Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

mimi wananiboa na hizo sadaka zao yani misa moja wanapitisa kisahani mara tatu!
mara 3 mbona ndogo mkuu?siku hizi baada ya kumaliza kujenga kanisa wamekuja na issue ya kitega uchumi cha kanisa mfano MALL au OFISI ZA KUPANGISHA,lakini mwisho wa siku nyinyi waumini mliochangia hakuna mnachofaidi.
 
siez kuongea mengi lakini nina mashaka kama unamwamini Mungu ama binadamu maana unaposema hata usipoombewa unapona sasa sielewi ulienda kutafuta nini huko maana nahisi ulienda kwa madhumuni ya research si kwa kuombewa so nahisi Mungu aliona imani yako .So usilalamike sie tumepona mengi kaa viuzuri na bwana dunia hii si salama bila Mungu.Mtafute kwa bidii umjue vizuri.
mkuu badea nikagundua hata wao wanacheza na probability tu kuwa kuna watakaopona wengine hakuna, hata wewe kama ulipona ujue ulikuwa kwenye uwezekano wa kupona sio maombi yaliokusaidia
 
Hata kabla ya Yesu, enzi za Manabii, bado Manabii wa uongo walikuwepo, enzi za Musa bado Manabii wa uongo walikuwepo! Hata wakati wa Yesu na mitume wa Yesu, bado Manabii wa uongo walikuwepo! Hata leo, Manabii wa uongo wapo na watakuwepo!

Yesu mwenyewe alisema jihadharini na Manabii wa uongo!

Mleta uzi kumbuka hata ktk mambo ya kawaida kuna bidhaa fake na counter fake! Lkn ukiuziwa fake haina maana genuine haipo, ipo
 
Tafadhali nielekeze nami niende huko..Nawatafuta sana hawa jamaa.
Hata kama upo kwenye Group la wasap niunganishie mkuu.
 
Kinachomponya mtu ni imani yake mwenyewe na siyo walio nje yake ukiamini hata Mimi nakuombea simple tu na unapo
na
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
Mimi si muumini wa makanisa ya kiroho lakini hofu yangu ni namna ulivyokua too general. kimsingi ww inaonyesha ulihudhuria kanisa moja tu tena kwa mtumishi huyo huyo na kama lengo lako lilikua utafiti hudhani kwamba ilikua ni busara kwako kuzungukia makanisa kadhaa ya aina hiyo ili kujustify hoja yako?? vinginevyo ni kama mtoto anaewalaumu mama wa kambo wote dunia kwa kumtumia mama yake wa kambo aliemlea as a sample specimen.......
 
Mkuu kumbuka wao ndio wanatangaza hayo maombezi sasa ukiwa na shida utaacha vipi kwenda
Dhana ya mtu kuombewa ni ya kifisadi.

Omba mwenyewe na asijue mtu, utafanikiwa.
Hao wana msombezi wengi ni matapeli.
Kuanzia kule Efata, Mzee wa Upako,Gwajima, Pool of Sloam, Kakobe, wote hao wana misimamo sawa~kukukamua!
 
Mimi si muumini wa makanisa ya kiroho lakini hofu yangu ni namna ulivyokua too general. kimsingi ww inaonyesha ulihudhuria kanisa moja tu tena kwa mtumishi huyo huyo na kama lengo lako lilikua utafiti hudhani kwamba ilikua ni busara kwako kuzungukia makanisa kadhaa ya aina hiyo ili kujustify hoja yako?? vinginevyo ni kama mtoto anaewalaumu mama wa kambo wote dunia kwa kumtumia mama yake wa kambo aliemlea as a sample specimen.......
Mkuu sikukatazi kuongea hivyo, pia sijaenda kanisa moja, ila kuna siku niliwahi sana hospital wakati wa kusubiri kuna mtumishi mmoja alikuja kutufariji sijui na yeye alikua na mgonjwa pale basi baada ya kuondoka watu wakawa wanafunguka kuhusu hao watumishi nikakumbuka na mimi nilivyohangaika nikajua kumbe siko peke yangu ndio maana nikapata courage ya kuandika hayo.
 
Biblia ni mali na ubunifu wa Kanisa Katoliki...Biblia ipo ku-suit mafundisho ya Kanisa Katoliki kama hujui....Biblia ni mapokeo
1.Hukujibu swali langu. Nimeuliza je biblia imetoa mwongozo kuwa kanisa la kweli ni Kanisa Katoliki la Mitume?
2.Kwa dhana yako ya biblia ninatofautiana na wewe. Mapokeo yako katika liturjia na miongozo mingine katika dhehebu husika. Hivyo Katekisimu, misale ndogo na misale ya waumini siyo biblia. Vitabu hivi vinahitilafiana na maandiko ya biblia katika baadhi ya maeneo. Kwa mfano Amri Kumi za Mungu katika biblia Kutoka 20:1-17 zinatofautiana na zilivyo katika vitabu hivyo.
3.Kwa habari ya kuomba/kuombewa maandiko yako wazi natoa nukuu chache Mathayo 10:1-8, Mathayo 28:19, Marko 16:15-18. Zaidi sana soma biblia yote ushibe neno la Mungu usitapeliwe. Roho wa Mungu akufunulie katika Jina la Yesu Kristo, Amina.
 
Wanaotafuta miujiza ndio wanaolizwa
Mkuu muujiza tofauti na maziongaombwe yanayofanywa kufurahisha watu miujiza tunahitaji sababu kama binadamu kuna mahali tunakwama kutokana na teknolojia yetu ya kimatibabu ilipofikia hivyo tunahaitaji divine intervention sio kwamba tunatafuta miujiza kujifurahisha tunahitaji kama means ya kuishi.
 
Dhana ya mtu kuombewa ni ya kifisadi.

Omba mwenyewe na asijue mtu, utafanikiwa.
Hao wana msombezi wengi ni matapeli.
Kuanzia kule Efata, Mzee wa Upako,Gwajima, Pool of Sloam, Kakobe, wote hao wana misimamo sawa~kukukamua!
hapo nilipo bold ndio secret code yao huwezi jua mpaka uwe na shida.
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
Inaonekana uliamini makanisa ya kiroho na watumishi wake, hukumuamini Yesu Kristo
 
Kwaani kabla ya hapo ulikuwa unaabudi wapi?na kwanini hukuombewa hukohuko kwenye kanisa lako Bwana anawajua walio wake na kama ungekuwa ni mtu uliyekulia ktk Ukristo wala usingesumbuka kuwasema vibaya hao watu ila kwa sababu kuna kitu ulifuata ndo maana huna mipaka zaidi ya kujitafutia laana.Mf.mimi nilikuwa mwislamu na niliokoka baada ya kuombewa wakati nilisumbuka ktk maeneo mengi bila msaada ila kwenye sinta kashifu uislamu hata siku moja maana neno la MUNGU li wazi
 
Neno tu MAKANISA YA KIROHO linatia mashaka,ni neno limebumbwa ili kuvutia lkn kiukweli kanisa ni kanisa,,hayo ni madhehebu,ipo tofauti ya kanisa na dhehebu
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
Pole mkuu. Hayo yamekukuta kutokana na uelewa wako mdogo wa maandiko na Neno la Mungu. Si kila roho itoayo unabii yatoka kwa Mungu. Kumbuka maandiko yako wazi ya kuwa siku zitakuja ambapo watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kiburi. Pia maandiko yamezungumzia kutokea kwa manabii wa uongo
 
Hivi niulize tu. Ni kanisa gani ukienda unaulizwa kama unazifata amri 10 za Mungu, lipo kweli? Make zile amri kwangu mie naamini ndo msingi na ndo uzima, ajabu ukienda kanisani hautakuja kuulizwa juu ya msingi huu wa kiroho. Kinachofanyika kule ni mbwembwe kibao, tusidanganyane, bila ya kuzifata hizo amri, make ndo dira yetu ..uponyaji haupo.
S.D.A hapo mkuuu ni amri 10 kwa kwenda mbele. ndio maan mtawatambua kwa sheria na ushuhuda
 
Kua mwangalifu..
Wengi ni wapiga ramlii,matapeli na wazandiki wapotoshajiii..
 
Back
Top Bottom