- Thread starter
- #81
ugonjwa wa kuabudu wakenya hauwezi kuisha.....!!!!!!
Mkuu, dawa ya ugonjwa huu ni nini?
ugonjwa wa kuabudu wakenya hauwezi kuisha.....!!!!!!
Huyu na Vicent Makori nawakubali sana. Ila tusiwe na kasumba kwamba mtu akiwa smart kwenye kazi basi ni mkenya. Wabongo wapo kibao wanafanya kazi very smart. Rafiki yangu ni injinia na ni mtanzania. Yupo Marekani kwenye kampuni kubwa na anawaongoza wazungu kibao chini yake.
Yule dada patner wa Vicent Makori ni Mtz, tena Nyakyusa !
Safi sana mkuu kwa watoto kupenda kuangalia Dira ya dunia kuliko Bongo flava/Movies. Tunasema Fanani ameikonga Hadhira.
Hapo ndipo watangazaji wengi wa sasa wanapokosea...wanasoma udaku na kusahau vitu vingine. Namkubali sana Kikeke.Mama yangu alikuwa wa kwanza kunijengea uwezo wa kuingia katika utangazaji, alikuwa anapenda sana kusikiliza habari za redioni na alinishawishi kufuatilia kila habari iliyokuwa inaendelea duniani, nikawa na uwezo wa kutamka maneno vizuri na kusoma habari, anasema Kikeke
Source: Gazeti la Mwananchi.
"Mimi ni Salim Kikeke, alamsiki"
Hebu tuache utindiga bwana! Unataka kusema Tz shule zote zime-Mulugo? Hata hapa TZ kuna shule nzuri bwana tusijemwua bure Salim, unajuaje kama kamweka kwenye shule za daraja la juu hapahapa TZ?. Tuache hizo wakuu (St. Francis, Feza Boys and Girls, Malkia wa Mitume - Ushirombo, Iterambogo - Kigoma na nyingine nyingi za aina hiyo - naogopa kuonekana mdini hapa).Hivi mtoto wako kusoma Tanzania mzazi kuishi ulaya ndiyo uzalendo?
Hapana huyo uliyemtaja hapo juu ni Mkenya. Anayesemwa hapo juu anaitwa Mwakalyelye (jina la kwanza nimelisahau). Pia kuna mwingine Mkhamiti Kibayasi (Zamani akijulikana kama Mkhamiti Juma enzi zile akiwa Radio Free). Unajua wa-Kenya wamefaidika sana na Kiswahili chetu muda mrefu sasa hivi inaonekana kama tumewakamata, maana wa-TZ sasa ni wengi sana huko kwenye radio za wenzetu. Hata ma-reporters wamekuwa wengi sana akina mimi ni Geooooorge Jogopa DW Dar!, Soud Munete DW Bonn Ujerumani, Zawadi Machibya - BBC (sijui Nairobi) n.kUnamaanisha Ester Gidhui au?
La kwanza ni NDIMYAKE!Hapana huyo uliyemtaja hapo juu ni Mkenya. Anayesemwa hapo juu anaitwa Mwakalyelye (jina la kwanza nimelisahau).