Amini hili mkuu, kumjua nabii wa ukweli au wa uongo kunahitaji muda, kupona ugonjwa sio kipimo chakumjua nabii wa ukweli au uongo, na sio ukienda kuombewa lazima upone pia unaweza kufaa tu, chamsingi omba mapenzi ya Mungu juu yako. kama ugonjwa wako ni wa kufaa kwa mujibu wa Mungu lazima ufe hata ukiombewa na nabii vingenevyo ongea na MUngu mwenyewe msawazishe wewe na yeye.
Kumbuka hukuna tatizo linamkuta mtu pasipo dhambi, dhambi ndiyo kila sababu ya uovu wote. ukikuta uovu wowote umeingia kwako au kwa watu wako au kwa familia yako au kwa ukoo wako, cha kwanza omba toba, mpaka mahusiano yako na Mungu yarudi, usikimbilie kuombewa wakati una dhambi na roho yako inakushuhudia, nabii sio mganga wa kienyeji nae anatafuta connection na Mungu huyo huyo uliyemtenda dhambi ili wewe upone.
Kwa mujibu agano jipya kuponywa kwako hakumuhitaji mtumishi yeyote, kunahitaji roho ya toba na moyo uliotiyari kuacha uovu wako kwenda na Mungu. Kumbuka wewe kwa MUNGU ni muhimu kuliko kitu chochote, akikutaka urudi kwake baada ya dhambi yako, anaondo ulinzi wake ili uovu na taababu vikujie, na kadiri unavyo kuwa mgumu ndiyo vinaongezeka ili uombe toba na akupate tene kwake, dhambi ni uasi kwake, magonjwa na shida ni check and balance ya uhusiano wako na MUNGU. Kwahiyo ukipata shida ujue check and balance ipo kazini.
Kazi kubwa ya watumishi ni
kuutangaza ufalme wa Mungu, na kukuunganisha wewe na Mungu, pia ni kukuonyesha kweli ya Mungu ili wewe uwe na misingi ya kujisimamia. Lakini wengi tumewafanya watumishi kama waganga wa kienyeji na ndiyo maana uovu umekuwa mwingi makanisani, shetani naye amegundua udhaifu wetu wa kushindwa kujisimamia na umetufunga humohumo.
Mambo muhimu kati yako na Uhusiano wako na Mungu.
- Ukiona uovu umeingia kwako tafuta sababu kwanini jambo hili limenikuta wakati huo omba toba kwani wote tumetenda na tunajua hakuna uganga juu ya yakobo wala uchawi juu ya israel, wakati unatafakari na kuomba toba yakufa na kupona, endelea kujitoa kwenye kila mlango wa dhambi. Kumbuka dhambi inayokusonga kwa kasi huo ndio mlango mkubwa. wengine ni uongo, wengine uizi,wengine uchawi, wengine uasherati nk
- Tafuta maarifaa juu ya dhambi na namana ya kuzishinda, tafuta ukuu na rehema ya Mungu juu ya wenye dhambi, soma maandiko na utaona kadili siku zinavyosonga mbele mzigo wako moyoni unapungua na hamu ya kumtafuta Mungu inaongezeka na utaanza kutojali sana juu ya tatizo ulilonalo, kama ulikuwa hulali usingizi kwa sababu ya tatizo utaanza kulala, ili litimie neno lililoandikwa hakika amechukua masikitiko yetu....... na kwakupigwa kwake tumepona (Isaya 53.4-5)
- Ukigundua uhusiano wako na Mungu umerudi anza kuomba tatizo lako likuondoke, na hata ukiomba wengine wakuombee ni sawa kwani uko online, hata ukienda kwa mtumishi akuombee hutakuwa na machukizo moyoni,na roho yako itakuongoza wapi pa kwenda hutakwenda kwa pressure ya ungonjwa bali uongozi wa roho aliyeko ndani yetu, hivyo ni rahisi kwenda kwa mtumishi sahihi, sio kila mtumishi ni sahihi kwa kila tatizo, hiyo ndiyo philosophy ya kwanini wawe wengi,wengine wako vizuri kwa kujenga imani, wengine kuondoa roho za umasikini, wengine magonjwa na miujiza, wengine neno la maarifaa na nk
- Pia fahamu nguvu ya kupona ipo kwetu wenyewe na sio kwa watumishi, ni rahisi mtumishi kutoa pepo na sio kuponya ugonjwa, pepo anakemewa na kuondoka kwa mamlaka, ugongwa huondoka baada ya sababu iliyosababisha kuondolewa na toba na kuomba rehema ya Mungu, japo magonjwa mengine yanaweza kuondoka kirahisi pamoja na mapepo kwani hao ndiyo husababisha magojwa hayo, yaani magonjwa ya uonevu. Lakini magonjwa mengine yapo kwa watu kwa sababu yanahaki kuwepo hivyo ondoa haki hiyo harafu omba rehema ya Mungu uondoke.