Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Imani ni very complicated phenomena kaka, tuishie hapo kwa leo
UKITAKA KUISHI MAISHA MAREFU ACHA KUWASEMA WATUMISHI VBR, KWANI ULIPO KWENDA KUOMBEWA WAO NDIO WALIKUANDIKIA BARUA YA MWALIKO?NAKUHAKIKISHIA USIPO ACHA HYO TABIA MWISHO WAKO HAUTAKUWA MZURI.BARIKIWA
 
Mtoa mada unaweza ukawa na point lakini umeshindwa kufanya presentation vizuri. And I can only assume hii imetokana na ukweli kuwa umefanya conclusion based on kile kilichokutokea wewe na siyo kile ambacho Mungu anaongea juu ya manabii wa uongo. Manabii wa uongo hawapo kwasababu wewe ulienda kanisani ukatabiriwa mambo mawili tofauti na mtumishi mmoja. Manabii wa uongo wapo kwasababu Yesu alitabiri miaka 2000 iliyopita kuwa watatokea.

Mtu wa kwanza kutabiri kuwa kutatokea manabii wa uongo ni Yesu mwenyewe. Alisema katika Mathayo 24:5 kuwa wengi watakuja kwa jina lake wakisema wao ni Kristo. Lakini kwenye Mathayo 24:24 Yesu anarudia tena kuonya kuwa "watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza hata walio wateule". Kwenye Yohana 5:43 anaendelea kuonya tena kuwa "mimi nimekuja kwa jina langu wala hamnipokei mwingine akija kwa jina lake mtampokea".

Mifano hiyo michache kutoka kwa Kristo ni uthibitisho tosha kuwa suala la uwezekano wa kuwepo manabii wa uongo siyo habari mpya tena. Ni dhahiri kuwa lazima wawepo hata mtu asipotuambia kuwa wapo.

Kitu cha msingi ni kuelewa kuwa huwezi kuwa na NABII WA UONGO kama hayupo NABII WA UKWELI. Yaani neno uongo linatokana na neno ukweli. Huwezi kumwambia mtu anakudanganya kama hujui ukweli unafananaje. Kwa mfano, huwezi kusema simu hii ni FAKE ilihali hujui sifa za kuifanya simu kuwa ORIGINAL ni zipi. Hutaweza.

So Yesu aliposema tujihadhari na manabii wa uongo, alichokuwa anamaanisha wakati huohuo ni kuwa tujifunze ni sifa zipi zinamfanya mtu kuwa nabii wa ukweli. Alikuwa hana lengo la kutufanya kustick na kufocus kutafuta manabii wa uongo popote walipo halafu tuanze kudraw dangerous conclusions kuwa MANABII WOTE NI WAONGO TU, halafu hatufanyi jitihada zozote kuwatafuta wale walio wa ukweli. Huko kutakuwa ni kujidanganya na tutakuwa tunamsaidia Shetani kutupumbaza tu. Hatupaswi kutoa msaada wa aina yoyote kwa Shetani.

Sasa ili usitoe msaada wa aina hiyo kwa Shetani. Yaani ili uache kuhangaika kuishi kwa kutafuta makosa (faultfinding) ya watumishi na uanze kuconcentate on sifa nzuri zinazofanya mtumishi awe NABII WA KWELI, ni lazima uzame kwenye NENO LA MUNGU. Ukijifunza vizuri Neno la Mungu, utajua ni jinsi gani ufalme wa Mungu unafanya kazi na ni sifa zipi zinamqualify mtu kuwa mtumishi wa Mungu wa ukweli. In fact Biblia ina majibu ya matatizo yote binadamu anayokutana nayo kiasi kwamba ukiwa msomaji mzuri wa Neno, itafikia kipindi wala hautahitaji tena kwenda kuonana na nabii ili atatue tatizo lako. NENO la Mungu linatosha kabisa kumaliza matatizo yooooooooote unayokutana nayo makubwa au madogo. Kitu muhimu ni kuamini tu. PERIOD.

Kwahiyo anza leo kusoma Biblia yako kwa utulivu huku ukiomba uongozi wa Roho Mtakatifu ili uachane na habari za kwenda kutafuta msaada kwa manabii--wawe wa uongo au wa ukweli.
Jibu zuri sana, UBARIKIWE
 
S.D.A hapo mkuuu ni amri 10 kwa kwenda mbele. ndio maan mtawatambua kwa sheria na ushuhuda
Wafuasi wengi wa SDA ni wana mizigo ya dhambi kama ilivyo kwa ndugu zao waislamu pamoja na kuonekana ni washika sheria.

Tuwe wakweli kwa kusema kuwa dini haina msaada kwa wanadamu zaidi ya kupotosha kwa kuzichinguza dini mbalimbali
 
Watakuja manabii wa uongo ." Hiyo imeandikwa" makanisa yote yaliyolipuka hivi karibuni ni wa nafki na waizi wa kubwa.
 
nashukuru kuna uzi wa bm pesambiili umekuja kuni support
 
hayo makanisa ni maduka ya watu
 
Wafuasi wengi wa SDA ni wana mizigo ya dhambi kama ilivyo kwa ndugu zao waislamu pamoja na kuonekana ni washika sheria.

Tuwe wakweli kwa kusema kuwa dini haina msaada kwa wanadamu zaidi ya kupotosha kwa kuzichinguza dini mbalimbali
Ni kweli kila mwanadamu ana mizigo, ndiyo maana Yesu akasema njooni kwangu wenye kulemewa na mizigo nami....,
Ni kweli kuwa Dini haikoi mtu!!
lakini ukweli ni kuwa sheria ya Mungu haibadiliki na ni takatifu
tunaokolewa na kwa neema tu ya Yesu. ila sasa hiyo neema ina masharti kidogo tu ( Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.) sasa tuanzie hapo Je twazishika sheria za YESU? Barikiwa mtumishi
 
'Mlima wa baridi', Kanisa la 'ufufuoufufuo na ulazima' , 'fulu kospel chuchi', kanisa la 'mtaalamu wa wake za watu' nendeni tu humu mtapigwa pesa zenu hamponi, mnaishi kwa matumaini HADI KIAMA!
 
Ni kweli kila mwanadamu ana mizigo, ndiyo maana Yesu akasema njooni kwangu wenye kulemewa na mizigo nami....,
Ni kweli kuwa Dini haikoi mtu!!
lakini ukweli ni kuwa sheria ya Mungu haibadiliki na ni takatifu
tunaokolewa na kwa neema tu ya Yesu. ila sasa hiyo neema ina masharti kidogo tu ( Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.) sasa tuanzie hapo Je twazishika sheria za YESU? Barikiwa mtumishi
Wasabato si wanafunzi wa Bwana Yesu bali Musa yule aliyeongoza Israeli.
Usabato na Ukristo ni tofauti ingawa wanajiita wakristo !

Msabato wa Kweli ni mshika siku siyo kama aliyohubiri Yesu bali Musa.
Kati ya Musa na Yesu kwa msabato aliye mkuu ni Musa !

Kwa msabato hakuna kuokoka bali shika siku ya Jumamosi

Kwa ujumla sioni tofauti ya msabato na muislam
 
Kushika siku ya sabato unamaanisha nini? Huoni kama mnaabudu siku badala ya MUNGU?

Ninavyojua wasabato wengi ikifika siku ya jumamosi ndiyo wanajifanya kuvaa ngozi ya mwanakondoo lakini siku zingine hizo ni shida tupu.

Siku zote ni siku za MUNGU na siyo jumamosi tu inabidi utende yaliyo mazuri kila siku na siyo tu hiyo siku ya jumamosi.
 
Mtoa mada usidanganywe na shetani kwasababu ya hao watumishi feki. Uponyaji kwa jina la Yesu upo na hata maandiko matakatifu yanakiri hivyo. Kiukweli kumekuwa na makanisa mengi ya kitapeli yanayojiita ya kiroho. Binafsi baada ya kugundua ujanja ujanja huu mimi na familia yangu tumeamua kusali Kanisa Katoliki tu na kama ni maombezi ni humo humo kupitia Karistimatiki Katoliki Emaus Centre ubungo badala ya kutangatanga na watumishi wa makanisa ya kiroho feki.
sawa kabisa karismatik ni uhakika kbsa kwingine ni utapeli tuu
 
Sikatai kwamba hakuna wahubiri waongo ila kuhusu RC hapo hunidanganyi maana ni weupe ktk mambo ya kiroho maana hata mimi nilikuwa huko ukitaka wahubiri wa kweli nende kwenye hayo makanisaa ya kiroho japo wahubiri wa uongo wako hukohuko na ukitaka mapokeo baki haphapo RC
karismatic moja ya kazi ni hayo maombezi vipi unasema ni uongo una uhakika na unachokiongea??
 
Wasabato si wanafunzi wa Bwana Yesu bali Musa yule aliyeongoza Israeli.
Usabato na Ukristo ni tofauti ingawa wanajiita wakristo !

Msabato wa Kweli ni mshika siku siyo kama aliyohubiri Yesu bali Musa.
Kati ya Musa na Yesu kwa msabato aliye mkuu ni Musa !

Kwa msabato hakuna kuokoka bali shika siku ya Jumamosi

Kwa ujumla sioni tofauti ya msabato na muislam
Mkuu twaweza kujifunza pamoja Maandiko, Hata mimi nilikuwa RC niliamini hivyo kabisa kabisa. tena nilikuwa mkali sana . alakini nilikubali kujifunza biblia. Kama uko tayari Tuanze ili uupate mwanga kama nilivyoupata mimi. Ukiangalia kwa juu juu ulichosema ni sahihi na kinaonekana hivyo, lakini sio hivyo mkuu. Barikiwa sana .
 
Mimi namwamini Mungu aliye hai milele na milele,na wala simwamini mchungaji maana mchungaji pia ni mwanadam tu kama Mimi.
 
Mkuu twaweza kujifunza pamoja Maandiko, Hata mimi nilikuwa RC niliamini hivyo kabisa kabisa. tena nilikuwa mkali sana . alakini nilikubali kujifunza biblia. Kama uko tayari Tuanze ili uupate mwanga kama nilivyoupata mimi. Ukiangalia kwa juu juu ulichosema ni sahihi na kinaonekana hivyo, lakini sio hivyo mkuu. Barikiwa sana .
Wewe hebu acha kujipiga chapuo ati ulikuwa RC..?? Hakuna takataka wa aina yako anaweza kuwa RC.

Unashika Sabato kwani wewe ni Muebrania....

Fallacy!
 
1.Hukujibu swali langu. Nimeuliza je biblia imetoa mwongozo kuwa kanisa la kweli ni Kanisa Katoliki la Mitume?
2.Kwa dhana yako ya biblia ninatofautiana na wewe. Mapokeo yako katika liturjia na miongozo mingine katika dhehebu husika. Hivyo Katekisimu, misale ndogo na misale ya waumini siyo biblia. Vitabu hivi vinahitilafiana na maandiko ya biblia katika baadhi ya maeneo. Kwa mfano Amri Kumi za Mungu katika biblia Kutoka 20:1-17 zinatofautiana na zilivyo katika vitabu hivyo.
3.Kwa habari ya kuomba/kuombewa maandiko yako wazi natoa nukuu chache Mathayo 10:1-8, Mathayo 28:19, Marko 16:15-18. Zaidi sana soma biblia yote ushibe neno la Mungu usitapeliwe. Roho wa Mungu akufunulie katika Jina la Yesu Kristo, Amina.
Ngoja nikae sawa nitakurudia...

Bila Kanisa Katoliki usingeijua hiyo biblia yako japo inavitabu pungufu...
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
hujakosea kusema makanisa yakiroho! ila sema umekwenda katika makanisa ya kiroho ya kishetani! makanisa ya kiroho ya Mungu wa kweli hawafanyi hayo mambo na nimachache mno!
 
Back
Top Bottom