Kuna huyu bwana wa Mwanza anajiita sijui nabii Malisa,siku hiyo nyumbani sina kazi nikaona nipoteze muda kwenye tv..anawahubiria waamini kwamba watoe sadaka mpaka ziwaume na kila atakayetoa sadaka yake itarudi kwake maradufu kupitia tigopesa,m-pesa na airtel money sikuamini nilichokisikia nikajiuliza kwanini yeye asiziombee zaka zake zikarudi kwake,na watu wanaamini,muhubiri ibada nzima anasisitiza toeni sadaka toeni sadaka,zinakoenda hapajulikani wala matumizi yake hamsomewi watu hawashtuki tu.mie ni RC tukitoa sadaka zinaelezwa matumizi yake,tukiambiwa mchango kwa ajili ya kuongeza sehemu either darasa la watoto,may be kununua chochote kwa matumizi ya Parokia mahalia tukishachanga tunaelezwa zimetumikaje,salio lililobaki na litatumika wapi na kama mtu una wasiwasi unaruhusiwa kuhoji na mwisho wa mwaka tunasomewa mapato,matumizi,balance iliyobaki siyo watu wanatoa sadaka mchungaji ananunua Hummer anaishi kwenye kighorofa na hamuwezi kuhoji,ukihoji unaambiwa una pepo,nitake kuujua ukweli uniambie nina pepo?hapo juu kuna mtu kasema kwamba Catholics tunasali kwa mapokeo,nakuhakikishia mkuu wewe hujapata kuufahamu Ukatoliki umehadithiwa tu.