Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.

Shida kubwa kwako ninayoina ni kufanya "generalization". Kusema makanisa ya kiroho ni suala la jumla mno. Je uliingia makanisa hayo Dar yote? Je ulienda Arusha na kuyaona yote? Makanisa ya kiroho ni yapi? na yasiyo ya kiroho ni yapi?
 
Hahaha..Hebu wacha kunifurahisha bana...Kama hujui historia ni bora kukaa kimya bana...Utaja aibika mkuu....

Wewe biblia umeijulia wapi..?? Kanisa lilikuwa toka ilipoitwa siku ya kwanza....Halafu ngoja nikupe hii! Unajua biblia imekamilika mwaka 300AD chini ya mtaguso wa Efeso..hahahaha ...

Kama hujui historia kaa kimya utaja aibika...Nikisema Biblia ni mali ya Kanisa Katoliki na maanisha na wala sibabaishi .....

Vipi wataka nikupe historia..

Daah...
Mwambie pia Quran inalitambua tuu kanisa katoliki nasio mengine.
 
Yesu yupo anaokoa na anaponya tena hakuna la kumshinda wapo watu wachache wanaotumia nafasu hii vibaya biblia inasema tumepewa bure tutoe bure
 
Mtoa mada usidanganywe na shetani kwasababu ya hao watumishi feki. Uponyaji kwa jina la Yesu upo na hata maandiko matakatifu yanakiri hivyo. Kiukweli kumekuwa na makanisa mengi ya kitapeli yanayojiita ya kiroho. Binafsi baada ya kugundua ujanja ujanja huu mimi na familia yangu tumeamua kusali Kanisa Katoliki tu na kama ni maombezi ni humo humo kupitia Karistimatiki Katoliki Emaus Centre ubungo badala ya kutangatanga na watumishi wa makanisa ya kiroho feki.
Umenikuna pamoyo!!
 
Mkuu kumbuka wao ndio wanatangaza hayo maombezi sasa ukiwa na shida utaacha vipi kwenda
We toa hela uombewe. Kelele za nini?
Mapadri na wachungaji wakale polisi?
Hio inaitwa kazi na posho.
Upone usipone kikubwa umelipa.
 
Mkuu kumbuka wao ndio wanatangaza hayo maombezi sasa ukiwa na shida utaacha vipi kwenda
Ofcourse mtu Awaye na Shida haki ya Mama unaweza kula Mavi yako ukiambiwa Yanaponya...
 
Soma neno takatifu Na ulielewe... Tatizo mnapenda sana miujiza bila kupata muda wa kusoma neno, Na kuomba katika roho Na Kweli, kufunga Kwa dhati. Acha dhambi uone jinsi MUNGU atakavyokutendea
Wasio na Dhambi Hawaugui au
 
We toa hela uombewe. Kelele za nini?
Mapadri na wachungaji wakale polisi?
Hio inaitwa kazi na posho.
Upone usipone kikubwa umelipa.
mkuu hata kama kazi na posho tunaangalia value of money haiwezekani usanii wao tuulipie ghaama kubwa kiasi hiki.
 
mkuu hata kama kazi na posho tunaangalia value of money haiwezekani usanii wao tuulipie ghaama kubwa kiasi hiki.
Mpinga kristo hajaanza Leo, Kazi yake kubwa ni kwenda kijume na neno la Mungu.

Uponyaji ni imani ya mtu, ukienda kuombewa kama imani yako ni ndogo huwezi pona
 
mkuu hata kama kazi na posho tunaangalia value of money haiwezekani usanii wao tuulipie ghaama kubwa kiasi hiki.
Teh teh teh.
Value for money kwani uko Kwenye sale ya saba saba?
Huko ni biashara kwenda mbele.
We umeshawahi kukutana na Mchungaji maskini kuliko kondoo wake?
Sasa ulidhani huo utajiri walipata kwa kuombewa?
We km hela huna na maombi HUPATI. Na ukiendelea Kulalama hela Hazirudi. Na kupona huponi

Mkiambiwa Mwende Hospitali mnatafuta Shortcuts. Sasa Tulia maombi yafanyike kwa kituo huku Wachungaji wanaendelea kujenga Masaki na Pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
 
Mpinga kristo hajaanza Leo, Kazi yake kubwa ni kwenda kijume na neno la Mungu.

Uponyaji ni imani ya mtu, ukienda kuombewa kama imani yako ni ndogo huwezi pona
Una maana wagonjwa wote wa UKIMWI Hawana Imani?

Acha porojo wewe. Maradhi mengine hata Uombewe na Wachungaji na Maaskofu dunia Nzima Huponi Ng'o.
Mtaibiwa mpk kufa nyie.
 
Dah!! Mungu akusaidie sana tena unahitaji toba ya kweli acha kujarinu mungu,hujaumwa na hukuwa na imani
 
enyi kizazi chenye imani haba mtakosa imani hadi lini????? kwahiyo natural selection ishakupitia, ndo mathara ya kusoma theory nusunusu,charles R.dawrn
 
Back
Top Bottom