back
Top Bottom